Whitesmith
JF-Expert Member
- Aug 12, 2017
- 386
- 517
Ndg wanajamvi habari za jumapili.
Niende kwenye mada moja kwa moja, “Jeshi lijitathimini” ndiyo Jeshi letu kwa macho ya nje limejivika vazi nzuri la uaminifu macho pa Watanzania wote lakini kwa ndani linapokuja suala la Ajira ndani ya Jeshi hasa hili tunaloliona la vijana wa JKT siyo Waaminifu kabisa. Wakuu wetu hawa wajitathimini tena kwanini wanazipoka haki za vijana wetu hawa hasa ambao hawana mahala pakuegemea.
Sakata la “Uasi wa Vijana wa JKT”
Jambo hili litazamwe upya na hawa vijana wasaidiwe hata km siyo ndani ya JWTZ lkn wapewe ajira maana hii ilikuwa ahadi ya Rais wa awamu ya tano. Kuna michezo mibaya sana labda kama Rais Samia hajui atadanganywa. Kabla vijana hawa kuna vijana ambao walishiriki shughuli mbalimbali za ujenzi kuanzia ngerengere, Dodoma nk ambao km ilivyo kwa hawa “Waasi”, wao walipewa ahadi nawakatimiziwa lakini haikuwa rahisi.
Ilianza kama ilivyokuwa kwa hawa “waasi” wakarejeshwa vikosini nakupewa Vyeti vyakumaliza mkataba wakatakiwa kuondoka huku wakipewa maagizo kuwa watatafutwa kukiwa na mabadiliko. Vijana wale wakafanya jitihada za kuwasiliana na uongozi lkn wakapewa maagizo kuwa waondoke hatua ya mwisho wakahangaika kupata mawasiliano ya alikuwa Rais Marehemu JPM wakafanikiwa, wakamweleza kuwa tumerudishwa nyumbani, JPM alishangaa kwann warudishwe wakati taarifa aliyonayo wanafanyiwa mchakato wa ajira na ana list amepelekewa?
Ndipo alipomwagiza Brigedia Mbuge ampelekea list ya vijana walioshiriki ujenzi kuanzia ukuta wa mererani, Ngerengere na Dodoma, uzuri Mbuge alishtuka akapeleka list iliyohalisi ndipo JPM akagundua kuna waliochomekwa. Akaagizwa vijana waliositishiwa mkataba warejeshwe na hatimaye sasa ni Wanajeshi.
Natoa hii historia ili kwa wale ambao hawaelewi figisu zilipopo Jeshini linapokuja suala la Ajira watambue kuwa vijana wale walijua wazi kuwa wanaondolewa kijanja ili wengine wachomekewe. Rais wangu Samia wangalie vizuri hao wakuu na uchukue hatua vijana hawa wanapigania haki zao walioahidiwa na Rais JPM. Pili, Jeshi linaongozwa na binadamu usije fikiria hakuna maovu huku ndani hapana yapo tu.
Linapokuja suala la maslahi huwa kuna misemo kama “Mbanga na Mbuyu” linakuwa na nguvu. Wakuu wetu katika hili siyo waaminifu wala waadilifu wao wanaangalia ndugu zao na watoto wao kwanza linapokuja suala la kuingia Jeshini.
Mjitathimini, Mjisahihishe “Jeshi la Ulinzi Wawananchi wa Tanzania” siyo vizuri kulisha nyumbu yako kwa jasho na damu za wengine