Jeshi letu linaonyesha umahiri wa kupigwa na tofali zama hizi!? Hawaoni wenzao huko duniani?

Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.

Wale walikuwa wanaonyesha onyesho la kufurahisha waliokwenda uwanjani na ukakamavu wao, ile ni sanaa kama sanaa zingine. Hawakuwa pale wakionesha mbinu za kupigana na adui.

Hivi majeshi yetu yanapofanya gwaride ina maana wanatuonesha mbinu yao ya kupigana na adui?

Wacheni kuwa mapunguani.
...Kwani huwezi kufurahisha kwa mbinu za kisasa? Zamani kulikuwa na mazingaombwe ili kufurahisha watu, unakuta mtu anatafuna gazeti weee mwishowe anathema handkerchief, jee Leo hayo yapo? Hiyo issue ya kupasua tofali zamani power mabula yeye alikuwa anapasua jiwe kubwa , achana na tofali ya udongo, na jamaa wala hakuwa mjeda.
 
Kama kweli wawe wanaagiza wananchi wawaletee tofali mtaanu waache kuja nazo! sasa tofali wanaziandaa zinakuja kwa gari la jeshi hizo tofali au tafali!!
 
JF Vilaza ni wengi sana maana wao kila eneo hujifanya wanalielewa. Mambo ya jeshi aseme askari. Kila zoezi lina maana yake kama ungeelewa composition ya jeshi huenda ungepanua uelewa wako. Changia idara ambayo wewe professionary unaielewa.
...Hiyo ungesema miaka ya sabini sawa but not today where everything is on your finger tips..Ila kwa wavivu wa kusoma vitu utawasikia "hayo kaulize huko kwa wahusika" ni unify tuu wa kusoma na kujielimisha unaowasumbua. Ndiyo maana kwenye kurani mola akaelekeza muitafute elimu hata ikibidi kwenda mpaka China.
 
Maonyesho ujinga ule ..fitani wanapasua matofali au ni upumbafu tu umewajaa watanzania? nyie mana jeshi au mna kikosi cha wasomba taka taka .. Nenda kaone majeshi Korea Kaskazini ,Israel na Kwingineko..sio huu ushuzi wa JWTZ
haki ya Mungu Jf Rahaa sanaaa km za Muvini muvini
 
Sherehe za Muungano hazina mvuto kabisa. Ni bora tuwe tunapumzika kama tufanyavyo siku za Nyerere na Karume days. Vinginevyo Rais awe analihutubia taifa moja kwa moja toka Ikulu. Kama vipi yafanyike makongamano ya kujadili kero za Muungano.

Nimekuwa nikifuatilia maonyesho ya mbinu za kijeshi za majeshi yetu kuanzia makomando mpaka jeshi la polisi, hakika hazionyeshi kwenda na wakati.

Katika zama hizi za teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani na kurusha makombola ya masafa marefu... Ninyi mnaonyesha kupigana na matofali na vipande vya mbao? Ni lini utakutana na adui umpige na tofali? Labda kama ni mbinu za kuwadhibiti wapinzani hapo sawa.

Mapambano dhidi ya wahalifu au Vita katika zama hizi yanafanywa kiakili na kiteknolojia zaidi. Mahitaji ya mtu anayeweza kuhimili kupigwa na nondo ama tofali yamepungua sana kama siyo kwisha kabisa.

Wahalifu wengi hawana maguvu ya mwili wala hawatumii nguvu katika kutekeleza mambo yao. Na hata wapiganaji wa zama hizi hawatumii tena magumi wala maguvu kubeba matofali. Kuna vifaa vya kiteknolojia vinavyofanya yote haya.

Niombe mtuonyeshe mambo yanayoendana na mabadiliko ya zama. Onyesheni show za kisasa kama zile za Korea Kaskazini.
Nchi yetu tuko outdated kwa kila kitu, katiba ,elimu,afya,jeshi,hidima za jamii na mengine mengine yooote bado tupo zama za kale za mawe. Na hatuko tayra kukibali maendeleio na mabadiriko ua dunia
 
Unawafahamu M23?
Embu acheni kukuza hili jeshi kwa kipimo cha M23 hao wabeba AK-47 na vibomu vya kutengeneza nyumbani.
Ingekua watu kama Al shabab au Boko haram sawa maaana wale wapo njema kila idara had mizinga wanayo so hao M23 ukiwaona tu km wanaumwa unyafuzi.
 
Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.

Wale walikuwa wanaonyesha onyesho la kufurahisha waliokwenda uwanjani na ukakamavu wao, ile ni sanaa kama sanaa zingine. Hawakuwa pale wakionesha mbinu za kupigana na adui.

Hivi majeshi yetu yanapofanya gwaride ina maana wanatuonesha mbinu yao ya kupigana na adui?

Wacheni kuwa mapunguani.
Ukweli unabaki palepale,tunateknolojia gani ya kisasa?????
 
Watanzania wanataka waone Missile kama za mkorea

Kah! Hizo hatuna ..tuwe nazo tunalinda nini sasa?
...Why not display what happened during muungano? Kwani watu walivunja tofali wakati huo? Nini maana hasa ya kumbukumbu ya huo muungano? Kama kungekuwa na siku ya kuadhimisha vita ya kagera then wakaonyesha yaliyojiri that time hiyo ingekuwa sawa.
 
Umetoa ufafanuzi mzuri japo sentensi yako ya mwisho imetoka nje ya mstari. Tukosoane bila kutumia lugha za kutweza.

Mshereheshaji alikuwa akitoa maneno ya utangilizi kwa kila onyesho mkuu. Kwahiyo kutuambia kwamba wale makomando walikuwa sawa na Yamoto bendi hapo mkuu naomba nikubishie. Ndiyo maana kulikuwa na vikundi kede kede vya burudani. Lengo la maonyesho yao ni kuonyesha umahiri wao.
....Umahiri wao kwenye nini mkuu?
 
Mkuu...

Sitaki kuwatetea kwamba wamefanya vyema sana... Lakini kwenye ukweli tushabikie na kwenye uongo tuupinge.

Ulitaka kwenye uwanja kama ule warushe risasi za ukweli au warushe mabomu ya ukweli kama wapo uwanja wa medani?

Ulitaka waje na mizinga pale au vifaru vizito na wapigane kama wapo uwanja wa medani?

Au hizo ndege zije mule uwanjani na kumwaga risasi na makombora kama wapo uwanja wa vita?

Makomandoo wote duniani maonesho yao yanalingana... Hebu google maonesho ya urusi uone kama komandoo wao "SPETNAZ" hawafanyi haya waliofanya watanzania wetu Leo... Ikiwa urusi yenye technolojia kubwa nayo inafanya maonesho hayahaya ya kuvunza tofali,kupasua mbao na kadhalika,ulitaka sisi tufanye nini?.

Angalia Special Force ya China katika maonesho yao kama hawafanyi hayahaya tuliofanya sisi Leo... Au Special Force ya North Korea kama hawapasui matofali,kupinda nondo na mengineyo.

Maonesho yote ya makomandoo ulimwenguni ulingana kwa kuwa yamelenga kwenye ukakamavu na utimamu wa mwili na akili.

Ebu katazame pia mafunzo ya Navy Seal ya Marekani uone kama hawayafanyi haya... Tena ni magumu zaidi ya haya uwa wanalalishwa baharini na mawimbi yakiwafunika.

Komandoo ni wanajeshi wa kazi maalumu... Sasa unataka akienda kukomboa mateka kwenye guest house aingie na vifaru au drones?... Hapo lazima utimamu wa mwili na mafunzo ya ngumu yatumike.

Kingine msipende kufananisha technolojia ya nchi za wenzetu na yetu... Marekani ina rais wa arobaini na kitu sisi ndio kwanza rais wa tano halafu tunataka tushindanishe technolojia.

Pia yale ni maonesho... Hivyo lazima yabaki kuwa maonesho ile ni 1/10 ya mafunzo alionayo komando.

Lazima jeshi liwe na mipaka ya kuonesha siri zake ili kuavoid kuwa dhaifu kwa adui.

Tuwe wazalendo na nchi yetu jamani.
....Yana uhusiano gani na muungano?
 
...Why not display what happened during muungano? Kwani watu walivunja tofali wakati huo? Nini maana hasa ya kumbukumbu ya huo muungano? Kama kungekuwa na siku ya kuadhimisha vita ya kagera then wakaonyesha yaliyojiri that time hiyo ingekuwa sawa.

State functions/ commemoration huwa zinakuwa hivyo.

Hayo unayoyataka hufanyika Siku ya mashujaa na siku ya kuanzishwa JWTZ.
 
Wanatufunza kuwa Askari jeshi wetu wakikosa Bunduki/kuishiwa risasi huwa wanatumia matofali kupigana vita
I'm joking JAMENI.
 
Back
Top Bottom