Sherehe za Muungano hazina mvuto kabisa. Ni bora tuwe tunapumzika kama tufanyavyo siku za Nyerere na Karume days. Vinginevyo Rais awe analihutubia taifa moja kwa moja toka Ikulu. Kama vipi yafanyike makongamano ya kujadili kero za Muungano.
Nimekuwa nikifuatilia maonesho ya mbinu za kijeshi za majeshi yetu kuanzia makomando mpaka jeshi la polisi, hakika hazioneshi kwenda na wakati.
Katika zama hizi za teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani na kurusha makombora ya masafa marefu... Ninyi mnaonesha kupigana na matofali na vipande vya mbao? Ni lini utakutana na adui umpige na tofali? Labda kama ni mbinu za kuwadhibiti wapinzani hapo sawa.
Mapambano dhidi ya wahalifu au Vita katika zama hizi yanafanywa kiakili na kiteknolojia zaidi. Mahitaji ya mtu anayeweza kuhimili kupigwa na nondo ama tofali yamepungua sana kama siyo kwisha kabisa.
Wahalifu wengi hawana maguvu ya mwili wala hawatumii nguvu katika kutekeleza mambo yao. Na hata wapiganaji wa zama hizi hawatumii tena magumi wala maguvu kubeba matofali. Kuna vifaa vya kiteknolojia vinavyofanya yote haya.
Niombe mtuoneshe mambo yanayoendana na mabadiliko ya zama. Onesheni show za kisasa kama zile za Korea Kaskazini.