Jeshi lawaamuru askari kulipa kwenye daladala


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,873
Likes
8,693
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,873 8,693 280
Jeshi lawaamuru askari kulipa kwenye daladala
Theopista Nsanzugwanko
Daily News; Thursday,July 31, 2008 @00:01

Makao Makuu ya Jeshi ya Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), yamewaagiza wanajeshi wote wanaotumia usafiri wa daladala kulipa nauli kuanzia kesho hata kama watakuwa wamevaa sare, imefahamika.

Agizo hilo limo katika waraka ulioandikwa Jumatatu wiki hii kwenda kwa vikosi vyote vya Jeshi kutoka Makao Makuu (Ngome), unaosema uvaaji sare isiwe kigezo cha kutolipa nauli. Kuanzia mwaka 1990 wanajeshi na askari wengine wamekuwa hawalipi nauli katika usafiri wa daladala Dar es Salaam na kwingineko.

Chanzo cha utaratibu huo ni agizo la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Augustine Mrema aliyetaka polisi wasilipe daladala kwa lengo kusimamia utulivu ndani ya mabasi hayo na katika vituo. Askari wengine, wakiwamo wanajeshi, walifuata mkumbo bila kuwapo amri nyingine ya kuwaruhusu kufanya hivyo.

Waraka unaoagiza wanajeshi kulipa nauli umebainisha kwamba Jeshi halitamvumilia mwanajeshi ye yote atakayehusika katika ugomvi na raia kwa kutolipa nauli.
Akizungumzia waraka huo, Msemaji Mkuu wa Jeshi, Meja Jenerali Alfred Mbowe aliiambia HabariLeo jana kuwa kwa muda mrefu wanajeshi walizoea kupanda mabasi ya abiria bila kulipa nauli hasa wanapokuwa na sare za kazi, lakini haikuwa sahihi.

Alisema ingawa kitendo hicho kilitokana na kusaidiwa na wamiliki wa mabasi, hakuna sheria inayoagiza wanajeshi kutolipa nauli. Jenerali Mbowe alisema katika waraka huo kuhusu daladala umetokana na malalamiko ya wamiliki wa daladala mkoa wa Dar es Salaam kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), wakitaka kila mwanajeshi kulipa nauli.

Sumatra imetangaza kupanda kwa nauli za mabasi nchini kuanzia kesho kutokana na kukua kwa gharama za uendeshaji. Nauli mpya zinaonyesha kwamba kwa umbali mfupi wa hadi kilometa 15 abiria watalipa Sh 300, umbali wa kati wa hadi kilometa 20 abiria watalipa Sh 400 na umbali mrefu wa hadi kilometa 25 nauli itakuwa Sh 500 na umbali wa hadi kilometa 30 nauli itakuwa Sh 600. Nauli mpya ya wanafunzi itakuwa Sh 100.

Jenerali Mbowe alisema wamiliki wa mabasi wana nia ya kuwasaidia lakini hali hairuhusu, hivyo ni vyema wakathamini msaada waliopewa kwa kipindi chote na kuanza kulipa nauli ikiwa wapo katika sare au la. HabariLeo inaendelea na jitihada za kuwatafuta makamanda wa majeshi mengine ya ulinzi na usalama ambayo askari wamezoea kupanda bure kwenye daladala watoe msimamo wao kuhusu suala hilo.

Mapema jana akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Mujengi Gwao, alisema kuanzia kesho kila askari anatakiwa kulipa nauli, akipanda katika basi ikiwa ana sare za jeshi au hana. Alisema kwa mujibu wa kanuni mpya za Sumatra kuhusu leseni za usafiri wa abiria kwa njia ya barabara nchini ya Oktoba 2007, hakuna sehemu inayosema askari hao wasilipe nauli.

Gwao alisema kanuni mpya za Sumatra zilizosainiwa na Serikali zinamtaka kila mtu anayepanda daladala kulipa nauli na wala haikumtenga askari wa jeshi lolote kuwa anapaswa kutolipa nauli akiwa katika sare za jeshi. Alisema kanuni hizo zinasema kuwa abiria yeyote anayekataa kulipa nauli atashtakiwa na adhabu yake ni faini ya kati ya Sh 100,000 hadi 300,000, kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.

Aliwataka makondakta na madereva kutoondoa mabasi iwapo askari yeyote atakataa kulipa nauli, jambo ambalo ni haki yao na hakuna mtu atakayemshtaki kwa kufanya hivyo. Kuanzia kesho kwa kutumia kanuni na sheria, makondakta na madereva watashtakiwa kwa kutovaa sare na vitambulisho pamoja na kila mmiliki kuwa na mikataba ya mshahara kwa makondakta na madereva, alisema
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
9,775
Likes
6,478
Points
280
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
9,775 6,478 280
Tatizo hakuna mfumo "System" iliobuniwa ambapo jeshi hilo na mengine wangekuwa wanamalizana na Sumatra kupitia Wizara husika na wanajeshi wanaendelea kuonekana hawalipi nauli lakini kumbe kila kitu kimekwishafanyika.

Mfumo huo ukiwekwa basi askari wote watakuwa na tiketi za msimu ambazo zinakuwa zimekwishalipiwa na jeshi na ndizo watakazotumia ama kwa miezi sita au mwaka mzima na baada ya hapo kuzi-renew.

Na kabla ya mfumo huo wa nauli ni lazima pawe na mfumo imara wa usafiri au Dar-es-Salaam Transport System kama mfano.
 
BabaH

BabaH

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Messages
703
Likes
7
Points
35
BabaH

BabaH

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2008
703 7 35
Kwanini mnataka wanajeshi wasilipe nauli?
Kwanza hata hicho kipindi nashangaa kwanini waliachiwa wakati sheria ilikuwa haisemi hivyo
Hawa wanalinda usalama gani? wakati wao ndio kila kukicha wanapiga raia, wanauwa watu, wanakodisha silaa, sasa mnataka wapelekwe bure kwa sababu zipi

Pili hawa wanapata mshahara sawa na wafanyakazi wengine, na kila mfanyakazi ni muhimu katika kazi yake, walimu, madaktari nao waende bure?

Hakuna logic hapa ni ukiritimba tuuuuu. walipe kama kawa
 
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Messages
6,920
Likes
7,527
Points
280
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined May 1, 2007
6,920 7,527 280
sasa hatimaye naona haki inatendeka:
Mwanajeshi anafanya kazi na analipwa kwa kazi yake, kwa nini asilipie gharama za maisha yake ikiwemo usafiri?.
mbona hospitalini hawatibiwi bure?, dukani hawapewi vitu bure?, kwa nini iwe katika usafiri?.
Pongezi ziwaendee jeshi makao makuu kwa kuliona hili na kulitolea uamuzi wa busara, japo walichelewa, lakini "it is never too late to do what is right"
 

Forum statistics

Threads 1,237,789
Members 475,675
Posts 29,301,351