Jeshi laidhibiti Myanmar baada ya kumshikilia Aung San Suu Kyi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Jeshi la Myanmar limethibitisha kulidhibiti taifa hilo baada ya kumuweka kizuizini kiongozi wa taifa hilo Aung San Suu Kyi pamoja na wanasiasa wengine mapema hii leo.

Baada ya kumkamata kiongozi huyo kwa saa kadhaa, televisheni ya taifa imetangaza kuwa katika hali ya dharura kwa muda wa mwaka mmoja.

Aung San Suu Kyi, kiongozi wa Myanmar, ambaye chama chake cha National League for Democracy (NLD) kipo madarakani amekamatwa, msemaji wa chama amesema.

Hatua hiyo ilikuja wakati wa mvutano mkali kati ya raia na wanajeshi wakihofia jeshi kutawala.

Katika uchaguzi uliofanyika mnamo mwezi Novemba, chama cha NLD kilishinda kura nyingi lakini jeshi likadai kuwa kura zilikuwa zimeibwa.

Myanmar ambayo inajulikana kama Burma, ilikuwa ikiongozwa na jeshi mpaka mwaka 2011. Kwa miaka mingi, Bi Suu Kyi alikuwa katika kifungo cha nyumbani.

Wanajeshi walikuwa mitaani katika mitaa ya mji mkuu wa Naypyitaw pamoja na mji wa Yangon. Huduma za simu na mtandao zilizimwa katika miji mikubwa wakati televisheni ya taifa inasema kwamba kulikuwa na itilafu za kiufundi.
 
Huyu mama alipewa tuzo ya Nobel kwa kupinga utawala wa kijeshi kwa miaka mingi japo aliwekwa kizuizini muda mrefu.

Ila baadaye aliachiwa na chama chake kushika madaraka ila aliungana na wanajeshi pamoja na baadhi ya mabudha wenye msimamo mkali kwenye kampeni dhidi ya waislamu wa Rohingya ambapo maelfu waliuawa na wengine kuishia kwenye kambi za wakimbizi huko Bangladesh.

Sasa jeshi leo limemgeuka na kuangusha serikali yake, hii inaonyesha ushirika kati ya giza na nuru haudumu.
 
Kiongozi mkuu na wakuu kibao wakijeshi wote wamekamatwa na wamewekwa ndani, inasemekana ni uongozi mbaya. Habari kamili fuatilia, kinachoendela hivi sasa wananchi wamefurahia.
 
Hii technic ya kuzima mitandao ndiyo imekua kimbilio la kuzima hamasa kwa wananchi kwasababu now social media zinatumia sana kuliko runinga.
 
Wakatoliki wa tz uchamungu kwao ni kuchukia waislam
Wewe Ustaadh acha kutulisha maneno ya uongo. Tungekua tuna wachukia, tungewajengea ule msikiti wa kule Chamwino Dodoma?

Si tungewafukuza watoto wenu kwenye shule zetu zinazo ongoza Kitaifa kila mwaka kwenye matokeo ya mitihani mbalimbali! Achilia mbali vyuo vyetu vikuu kama SAUT, RUCU, MWECU, nk. Kote huko mnasoma bila bughudha yoyote ile!
 
Huyu mama alipewa tuzo ya Nobel kwa kupinga utawala wa kijeshi kwa miaka mingi japo aliwekwa kizuizini muda mrefu.

Ila baadaye aliachiwa na chama chake kushika madaraka ila aliungana na wanajeshi pamoja na baadhi ya mabudha wenye msimamo mkali kwenye kampeni dhidi ya waislamu wa Rohingya ambapo maelfu waliuawa na wengine kuishia kwenye kambi za wakimbizi huko Bangladesh.

Sasa jeshi leo limemgeuka na kuangusha serikali yake, hii inaonyesha ushirika kati ya giza na nuru haudumu.
Kwa kitendo cha kuwafukuza wale warohingya kwenye nchi yao bila ya yy kuchukua hatua yoyote ya kivitendo na kuwaacha wakihanya ughaibun kimeonyesha uhalisia wa huyu mama.
 
Wewe Ustaadh acha kutulisha maneno ya uongo. Tungekua tuna wachukia, tungewajengea ule msikiti wa kule Chamwino Dodoma?

Si tungewafukuza watoto wenu kwenye shule zetu zinazo ongoza Kitaifa kila mwaka kwenye matokeo ya mitihani mbalimbali! Achilia mbali vyuo vyetu vikuu kama SAUT, RUCU, MWECU, nk. Kote huko mnasoma bila bughudha yoyote ile!
Hakuna hata mkiristo mmoja Mtanzania anaeweza kujenga madrasa wacha chuo,hizo unazozisikia hizo zifuatilie ili uwajuwage wenyewe na wanasema kama hujui urizia iri upate kuereweshwa.

Yaani era inakotoka ikikatwa basi izo seminari zote zitageuka mazizi ya ng'ombe mbali ya makanisa nayo ni hivyo hivyo , sadaka ikianza kukata tunakimbilia kwenye ubunge kawe mbunge.

Ila hii misikiti unayoiona mbavu za mbuzi ata mtu mmoja anaingia anaswali na kutoka zake afu hakuna kulazimishana kuna kuhimizana,tatizo huelewi hizo tofauti za maneno hayo.
 
Back
Top Bottom