Jeshi la wapiganaji limezidiwa vibaya mno, tunakoelekea litampa adui mgongo.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,882
Kwema Wakuu!

Tathmini yangu inaniambia katika mapambano yanayoendelea Jeshi la wapiganaji limepigwa vibaya mno na Kama Hali itaendelea hivi basi wapiganaji watamuachia Adui Yao mgongo.

Kuna namna nyingi ya kupigana na adui yako lakini namna nzuri zaidi ni kumpiga kiongozi Mkuu, huyo ukibahatisha kumpiga basi umeshachukua robo tatu ya ushindi.

Lakini kama utamkosa vibaya kiongozi Mkuu basi hakikisha unamjeruhi Maeneo nyeti mfano macho ili asione, hata akitoroshwa na majeshi yake lakini hatakuwa na uwezo wa kuona tena,
Kama hiyo haitoshi jitahidi ufanye shambulizi litalomuathiri katika mfumo wake wa kuongea au kufikiri. Hata wakimtorosha atakuwa amekwisha.

Subiri,
Wapiganaji wamekata tamaa, wamekuwa kama vijimbwa Koko vinavyobweka mikia ikiwa matakoni katikati ya miguu.

Sasa nimetambua kuwa kumbe ukitaka haki itawamalaki sio lazima umuondoe Shetani. Hilo ndilo nililojifunza katika mapigano haya.
Nikagundua pia kuwa werevu na wenye hekima wapiganapo hawawaui maadui wote katika vita. Ili wasikose watu wakuwatupia lawama na udhaifu wao.

Wapiganaji wamezidiwa Sana. Vita imewalemea hapa wanatamani adui ahairishe Pambano lakini adui naye kadhamiria(sio kuwamaliza na kuwaangamiza) Bali kuhakikisha wapiganaji wanahenyeka na kuonja joto la jiwe.

Hiyo ndio Siasa na mambo yake.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
We umbwa thread zako za kipuuzi saana! Rubbish mods fulani hii takataka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom