Jeshi la wanamaji Iran lainusuru meli na kuwatia nguvuni maharmaia 12 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la wanamaji Iran lainusuru meli na kuwatia nguvuni maharmaia 12

Discussion in 'International Forum' started by bakuza, Apr 5, 2012.

 1. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jeshi la wanamaji Iran lainusuru meli na kuwatia nguvuni maharmaia 12 [​IMG]

  Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeinusuru meli ya mizigo katika Bahari ya Hindi na kuwatia mbaroni maharamia 12 kufuatia mapigano ya masaa 48.
  Akizungumza mjini Tehran, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran Admeli Habibollah Sayyari amesema meli hiyo ya mizigo iliyokuwa ikielekea Iran ilishambuliwa Machi 26 na Maharamia ambao walichukua udhibiti wake. Jeshi la Wanamaji la Iran lilipokea habari kuhusu tukio hilo, lililojiri kilomita 3000 kutoka maji ya Iran, na kufika hapo mara moja. Makomando wa Jeshi la Wanamaji la Iran walipambana ana kwa ana na maharamia hao ndani ya meli hiyo kwa masaa 48 na hatimaye waliwatia mbaroni maharmia 12 na kuinusuru meli hiyo na wahudumu wake. Imearifiwa kuwa watu wawili wasiokuwa Wairani waliuawa katika tukio hilo. Admeli Sayyari amesema maharamia hao watakabidhiwa vyombo vya Mahakama Iran. Manoari za kivita za Iran zinalinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi kwa lengo la kukabiliana na maharamia. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO limepongeza mafanikio ya Jeshi la Wanamaji la Iran katika kukabiliana na maharamia. :scared::fencing:
   
 2. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa hii ishu USA na Israel roho zao mbaya zitakuwa zinawauma sana...
   
 3. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Ukute waliwatumia haohao maharamia kuwachokoza wairani ilikupima ubavu wa Iran, US na wenzake hawana dogo wale.
   
 4. A

  Aman Ng'oma Verified User

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 930
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Iran ni taifa jingine lile USA na ISLAEL wanalijua hilo.
   
Loading...