Mrengwa wa kulia
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 990
- 3,488
Samaki katema ndoano.
Twende kazi
Mkuu wa shirika la nyuklia nchini Ukraine, Petro Kotin amesema kwamba kuna ishara kwamba wanajeshi wa Russia wanajitayarisha kuondoka kutoka kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia ambacho wamekuwa wakishikilia tangu mwezi March baada ya kuvamia nchini hiyo.
Endapo hilo litatokea, itakuwa mabadiliko makubwa katika vita vya Ukraine katika sehemu za kusini mashariki mwa eneo la Zaporizhzhia ambapo wanajeshi hao hawajabadilisha sehemu wanazoshikilia kwa muda wa miezi kadhaa.
Makombora ya kila mara karibu na kiwanda hicho cha Nyuklia, yalipelekea kuwepo wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa janga kubwa na Nyuklia endapo kiwanda kingeharibiwa.
Russia na Ukraine wamekuwa wakishutumiana kwa miezi kadhaa kwa kurusha makombora karibu na kiwanda cha Zaporizhiizhia, ambacho kwa sasa hakizalishi nshati.
Wanajeshi wa Ukraine waemfanikiwa kudhibithi mji wa Kherson mwezi huu, pamoja na sehemu kubwa ya ukingo wa kulia wa Dnipro na mashariki mwa Zaporizhzhia.
Hata kherson ilianza tetesi hivi hivi.
Source: VOA