SoC02 Jeshi la uchumi wa Taifa(JUT) na ufumbuzi wa maendeleo wa Taifa

Stories of Change - 2022 Competition

Msandawe Jr

Member
Jun 22, 2013
20
34
Maendeleo ya taifa la Tanzania unategemea rasilimali pamoja na namna rasilimali zitakavyo simamiwa.Miaka ya hivi karibuni idadi kubwa ya vijana wanehitimu na wanaendelea kuhitimu katika shule za msingi na sekondari,vyuo na vyuo vikuu ndani na nje ya nchi. Ni jambo la kujivunia kutokomeza adui 'ujinga' na jitihada za kuongeza idadi kubwa ya wasomi wenye weledi wa kufanya kazi.

Rasilimali watu katika nchi yetu imeongezeka kwa kasi kubwa kiasi kwamba kuzizidi nafasi za ajira zilizopo katika nchi na kufanya ajira rasmi kuwa kama lulu.Taifa linahitaji kufanya mabadiliko ya haraka kukabiliana na tatizo la mfumuko wa ukosefu ujira kwa vijana ilikukuza uchumi wa Taifa letu.

Vijana wengi wanakaa mitaani bila ya ajira rasmi kitukinachofany ongezeke la umaskini,mmomonyoko wa maadili,wizi na utapeli n.k. kutokana matokeo ya kukosa ajira rasmi vijana wameshindwa kutumia taaluma na ujuzi wao kutafuta namna bora kuishi na kuzalisha mali katika taifa.Idadi ndogo ya ajira rasmi imesababisha rushwa ,matabaka na upendeleo kuongezeka nakufanya vijana kukatamaa na kuwepo kwa wimbi kubwa la wasomi wanaoishi kwa kucheza michezo ya bahati nasibu ilikujikwamua kiuchumi.Tumefika wakati 'connection ' ni muhimu ili upate kazi kuliko taaluma na uhodari katika kazi. Ilihali haya yote yanatokea idadi ya shule, vyuo na vyuo vikuu vinaongezeka kila kukicha na idadi ya wanaofaulu inaongezeka.

Ili taifa liweze kupiga hatu katika changamoto hii na kutoa fursa za ajira kwa vijana shughuli za uzalishaji mali zinatakiwa kuongezwa kwa wingi hususani kilimo,uvuvi,ufugaji,viwanda,madini,ufundi,teknolojia n.k. Shughuli hizi zitakuchukua idadi kubwa ya vijana na kupunguza uhaba wa ajira hivyo asilimia chache ya vijana wanaobaki wataweza kujiajiri wewyewe.

Vijana wanaweza kujiajiri ijapokuwa kunachangamoto zinazojitokeza kwa mfumo wa nchi mfano namna bora ya kupata mitaji,utaratibu mgumu wa urasimishaji wa biashara pamoja na masoko ya bidhaa baada ya kuzalishwa.Changamoto hizo zikitatuliwa kwa kiasi kukubwa vijana wanaweza kujiajili na kukuza uchumi wa taifa,ijapokuwa baadhi ya changamoto hujitokeza kwa vijana wenyewe hususani usimamiz mbovu wa fedha pamoja na kukosha ushirikiano kati ya vijana.

Taifa kwa kuona umuhimu wa kuwapa vijana mafunzo ya uzalishaji mali na uzalendo limeanzisha mfumo wa jeshi la kujenga taifa (JKT) ili kuwakusanya vijana katika makambi mbali mbali kuwapa elimu ya uzalishaji mali na uzalendo kwa taifa lao. Mfumo huu wa JKT umekuwa na mapungufu mengi ikiwemo kutokuweza kuchukua idadi kubwa ya vijana kwa kuzingatia ufinyu wa bajeti,kutokutoa nafasi ya uwezo wa kujiajiri baada ya mafunzo na kuwafanya vijana kwenda katika jeshi la kujenga taifa kwa lengo la kuajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi badala ya kupata ujuzi na uzalendo kwaajili ya kuijenga nchi.

Suluhisho mbadala kwa kuunda taifa lenye vijana wenye weledi katikakazi zao na uzalendo kwa taifa lao ni kuunda 'Jeshi la Uchumi wa Taifa'

Jeshi la uchumi wa taifa (JUT) ni taasisi ya uma inayojishughulisha na kukusanya vijana wote wa kitanzania wenye umri wa miaka kumi na nane(18) hadi thelathini na tano(35) wenye akili timamu na uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali bila kujali kiwango cha elimu,kabira,dini,historia ya familia wala jinsia.JUT inalenga kutoa mafunzo ya ujasiliamali,fursa za ajira ya muda wa miaka mitatu (3) kuongeza uzoefu katika taaluma kwa vijana wote wenye taaluma pamoja na kutoa mitaji baada ya kipindi cha miaka mitatu ya kujitolea katika kujenga uchumi wa nchi.

JUT inatoa fursa kwa vijana kupata uzoefu wa vitendo kwa muda usiopungua miaka mitatu ya lazima au mitano ya hiari kabla ya kwenda kuajiliwa katika taasisi za serikali au taasisi binafsi au kujiajiri.

JUT ni suluhisho la ufumbuzi wa maendeleo ya Taifa,kama taifa kuwe na mfumo wa kukusanya vijana wote katika kambi za kuzalisha uchumi na kuwapangia majukumu ya kujenga uchumi wa taifa kulingana na taaluma zao na kwa vijana wasio na taaluma yoyote wapewe mafunzo kwa vitendo kisha wapewe nafasi za kufanya kazi za kujenga uchumi kwa kulingana na ujuzi walioupata.

Vijana wote wanapomaliza muda wao wa miaka mitatu ya lazima wapewe mitaji ya kuanzisha biashara pamoja na vibari vy kuilasimisha biashara hiyo,mashirika,taaasisi nal,kampuni zitoe ajira kwa vijana walio katika makambi ya JUT kulingana na mahitaji yao.

Hivyo baadala ya kuwa namfumo wa kuomba ajira kupitia mfumo wa ajira ndani ya sekretariti ya ajira kuwe na mpango wa kuhakikisha kila kijana alieko kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiliamali na ujuzi apate nafasi ya kazi kulingana na taaluma,ujuzi au mahitaji ya wakati huo.

Miradi yote ya nchi ipewe JUT ili wataalamu waliopo katika makambi wapate fursa ya kuongeza uzoefu na kupata kutoa mchango wao kwa uchumi wa Taifa. Mfumo wa usimamizi wa JUT ujengwe katika misingi ya umoja,ushirikiano,uzalendo na haki ili kuongeza hamasa kwa vijana kujitolea kwa wingi kwenye kulijenga taifa lao.

Mfumo wa JUT utasaidia kuwaandaa vijana kwa ushindani wa soko la ajira duniani kwani vijana wote walio katika makambi ya JUT watapata fursa ya kujifunza na kupewa nyaraka zote muhimu kwaajili ya kazi ndani na nje ya nchi.

Kama Taifa tusipo amka mapema kuangalia tatizo hili la mfumuko wa ukosefu wa ajira itafika wakati tutashindwa kutaua tatizo hilo, kama msemo wa waswaaili unavyosema'usipo ziba ufa utajenga ukuta'.
 
Kaka nakuomba inbox please
 
ningeiona mapema ningekupa vote, kuwe na incentive kwa waajiri wanao employ vijana waliopitia JUT itawapa motisha kuchukua vijana,nice topic 👍👍👍👍
 
Back
Top Bottom