Jeshi la Sudan laonywa kuteua Waziri Mkuu bila kushirikisha wadau wa kiraia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Marekani na Umoja wa Ulaya wameuonya utawala wa kijeshi nchini Sudan, kutofanya uamuzi wa upande mmoja juu ya uteuzi wa waziri mkuu mpya baada ya kiongozi wa kiraia Abdallah Hamdok kujiuzulu, katikati ya maandamano ya kuupinga utawala huo wa kijeshi

Katika taarifa ya pamoja Marekani, Uingereza, Norway na Umoja wa Ulaya wamesema hawatamuunga mkono waziri mkuu atakayeteuliwa, iwapo wadau wengi wa kiraia hawatahusishwa

Taarifa hiyo ya pamoja pia imetoa mwito wa kuendelea kwa maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2023 chini ya makubaliano ya kipindi cha mpito, lakini pia kuimarishwa kwa mfumo huru wa mahakama na bunge, huku ikionya hatua ya upande mmoja ya kuteua waziri mkuu mpya na baraza la mawaziri inaweza kudhoofisha uaminifu wa taasisi hizo.
 
Kuna haja gani ya kuzitaja hizo nchi wakati zote zipo umoja wa ulaya?
Si ingetosha tu kusema umoja wa ulaya?
Halafu hawa wazungu ni kweli bado wanatutawala?
Kwanini kutuingikia sana mambo yetu
Au kwasababu ya misaada?
Kwasababu mikopo tunalipa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom