Zanzibar 2020 Jeshi la Polisi Zanzibar limelazimika kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kutokana na viashiria vya uvunjifu wa amani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Unguja. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar limesema limelazimika kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kutokana na uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Limesema waliokamatwa ni waliochoma matairi na kuyaweka katikati ya barabara na waliokwenda katika vituo vya kupigia kura wakati leo wanaoruhusiwa kupiga kura ni makundi maalum wakiwemo askari wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na kuyashambulia kwa mawe magari ya polisi.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Oktoba 27, 2020 na Kamanda Polisi wa Mkoa huo, Awadh Juma Haji wakati akizungumza na Mwananchi Digital.

Amesema mbali ya matumizi ya mabomu hayo, wanawashikilia baadhi ya vijana waliodai kuhusika katika matukio hayo.

Amebainisha kuwa vijana hao wanatuhumiwa kuchoma moto matairi ya magari na kuyaweka katikati ya barabara na maeneo mbalimbali kinyume na sheria, kuyashambulia kwa mawe magari ya askari polisi waliokuwa katika doria huku wakijua kuwa kazi ya polisi ni kusimamia amani na utulivu.
 
..Polisi walitakiwa wasitishe kura ya mapema.

..Vifo vilivyotokea chanzo chake ni kura ya mapema.

..Kwanini Polisi waliruhusu kura ya mapema iendelee wakielewa kabisa kwamba kulikuwa na "viashiria" vya kuvunja amani?
 
Nasikia mtwara imevamiwa na alishababu vipi polisi wetu watakwenda na huko ?
 
mabomu ya machozi vipi kuhusu waliopigwa risasi sasa ikiwa hao wanaofanya fujo,waliojikusanya mnamaliza risasi na mabomu ,hivi mtaweza kuikomboa mtwara ile sehemu kila siku inatekwa.
 
Watuambie maiti zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii nani amewaua wale watu?

Mnachukua muda mrefu kutoa majibu halafu mnakuja na taarifa laini isiyojitosheleza.
 
..Polisi walitakiwa wasitishe kura ya mapema.

..Vifo vilivyotokea chanzo chake ni kura ya mapema.

..Kwanini Polisi waliruhusu kura ya mapema iendelee wakielewa kabisa kwamba kulikuwa na "viashiria" vya kuvunja amani?
Sheria inasemaje kwenye hili la kura ya mapema?.
 
Jeshi haliwezi kushindana na wananchi wake likawashinda...kinachotakiwa hapo ni busara tu.
Wewe ndo ungekuwa polisi alafu vijana wanakulushia mawe, wakati huo wanaharibu magari kwa mawe ungetumia busara gani zaidi ya kuwadhibiti? 🤔

Ikiwa jeshi haliwezi kuwashinda wananchi wake kama usemavyo, Basi msilalamike huku mitandaoni, nendeni mkapambane nao.
 
Sheria inasemaje kwenye hili la kura ya mapema?.

..inawezekana mambo yako vizuri kwenye vitabu vya sheria, ila unapoingia field na kuanza kuitekeleza sheria matokeo yake ndiyo hivyo vifo na vilema kwa wananchi.

..wahusika wangekuwa na busara, na wangekuwa wanayathamini maisha ya Watanzania, naamini wangeachana na zoezi la kura ya mapema.
 
UPDATES: Kwenye tukio la kuuawa watu watatu kwenye kijiji cha Kangagani, jimbo la Ole, kaskazini Pemba, mpasha habari wetu aliyeko kwenye eneo la tukio ametujulisha hivi punde taarifa za waliouawa kwamba wote walipigwa risasi wakiwa majumbani ama vibarazani:

1. Bi Asha Haji Hassan mwenye umri wa miaka 33 ameuawa wakati akitoka nyumbani kwa baba yake kwenda nyumbani kwake. Bi Asha ameacha mume na watoto sita.

2. Yussuf Shaame Muhiddin mwenye umri wa miaka 27 ameuawa wakati akiwa barazani anacheza keramu na wenzake. Hana mke wala watoto.

3. Komba Hamad Salum (maarufu Kipigi) mwenye umri wa miaka 30, naye alikuwa barazani pake wakati alipopigwa risasi na kuuawa. Ameacha mke na watoto watatu.

Kwa upande wa majeruhi, ambapo hadi sasa idadi inayofahamika ni tisa, ni hawa wafuatao:

1. Abbas Haji Nyange (miaka 27), amepigwa risasi wakati akichota maji kwenye mfereji nyumbani kwake. Utumbo umetoka nje, na kwa sasa amewahishwa Hospitali ya Vitongoji.
2. Bakari Khamis Bakari (miaka 55)
3. Mukhtar Yahya Hassan (mtoto wa miaka 16)
4. Khamis Mohammed Mmanga (miaka 40)
5. Hassan Kombo Ali (mtoto wa miaka 13)
6. Abbas Mgau Ali (miaka 22)
7. Mgau Omar Mgau (miaka 35)
8. Hamad Omar Hamad (miaka 20)
9. Ali Hamad Seif (16)

Hadi tunakwenda hewani, bado maiti zote zipo kijijini Kangagani na baadhi ya majeruhi wameshindikana kupelekwa hospitalini kwa sababu ya kutanda maaskari kwenye barabara za kuelekea Chake Chake, Vitongoji na Wete.

Weyani TV itakuwa inakuletea muhtasari wa mwenendo wa mambo kama yanavyojiri na kupokelewa na dawati letu la habari.
 
Back
Top Bottom