Jeshi la Polisi Zanzibar latoa ufafanuzi kuhusu Madai ya kutaka kumkamata Maalim Seif

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Jeshi la Polisi Zanzibar limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa jeshi hilo linapanga kumkamata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandaoni zinasema Maalim Seif anatakiwa kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na kujitangazia ushindi katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 kama inavyoshinikizwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar.

Akiongea na mwandishi wa Dw, Issac Gamba, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishina Mkadam Khamis Mkadam, amesema yeye hajapata taarifa yoyote toka kwa wakubwa wake inayomtaka amkamate Maalim Seif.

Amesema jeshi la polisi ni taasisi kubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, hivyo yaweza kuwa amri kama hiyo imetolewa kwa viongozi wengine


Chanzo: Mpekuzi
 
kama akikamatwa na kupelekwa mahakamani maana yake kosa lile linahukumu yake na sio kufuta uchaguzi .hapa watajichanganya tena sasa ivi na wata.pa point zaidi maalim seifu .

Ilitakiwa maalim akamatwe siku ile ile na sio kufuta uchaguzi .
 
Nashangaa aliyefoji zuio la mahakama yuko huru wakati ni kosa la jinai.Na wasio na hatia wapo ndani.Duh hakika bila haki hakuna amani
 
Back
Top Bottom