Fredwash
JF-Expert Member
- Oct 27, 2009
- 1,041
- 1,375
jaman naomba wajuze wa mambo mtujuze.. je hii sheria ya pf3 kwel haijapitwa na wakat...
kwangu mm naona ilitakiwa walau wailegeze kuwa mtu atibiwe lakin kila hospt iwe na free toll call kwa vituo vya polis wakipokea mgonjwa wanamtibu wakat huo huo wanatoa taarifa zake kamil kwa polisi.. kwa maana ya jina, umri, anapoishi, alivyoumia then haruhusiw kutoka bila hiyo pf3, yaan ndio itumike wakat wa kumdischarge, la sivyo watu watakuwa wanafia mapokez ama eneo la tukio kisa hawez pelekwa hospt bila pf3
===============
Chanzo: ITV

Jeshi la Polisi Zanzibar latoa onyo kwa hospitali zinazotibu watu walioumia bila PF3.
Jeshi la Polisi Zanzibar limepiga marufuku na limesisitiza kuwa litawachukulia hatua za kisheria madaktari na hospitali ambazo zinawatibu watu waliojeruhiwa au kuumia bila ya fomu ya polis-PF3 huku ikisema haina uhusiano wowote na vikundi vinavyoitwa Zombie.
Kauli hiyo ya polisi imetolewa na naibu mkuurgenzi wa upelelezi na makosa ya jinai Zanzibar naibu kamishna Salum Msangi wakati akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo hapa Zanzibar ambapo amesema pamekuwepo na baadhi ya wahalifu wamekuwa wakitiwa na madaktari bila ya utaratibu hali ambayo inahatarisha jamii hivyo amesema polisi iko makini itachukua hatua.
Akizungumzia malalamiko ya kuwepo kikundi kianchitwa Zombie ambacho kinalalamikiwa kuwapiga wananchi kamishna Msangi amesema polisi haina taarifa yeyote yakuhusika na kikundi hicho na kuwataka wananchi kutoa taarifa polisi wanapokutana au kupigwa na kikundi hicho kwa vile hadi sasa hakuna taraifa yeyote polisi inayuhusu kikundi hicho.
Mkuu huyo wa upelelezi Zanzibar pia ametahadharisha watu walioanza kupeperusha vipeperushi vya kuhatarisha amani huku pia akisisitiza jeshi hilo lemejipanga kuhakikisha usalama na amani inakuwepo wakati wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar Machi 20.
Chanzo: ITV