Zanzibar 2020 Jeshi la Polisi Zanzibar laanza mazoezi ya utayari kukabiliana na maandamano na wavunjifu wa amani

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
96,020
2,000
Kwa mujiu wa ITV, Jeshi la PolisI Zanzibar limefanya mazoezi ya kupambana na waandamanaji.

Hiyo inakuja siku chache baada ya Maalim Seif kuapa kuwa safari hii hakuna atakayekubali kuchakachuliwa kwenye matokeo ya kura.

Naona ngoma imeanza kulindima kila sehemu.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,386
2,000
Inasikitisha sana makamanda wa jeshi la polisi wanasema wazi kuna baadhi wanasiasa wameanza kutoa kauli, huenda wanalenga kauli za Maalimu Seifu kusema kufuatia dhuluma kuenguliwa wagombea ACT Pemba na kwingineko.

NEC na ZEC watoe haki Watanzania tufanye maamuzi katika sanduku la kura. Polisi ,mabomu,risasi na mabavu vitabomoa zaidi amani na umoja wa taifa letu.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
96,020
2,000
CCM inaangamia kwa viongozi wake kukosa maarifa!

Ya 2001 yanaweza kujirudi na safari hii yanaweza kuwa worse but they should know that the world is watching.

Bara nako ni swala la muda tu maana walioenguliwa mpaka sasa hatima yao haijulikana.
Nawaonea huruma hao viongozi watakavyo kuwa wanasota pale the Hague

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,037
2,000
Naona amekwenda Zanzibar kuchochea vurugu Badala ya kuleta Amani, Huyu IGP ana kasoro nyingi sana....imagine anafika kule neno lake la Kwanza ni kwamba nimekuja kuwaambia "nitawagonga", huyu ni mzima au ana mental disorder flan hatuielewi?

Nadhani Huyu IGP pia ndo aliyeanzisha kitu kinachoitwa Jeshi la Akiba ambacho kimesambaratishwa na Lissu jana, Naomba Mamlaka zimwondoe Sirro Unguja na Pemba haraka ataleta maafa!
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
96,020
2,000
Naona amekwenda Zanzibar kuchochea vurugu Badala ya kuleta Amani, Huyu IGP ana kasoro nyingi sana....imagine anafika kule neno lake la Kwanza ni kwamba nimekuja kuwaambia "nitawagonga", huyu ni mzima au ana mental disorder flan hatuielewi?

Nadhani Huyu IGP pia ndo aliyeanzisha kitu kinachoitwa Jeshi la Akiba ambacho kimesambaratishwa na Lissu jana, Naomba Mamlaka zimwondoe Sirro Unguja na Pemba haraka ataleta maafa!
Mwache maana kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,027
2,000
Wazanzibar siyo watu wa kuogopa virungu, mabuti ya polisi au risasi. Wao wanaamini wakifa huku wanatetea haki wanakwenda peponi sasa chagua mwenyewe uko tayari kuua wangapi ili kupora haki yao au la basi wape haki yao hutoona unywele wa mtu hata mmoja ukiguswa!
Serikali ndo inawapelekea fujo Wazanzibari
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom