Jeshi la polisi wilayani Iramba- Singida lawasweka walimu wawili wa kiume mahabusu kwa kuhisiwa kutembea na mwanafunzi.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
Habari zenu wana JF.

Kwa habari za uhakika nilizopata kutoka kituo cha polisi Kiomboi huko wilayani Iramba ni kuwa Jeshi letu la polisi linawashikilia walimu wawili wa kiume wa shule ya Sekondari Kizaga kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na mwanafunzi wa kike shuleni hapo.

Inadaiwa mwanafunzi huyo aliwataja walimu hao kuwa aliwahi kulala nao kwa vipindi tofauti. Kisa hiki kilikuja baada ya mwanafunzi huyo kukumbwa na mkasa mwingine wa kimapenzi hivi karibuni ambapo ktk kuhojiwa aliambiwa awataje wanaume wote aliowahi kutokananao kimapenzi.

Hatima ya walimu hao bado haijulikani na kwa taarifa zaidi ni kuwa walimu wawili wa kiume waliwahi kufukuzwa kazi shuleni Kizaga kwa tabia hizi hizi.

Nitazidi kuja na updates kila nipatapo yanayojiri ktk sakata hili.
 
Back
Top Bottom