Jeshi la Polisi:Waziri wa Mambo ya Ndani Jiandae kung'oka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la Polisi:Waziri wa Mambo ya Ndani Jiandae kung'oka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, May 9, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Wana JF,

  Baada ya kimbunga cha Bungeni hivi majuzi cha kutokuwa na imani na PM na kupelekea Rais kulifuma Baraza lake la Mawaziri naona kumetulia na tunangojea output ya hawa wateule wapya na wa zamani.

  Jicho langu nataka kulielekeza zaidi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Emmanuel Nchimbi aliyehamia toka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Mkuu wa kaya ameshaonya kuuwa kwa sasa haitakuwa tu kujiuzulu kwa Waziri mhusika pindi madudu yanapobainika chini ya Wizara anayoiongoza.

  Napenda nimwase Mhe. Nchimbi kwamba kama hatachukua hatua za makusudi kuondoa HUU UTENDAJI MBOVU WA JESHI LETU LA POLISI basi very soon hii kitu itamgharimu. Itaweza kumgharimu kama ilivyotokea kwa Rais mstaafu ALI HASSAN MWINYI enzi za Mwalimu kwa aidha kuiuzulu mwenyewe kwa hiari au kwa kulazimishwa.

  Utendaji mbovu wa Jeshi la Polisi Tanzania uko dhahiri kwa kila Mtanzania mpenda HAKI,AMANI NA UTULIVU. Jeshi la Polisi wamekuwa ni VIBARAKA WA CHAMA TAWALA. Wako pale kutetea maslahi ya CCM kwa gharama yoyote hata kama ni KUPOTEZA UHAI WA RAIA HASA WALE KUTOKA UPANDE WA UPINZANI.

  Matukio yaliyojitokeza kabla,wakti na baada ya Uchaguzi Mkuu 2010 yanaonyesha kuwa Jeshi let la Polisi halifanyi wajibu wake ipasavyo.Maandamano ya Arusha yalisababisha umwagikaji wa damu pasi na sababu za msingi. Kamata kamata za Wabunge na Wafuasi wa vyama vya Upinzani zimekithiri na hasa uoande wa CHADEMA.Tumeona kule Arusha,Mwanza,Songea,Tarime,Igunga na maeneo mengine KWAMBA POLISI WANATUMIA NGUVU KUBWA SANA YA KUDHIBITI MAANDAMANO YA WAPINZANI MPAKA WANASABABISHA VIFO KWA RAIA. Tumeona WABUNGE 2 WA CHADEMA KULE MWANZA WAKIPIGWA NUSURA YA KUFA CHINI YA USIMAMIZI WA JESHI LA POLISI NA HAKUNA HATUA ZOZOTE ZINAZOCHUKULIWA NA IADHA IGP,WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AU RAIS MWENYEWE.

  IGP MWEMA NA WAZIRI ALIYEONDOKA VUAI NAHODHA WAMEONYESHA UDHAIFU WA HALI YA JUU KWA KUSHINDWA KAZI! Baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri nataka kupeleka salamu kwa Waziri wa sasa wa Mambo ya Ndani na Naibu wake kuwa haitakwa business as usual kama ilivyozoeleka. Watu hasa wa CCM wasifikiri kuwa wajibikaji ni pale tu Wizara inapoonekana kutokeza kwenye ripoti za Mkagauzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG).

  Kama Polisi wanaua Raia wasio na hatia kwa kisingizio cha Maandamano ya Wapinzani basi wajiandae kung'oka. Hatutakubali kuona Watanzania wakiuawa na Polisi kwasabu tu wapinzani. Kama PM atashindwa kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani basi KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAYE BADO IPO BUNGENI,HAIJAFUTWA! Kwa hiyo tunaomba tu kwa IGP Mwema asije akamharibia bosi wake kwa kulea ujinga unaofanywa na Polisi wake.

  Kwa kuanzia namtaka Waziri wa Mambo ya Ndani aanze na wale Polisi waliohusika na kupigwa kwa Wabunge wawili-2 wa CDM.Tunajua hawa Polisi wanajulikana kwasabu Polisi anayekuwa kwenye lindo anajulikana kila siku. Lakini kwa makusudi kabisa hawa Polisi mpaka sasa hawajakamatwa! KULINDANA KUKO PALEPALE KWA VILE WALIPOIGWA NI WABUNGE WA CHADEMA. JE,INGELIKUWA WABUNGE WA CCM WAMEPIGWA NA KUUMIZWA NI WANACHADEMA WANGAPI WA CHADEMA WANGELIKUWA WAKO MAHABUSU NA KESI MAHAKAMANI?

  Mkifanya mchezo mtakuwa mmekalia kuti kavu. Anytime litaanguka pamoja na wewe mwenyewe na naibu wako.
  Kazi kwako Mheshimiwa Nchimbi Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu wako.
   
 2. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  umenena mkuu. wakilianzisha wasitazamie kulizima!
   
Loading...