Jeshi la polisi, viongozi wenye fikra dhaifu Tz - Jifunzeni toka Afrika Kusini

UJANJAUJANJA

JF-Expert Member
Oct 14, 2012
226
122
Ndugu zangu wana JF,

Nawasalimu.

Katika kutafakari yanayojiri nchini mwetu, hali ya kisiasa na usalama,leo nimeitumia siku yangu tangu asbh kuiangalia tena filamu ya Sarafina. Sote, au wengi wetu tunafahamu ni filamu inayoelezea harakati za ukombozi nchini Afika ya Kusini.Katika filamu ile,vyombo vya dola vilitumia nguvu kubwa sana kudhibiti umma wa wananchi ambao ulikuwa ukiyahitaji mabadiliko kwa hali na mali,pamoja na nguvu zote hizo kutumika na kupelekea kupotea kwa maisha ya wengi waliyoyapigania mabadiliko hayo,hatimaye uhuru wa kweli wa wana wa afrika ya kusini ukapatikana,nguvu ya umma ikashinda ngubu ya vyombo vyote vya usalama.

Katika kufuatilia yanayojiri nchini Tanzania kwa sasa, ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa nguvu kubwa na rasilimali kubwa sana za nchi zinatumika katika kuidhibiti Chadema pamoja na wafuasi ana wapenzi wake. na kwa hali ilivyo sasa, chama hiki kimeonekana kuwa mwiba mkali sana kwa CCM kuendelea kuwepo madarakani. Silaha pekee waliyonayo CCM sasa ni kutumia nguvu za vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kujihalalishia kuwepo madarakani. Mauaji yanayofanywa na vyombo vya uslalama kwa raia wanaopigania mabadiliko pamoja na mateso yanayofanywa kwa wapigania haki,ikiwemo kuwabambikizia kesi zisizo na kichwa wala miguu,ni ishara zinazoanza kuionesha ile nuru ya ukombozi halisi wa Mtanzania.

Navishauri vyombo vya usalama vifanye kazi yake kwa kufuata sheria na si chama kilichopo madarakani,wachukue muda kuiangalia filamu ya Sarafina ili watambue kwamba yote wayafanyayo yana mwisho na ni heri wakaacha siasa ifanywe tu na wanasiasa. Nguvu ya umma siku zote hushinda nguvu za majeshi yote. Tuiangalie tena filamu hiyo na itufundishe kitu. Tutumie akili zetu kufikiri na kutenda
 
Hoja nypesi sana mkuu ni kimajungu tu na unazi wa kisiasa.

tumia mda kutafakari halafu uje tena.
 
Hoja nypesi sana mkuu ni kimajungu tu na unazi wa kisiasa.

tumia mda kutafakari halafu uje tena.

Mkuu Simiyu Yute, jidanganye tu,wahenga walisema "Changes are inevitable". It is just a matter of time, let us pray we all be blessed to see that day and you will remember what I had just intimated today.
 
Mimi ninafikiri aliye anzisha majeshi duniani alifanya research kubwa kuhusu jinsi ya kuwawekea binadamu saikolojia ya mbwa na alifankiwa kufanya hivyo.

Kama mtu mmoja peke yake anasima anasema kamata wao mkia ukiwa juu wanakama nafikiri niko sahihi.

Tuhitaji jeshi la kulinda raia na si kulinda wezi selikalini.
 
Nilidhani I was alone doing that kumbe wengi. Kinachonishangaza ni uhusiano wa Kauli za viongozi wa makaburu na wa kwetu. Wao wanasema they are looking for trouble makers and the boers also kept on saying similar words. Unapokuwa na tatizo na wananchi wasikilize badala ya kutafuta mchawi kwamba anawachochea kufanya vurungu. Tafuta sababu zinazowafanya wawe waliko sasa badala ya kufikiri kuwa wapo kule kwa sababu kuna mtu anawashawishi kukataa serikali Yao
 
. Nilidhani I was alone doing that kumbe wengi. Kinachonishangaza ni uhusiano wa Kauli za viongozi wa makaburu na wa kwetu. Wao wanasema they are looking for trouble makers and the boers also kept on saying similar words. Unapokuwa na tatizo na wananchi wasikilize badala ya kutafuta mchawi kwamba anawachochea kufanya vurungu. Tafuta sababu zinazowafanya wawe waliko sasa badala ya kufikiri kuwa wapo kule kwa sababu kuna mtu anawashawishi kukataa serikali Yao


Ndugu yangu Mghaka,

Nakubaliana na wewe, yaani nafikiri pia ni muhimu kwa viongozi wetu pia kuiangalia tena filamu hiyo halafu kisha wafanye "reflection" of what they are doing and saying with what was done and said by the boers in South Africa, for sure changes are inevitable, they are just delayed
 
Hoja nypesi sana mkuu ni kimajungu tu na unazi wa kisiasa.

tumia mda kutafakari halafu uje tena.
Hapa unatakaa kwamba vyombo vya dola havikutumika kuwadhibiti wapigania Uhuru Afrika Kusini au unapinga kwamba vyombo vya dola havitumiki kuwadhibiti wapinzani Tanzania? Jaribu kuutafuta huo mkanda wa Sarafina alafu utafakari huko upande gani. Shame on you
 
Hapa unatakaa kwamba vyombo vya dola havikutumika kuwadhibiti wapigania Uhuru Afrika Kusini au unapinga kwamba vyombo vya dola havitumiki kuwadhibiti wapinzani Tanzania? Jaribu kuutafuta huo mkanda wa Sarafina alafu utafakari huko upande gani. Shame on you
Vyama vya upinzani vinajidhiti vyenyewe kwa kukosabdira na mwelekeo badala yake vinakuwa wafanya vurugu
 
Aisee kuna mwenyekiti wa CHADEMA kule Makete kabambikiwa kesi ya uzushi na polisi na amefungwa miezi tisa(9).Jamani CCM ni hatari tusipoangalia tutashindwa hatutaeleweka kwa raia wetu!
 
Waafrika kusini wakati sio watumwa tena wa Kifikra linapokuja suala la uzalendo. Wanaandamana kwa nguvu zote kumshambulia Obama alipoingia nchini mwao. Wameandika mabango ya kupinga siasa za Rais huyo, wanakataa Afrika na waafrika kufanywa vinyago wasio thamani mbele ya wazungu.

Lipo funzo kwa viongozi uchwara wa hapa Tz pamoja na jeshi lao la polisi linaloendekeza fikra butu na mpindo za viongozi hao. Picha niliyoiambatanisha hapa haionyeshi dalili ya mabomu ya machozi, magari ya maji washa na magari ya delaya kama ambavyo wangeandamana Watanzania kwenye ujio wa bwana mkubwa Obama. Tunatishwa ili tusieleze fikra zetu juu ya hali ya mambo. Hii ya Afrika kusini ndio demokrasia ya kweli.

Tanzania.... Fikra huru bila mabomu inawezekana!!!
as.jpeg
 
Polisi wa Tanzania ni watumwa wa watawala! Hata siku moja hawajawahi kutumia weledi wao katika kusimamia haki za kikatiba za wananchi!

Polisi wamesahau kuwa wao ni walinzi wa raia na mali zao na badala yake wanadhani ni walinzi wa CCM na sera zake!
 
Hujakatazwa kuchora bango na kulinyanyua wakati wa ziara ya Obama.
Wewe liandike tu tena nakushauri iwe kwa lugha atakayoielewa mradi usitukane kukashifu wala kutoa manaeno yasiyofaa wakati wa kumwonyesha bango hilo

Ikitokea hao Polisi na wengine wakakunyanyasa wakati unaonyesha bango lako tutawapa vipande vyao!
 
MAKOLE na wewe hujakatazwa kugoma, kuandamana kama huridhiki kwani una sababu zako
Huko Misri saa hizi kimewaka, baada ya kumkataa Mubarak akaingia Morsi Mohamed wa The Muslim Brotherhood
Kwa hiyo POLISI na JESHI utalionea bure kwani nao ni binadamu wana fikra kuliko wewe na hawafuati Mkumbo
angalia hao wanaompinga BARAKA OBAMA wanataka nini?
4.jpg

3.JPG

2.JPG
 
Last edited by a moderator:
Waafrika kusini wakati sio watumwa tena wa Kifikra linapokuja suala la uzalendo. Wanaandamana kwa nguvu zote kumshambulia Obama alipoingia nchini mwao. Wameandika mabango ya kupinga siasa za Rais huyo, wanakataa Afrika na waafrika kufanywa vinyago wasio thamani mbele ya wazungu.

Lipo funzo kwa viongozi uchwara wa hapa Tz pamoja na jeshi lao la polisi linaloendekeza fikra butu na mpindo za viongozi hao. Picha niliyoiambatanisha hapa haionyeshi dalili ya mabomu ya machozi, magari ya maji washa na magari ya delaya kama ambavyo wangeandamana Watanzania kwenye ujio wa bwana mkubwa Obama. Tunatishwa ili tusieleze fikra zetu juu ya hali ya mambo. Hii ya Afrika kusini ndio demokrasia ya kweli.

Tanzania.... Fikra huru bila mabomu inawezekana!!!
View attachment 100228
Hayo ndio mambo ya kupigania yapatikane kwanza sio kupigania kwenda Ikulu; tupate viongozi kwenye vitongoji, kata, udiwani na ubunge kwa wingi kuliko chama tawala ili tuzibadili sheria ziendane na demokrasia ya kweli na hatimaye tutinge Ikulu kiulaini. Nyie mnajidanganya eti watawala wana hofu ya kutoka madarakani kitu ambacho sio kweli hofu hiyo hawana wala hawawezi kuwa nayo siku za karibuni kwa kuwa wanajua wazi hakuna upinzani wa kuingia Ikulu leo wala kesho . Wanachokifanya wao ni kuwadhibiti msipate viongozi katika ngazi za chini kwenye vitongoji, udiwani na ubunge kwani wanajua hiyo ndio pekee njia itakayoweza kuwauwa kiuhakika
 
yaani tujadili mustakabali wa taifa letu kwa kutumia filamu ya sarafina?jeshi letu la polisi liko imara kuliko la afrika kusini...hv unajua afrika kusini ndo taifa linaloongoza kwa crime rate duniani?KAMWE hatuwezi kujifunza chochote kwa walioshindwa
 
Back
Top Bottom