Jeshi la Polisi Vifo hivi Kulikoni!? Waziri wa Mambo ya Ndani Tupe Maelezo si Siasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la Polisi Vifo hivi Kulikoni!? Waziri wa Mambo ya Ndani Tupe Maelezo si Siasa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Jan 27, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Hii tabia ya viongozi wetu kutokuwajibika imeota mizizi sana. Tumeiendekeza mpaka sasa imekuwa ni kawaida. Kwa mfano,

  Leo tarehe 27.01.2011 kuna taarifa hizi;

  1. Watu 3 wamekutwa wamekufa katika mazingira ya kutatanisha Kinondoni na Temeke. Source Nipashe uk. wa 3.

  2. Mtu 1 auwawa akijaribu kuiba dukani Kyela. Source Nipashe uk. wa 10.

  3. Mke auwawa kisa ujumbe wa simu Serengeti Mara, chuma kichwani. Source Nipashe uk wa 11.

  4. Mtoto auwawa na baba yake Longido Arusha, kitu kizito. Source Nipashe uk wa 17.

  5. Mtoto auwawa na kufukiwa kwenye shamba la mkonge, Morogoro. Source Mwananchi uk wa 9.

  6. Mtu 1 auwawa Morogoro akutwa na jeraha usoni, kitu chenye ncha kali. Source Mwananchi uk wa 9.

  7. Mwanamke auwawa kisa wivu wa mapenzi, akatwa shingo kwa kisu, Babati, Manyara.

  Hizo ni habari zilizoripotiwa kwenye magazeti mawili tu. Naamini zitakuwepo nyingine ambazo haziwafikii waandishi wa habari. Swali langu, kulikoni!??

  Mauaji hayo yanaonekana kuwahusu wanawake zaidi. Unyanyasaji wa wanawake. Kwenye gazeti la Nipashe kuna habari Mwanamke apigwa bakora akiwa amefungwa miguu na shingo na kufungiwa ndani siku tano! Kisa mtoto wa kondoo aliyeachiwa amchunge na mume wake mwenye wake watano alikufa! Hiyo imetokea Serengeti, Mara! Nipashe uk wa 8!

  Kuna uhusiano gani wa maisha na elimu duni na mauaji haya!? Ni hali ya ugumu wa maisha unachochea vitendo hivi au nini?

  Polisi wako wapi kudhibiti mauaji haya? Taarifa zao za kiintelligensia zinasema sababu ni nini?

  Siku si nyingi tumesikia mzazi ameua watoto wake akajiua na yeye! Bado kuna matukio mengi ya watu kujinyonga!!

  Nani anatakiwa alisemee hili? Kama wananchi hatutakiwi kushiriki kuzuia hii hali? Tutashirikiana na polisi wakati ndani ya mwezi huu polisi hao hao wameua raia watano! Arusha na Mbarali!!??

  Ni maswali yanayotatiza sana! Ni hali inayoshtua sana!

  Tujadili! Tuhoji pia. Waziri wa Mambo ya Ndani ameliona hili? Au yuko busy anapambana na migomo na kuzuia maandamano? Polisi je?
   
 2. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Bado wanasheherekea ushindi, na kusoma miongozo ya bunge ili kudhibiti wanasiasa wa ushindani wao wanawaita wapinzani. Haya yote yanatokea kwa kodi yetu ili tuvume machungu zaidi. Wakimaliza kusheherekea wataanza semina elekezi kisha makongamani.
  Mola awapumzishe hao ndg ktk ufalme wake, amen
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Likizo yao ikiendelea at the expense of Tanzanians! What a shame! Life lost is never accounted for! No one cares!

  Matukio haya yanaonekana ni ya kawaida. Utasikia 'uchunguzi unaendelea'
   
 4. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Lakini siyo yote Kati ya uliyoorodhesha hapo yanatokana na action or inaction ya polisi. Hivyo una hoja mbili tofauti.

  1. Maisha magumu yanazidisha hasira na kuongeza ukatili dhidi ya binadamu
  2. Polisi wameshindwa wajibu wao
   
Loading...