VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Zuio lenu la kuzuia mikutano,maandamano na makongamano ya kisiasa ya ndani na nje liliwafikia walengwa. Kuanzia siku lilipotolewa,wahusika wamelitekeleza ima kwa shurti au utii. Malalamiko yakatamalaki.
Mwezi huu,CCM tutakuwa na mkutano wetu mkuu pale Dodoma. Wajumbe wa mkutano wetu mkuu ni wengi kutoka nchi nzima. Dodoma itafurika na kufurahisha. Mkutano wetu wa Dodoma,kwa mujibu wa katazo lenu la kipolisi,nao umekatazwa. Haupaswi kufanyika bila kuondolewa kwa katazo.
Vyama vingine vya siasa nchini navyo vinatamani kufanya mikutano yao. Kujitangaza,kuongea na wananchi na kujiimarisha. Kufanya siasa hasa na si hasi za visasi. Jeshi la polisi,mmekuwa mkifanya kazi kubwa ya kulinda usalama. Mnastahili pongezi. Tafadhalini,ondoeni zuio lenu ili CCM na wengine wafaidi matunda ya demokrasia ya vyama vingi.
Jeshi la polisi,tusaidieni CCM twende Dodoma kwa amani kumkabidhi uenyekiti wa chama Rais mpendwa John Pombe Magufuli. Wakati sisi CCM tukifurahi,wapinzani nao wafurahi. Muda wa kuondolewa zuio umewadia!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Singida)