Jeshi la Polisi Tanzania kutotii amri zitolewazo na Waziri; tatizo liko wapi?

Huyo aliyemtengua si ndiye alikuwa anawapongeza na kuwapa misifa. Sasa amewageuka.

What goes around comes around.
 
Huyo lugola alikuwa askar polisi nadhan aliondolewa kazin akiwa nyota tatu pale magomeni na walifanya kazi kituo kimoja na IGP siro Sasa sijui ana kwama wapi lugola Mana utaratibu wote anaujua hii wizara Ina hitaji mtu mwenye busara Kama husein mwinyi hapa kwa lugola poor kabisa hamna kitu ana waibisha Sana askar police hopeless Sana anawavunja moyo askar wetu police
Unadhani Mwinyi akiletwa huko Police hatafanya kama Lugola?

Yatakua yaleyale tu.
 
Polisi ni miongoni mwa wahanga wakubwa wa wanasiasa,hiyo yote nikwasababu wanashughulikia wananchi moja kwa moja,laiti na JWTZ wangekua wanadili na hawa raia wenye lawama kila uchwao,hakika wangevunjika mioyo.
Ukiskia ile hutuba ya C law juzi na makamanda wa mikoa bado POLISI mnasafari ndefu nyinyi tu huko ndani ni vurugu mechi chek RPC wa ARUSHA nenda wa Dodoma nenda mcheki mambokale yaani utafikiri wako majeshi tofauti POLISI hawana standard moja ni double standard
 
A

Aliyoongea CLAW yawezekana kabisa ilikua ni namna yakujionyesha kwa MKUBWA ambaye ni mteule wake,na vilevile kuweka mambo sawa kutokana nakusemwa vibaya na baadhi ya ma-R.IPs.
 
Mkuu alishawaambia watembee vifua mbele kwani yuko nyuma yao. Amri pekee walioamriwa kuifuata bila hata kuhitaji sheria inasemaje ktk hilo ni zile zinazohisu Wanasiasa wa Upinzani Nchini. Yaani kuwaazuia wasitekeleze majukumu yao pamoja na kuwakamata na kuwafungulia kesi zozote zitakazomfurahishi Mkuu.
Sasa leo wanaumbuana hadharani mbele ya Wananchi wanaowaongoza.

Kauli za Mkuu ndiyo chanzo cha haya yote na si udhaifu wa Jeshi lenyewe. Ukiwa Kiongozi kisha unashiriki vitendo vya kutotii sheria basi hata amri ziko zitapuuzwa vile vile. Kiongozi anapaswa kuwa kinara wa kuzifuata Sheria za Nchi ndipo wale wote wa chini watatii amri zile bila shuruti.
Nakumbuka Kangi Lugola alishawaamrisha polisi kumkamata Zitto kwa kufanya mkutano jimbo ambalo sio la kwake wakamgomea. Kangi amegomewa mara nyingi sana hadi akaona imezidi akashtaki kwa Magufuli
 
Tatizo hapo naona wanamuiga Rais kutoa Amri hadharani na kufanyika hapo hapo
Sijui utaratibu wao upoje lakini ninavyojua maandishi ni bora zaidi ie emails
Lakini haya matamshi wengi wanaona kama wanafurahisha watu ndio maana wanadharau

Nilikuwa najua nidhamu ndio jambo kubwa sana huko
 
Unadhani Mwinyi akiletwa huko Police hatafanya kama Lugola?

Yatakua yaleyale tu.
Wanasema hata simba akiamua kula majani,basi ni ili atapike minyama iliyomkaba.hatakula kama anavyokula faru.

Fikiria nadharia ya kuhamisha kituo kizima ilivyo ngumu kutelelezeka haraka kama tamko lilivyokuja,achilia mbali taratibu za kiutumishi.

Shida ya lugo amekuwa mtu wa jukwaa sana mpaka anafanana na katuni.
 
Nahisi kuna missunderstanding/kutokua na maelewano ama viongozi kwa viongozi ndani ya idara/taasisi husika
 
Huyu atapigwa jungu moja mpaka ajikute jimboni kwakwe anakula mabumunda.

Polisi ni washenzi sana,hajui ni kwanini ni wizara yenye mawaziri wengi kuliko nyingine tangu uhuru!!!!
Kwa majungu wizara ya mambo ya ndani kunaongoza
 
mmaowatetea polisi hamjui uonevu wao.

1. nilikuwa nakaa kijiji x km 25 toka mjini, polisi wa pikipiki walikuwa wananikamata sana nikiwa na pkpk na kukuachia ni buku 10 tu. kwa siku za minada walikuwa wanakusanya zaidi ya m1 kwa wafugaji na wafanya biashara wa ng'ombe kisa pkpk.

2.nilipata majanga ya dogo niliekuwa naishi nae akadakwa anamla mwanafunzi mwenzie. wakanikamata nikakaa ndani wiki 2 na dogo. nilivyo jeuri nilikuwa nawatukana hadi niko nyuma ya nondo na nilikata tamaa ya kuishi tena. walikuwa wanataka m3 walisovu, nami nikawagimea hadi walipopigiwa simu na DCP fulani ambaye ni mkazi wa kijiji ninachoishi wakaniachia bila kutoa senti.

magu na kangi shikilia hapohapo hadi akili ziwakae sawa.
 
Siasa imekuwa ndio mambo yote ktk nchi hii, taaluma inachechemea. Hata yanapata nafasi kwenye vyombo vya habari. Vijijini kuna watendaji ndio kila kitu. Wananchi kuwekwa sero kwenye ofisi zao mpaka utoe malipo ya ng'ombe au mbuzi ni kawaida.
 
Lugola anaonewa tu hapo hana kosa lolote, kakuta watu wanalalamikiwa akachukua hatua kuwahamisha lakini watekelezaji wakadharau pengine dharau hii imeanzia kwa IGP mwenyewe huenda hata alijulishwa akapuuzia mwisho anatolewa kafara mtu mwingine. Pamoja na yote ni dhahili lugola hapolendwi na Polisi kwa sababu anazijua hila zao zote na madudu yao yote kwa sababu alishafanya kazi hiyo, na kutokana na kustaafu na cheo kidogo hawa makamishina wanampuuza kwa kusema hawawezi kupewa amri na superitendant , sasa nidhamu ya kisiasa inarudishwa kwa lazima na IGP ajiangalie asije akawa balozi wa .....sio muda.

Back
Top Bottom