Jeshi la polisi ni ukoo wa kambale; samaki mdogo kwa mkubwa, wote wana ndevu

kilimo kwz

Member
Jan 18, 2022
26
48
Wakuu kwema?

Baada ya mjadala wa muda mrefu kuhusu uovu wa polisi ulikokidhiri hasa siku za hivi karibuni,nimeona nami niseme kitu kwa uzoefu wangu wa hawa watesi.

Kwangu mimi jeshi la polisi nalifananisha na ukoo wa kambale ambao kila samaki ana ndevu bila kujali umri,yaani namaanisha hakuna nidhamu ya vyeo kati yao na haya Nina mifano nayo ambayo nimeiona mara kadhaa.

Mara ya kwanza miaka kadhaa imepita nilipokamatwa mitaa ya ccm kirumba Mwanza usiku wa saa mbili usiku na askari waliokuwa kwenye defender, nilikuwa napita kwa miguu kuzunguka uwanja wa CCM kirumba nikielekea mtaa wa Ghana, nilidakwa na askari wawili waliokuwa wamesimama pembeni na kabla sijaongea kitu nilibebwa kwa mwendo wa Tanganyika jeki huku nikisachiwa kama mateka na kupelekwa kwenye kalandinga na kutupwa ndani ya karandinga, nilikuta raia Kama wawili, baada ya kukaa sawa ndo nikaja kujua nimesha cholomewa pesa zote zilikuwa kwenye suruali kiasi cha elf 30, ilibidi nitulie kwa mda huku nikifakari kosa langu nilikaa pale kwa takribani dakika 10 na ndo ikabidi nianze kujitetea ukizingatia mm kipindi hicho nilikuwa mwana chuo, niliongea kwa sauti kuwa mm sikuwa na kosa na nilikuwa mpita njia nikielekea Nyumbani.

Askari mwenye nyota mbili yaani insepecta wa polisi alionyesha kunisikiliza hasa ukizingatia baada ya kuwa nimesema ni mwanachuo, lakini ajabu na kweli askari mwenye cheo cha constable aliyeonyesha dhahiri kuwa amelewa aliupinga utetezi wangu na kusema sitoweza kuachiwa maana wao wapo hapo kufanya operation ya kukamata yeyote wanaemuona, ubishi mkubwa uliibuka kati ya constable na yule insepoctor kiasi cha yule constable kunyoosha mtutu wake wa bunduki akimwelekezea yule inspector, kile kitu kilishanganza sana kwani kwa uzoefu wangu linioupata nikiwa JKT kwa mujibu wa sheria hairuhusiwi kabisa kufanya hivo, heko sana kwa JWTZ upuuzi huo sikuwani kuuona kabisa pamoja na kuwa nilikaa huko miezi nne 824KJ.

Ebhana ilibidi inspector awe mpole, niliendelea kukaa pale mpaka pale alivyokuja tena yule askari mmoja kati ya walionikamata na kunisachi ilibidi nilimwongeshe na kumpa tena elf 20 ambayo hawakuiona kwani ilikuwa ndani ya sharti na nilimuomba aongee na constable mwenzake yule mbishi ili niachiwe kwani kesho yake milikuwa nasafiri kuelekea Dodoma chuoni, yule askari alimuita pembeni na sijui waliongea nini ila askari yule mbishi alinifuata na kunivuta nje ya gari nilipigwa buti na kuambiwa nitoweke hapo haraka sana, nilikimbia sana na kutoweka huku nikiwa nimedhurumiwa elf 50 bila kosa kabisa.

Mifano ipo mingi kuwa nidhamu ndani ya jeshi la polisi ipo chini na kuna kulindana Sana,naomba kwa leo niishie hapo,ila jeshi la polisi ni ukoo wa kambale hakuna mkubwa na mdogo wote wana ndevu.
 
Naongea toka moyoni,

Nina chuki sana na polisi,

Kuna siku nipo na jamaa yangu tupo na gari lake, tupo kwenye zebra + Tuta kwa pamoja watu wakivuka barabara mara ikaja boda ikagonga gari kwa nyuma tukashuka, kuja kucheck ni boda imegonga pumper imebonyea na kupasuka.

Tukawa tunaongea na huyo boda kwa nia ya kulipana, boda alikuwa anajitetea kuwa hana kitu. ikabidi tutaute polisi, tukatoka hapo na boda hadi polisi na gari.

Boda akawa anajitetea hana kitu, hali ngumu ametoka Hosp. mama yake kalazwa zaidi ya wiki ana mawazo nk. yani ni kijijini na jamaa anaonekana kweli hawezi mudu kirahisi kutengeneza gari.

basi huruma ikatuingia tukawa kwenye mlengo wa kumsamehe.

Daah tukaona polisi anavimba na jamaa kinoma wakati sisi tumewithdraw dispute.

Polisi anasema hata kama jamaa wamekusamehe, muda wangu lazima uulipie. una sh. ngapi?

Jamaa anasema ana elfu 5 polisi lakini hataki. jamaa akasema nyumbani ana debe 2 za maharage.

polisi akamwambie jamaa aache pikipiki akalete hizo Debe 2 wamalize kesi.
 
Hata nyie pia wapuuzi, yaani msimsamehe mwana matatizo huyo, mmempeleka polisi, ndio mumsamehe. Na mlienda mkiamini hatotoka bila kuwalipa. Nenda kule hata nyie ni kama polisi tu.
Boda boda wa kupeleka polisi ni yule anayekaidi.
 
Back
Top Bottom