Jeshi la polisi ni mzigo mwingine

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
250
“WAKATI Polisi wakiendelea kukalia jalada la Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), anayetuhumiwa kubaka na kutishia kuua binti wa miaka 16, sasa suala hilo limefikishwa katika ubalozi wa Marekani.”


………..“Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alipoulizwa juu ya hatua waliyofikia katika kupeleka kesi hiyo mahakamani, alisema bado wanaendelea na uchunguzi. Alipoulizwa ni uchunguzi wa namna gani wanaoufanya na kama wameshapata maelezo ya Profesa Kapuya, Kamanda Wambura alisema miongoni mwa hatua za uchunguzi ni pamoja na kumuhoji mtu anayetuhumiwa.”


Sorce. Tanzania Daima
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,528
2,000
Kwa nini watanzania tunawaabudu marekani hivyo?Kila kitu kushtaki marekani!ipo siku mtu akimfumania mwenzake ataenda kushtaki ubalozi wa marekani.Kama wamarekani wa maana tuige na ushoga wao
 

Kajunjumele BA

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
673
195
Kwa nini watanzania tunawaabudu marekani hivyo?Kila kitu kushtaki marekani!ipo siku mtu akimfumania mwenzake ataenda kushtaki ubalozi wa marekani.Kama wamarekani wa maana tuige na ushoga wao

Mkuu huyo ndiyo Kaka mkubwa na hilo halina ubishi si unaona hata wakuu wetu hawaishi kwenda huko marakwa mara ili kujichekelesha bila kuchekeshwa. We si unaona Kaka mkubwa alipotembelea Ubungo mambo yote kimya hakuna anayezungumza tena kuhusu uhalali wa ile kitu inayotoa nishati Pale.

Watu wanakwenda kwa Kaka Mkubwa kwasababu wanajua Serikali hii haigopi Mahakama wala "Kinyago chao wanacho kichonga cha kulinda na kufukuza wananchi wapenda demokrasia lakini hapa soma "wanyama wa haribifu wa mazao" "Zamani wakati likiwa jeshi la wazalendo liliitwa Jeshi la Polisi USALAMA WA RAIA" lakini sikuhizi limebadilika sana hapo kwenye usalama wa Raia soma usalama wa viongozi wa CCM.Mungu pishilia mbali laiti mtuhumiwa angekuwa kiongozi kutoka "CHAMA FULANI KINA CHOPENDWA NA WANANCHI WENGI NAKUCHUKIWA NA WATAWALA WENGI" angekuwa ameisha vunjwa vunjwa miguu kwa mabomu matamko kibao na hata Helkopta zingekuwa zinamsindikiza kwenda Kisutu wa kidai ni mtu hatari sana.

Kwahiyo ukitaka kuwadhibiti hawa jamaa wewe ukiona wanakubana tu kimbilia kwa Kaka Mkubwa yeye akikohoa utasikia nchi nzima viongozi wana Itika Naam Naam na wengine Rabeka Bwana naja.Huko ndo Dawa yao kwani hawaigopi Mahakama wala Polisi kwasababu wanajua kwamba wengi walioko kule wamewavalisha bangili Mdomoni hawawezi kuwauma kabisa na wakifurukuta wataishia kubweka tu baaasi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom