M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
So far nchi yetu haijaweza kukumbwa na matukio ya moja kwa moja ya ugaidi kama ambavyo imekuwa ikitokea katika nchi nyingine za Africa na kwingineko.
Sababu kubwa si nyingine bali ni ile tabia/hali ambayo Watanzania tumejengewa tangu tupate uhuru - uoga wa kutokuhoji (docility) hata pale inapobidi kufanya hivyo. Kwa mambo ambayo watawala wa nchi hii wamekuwa wakiyafanya dhidi ya raia wasiowapenda, sidhani kama kungekosekana kuibuka kwa vikundi vya uasi, ambavyo mara nyingi hutafsiriwa kuwa ni vya kigaidi.
Kwa kweli katika hili, pamoja na yake mengine mazuri yote, Mwalimu (baba wa taifa JKN) alitupoteza.
Lakini, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
Kama Mwalimu mwenyewe wakati wa uhai wake alivyowahi kukiri na kutuasa kuhusu ubovu wa katiba yetu - kwamba akiingia rais ambaye kupuuzia haki za wananchi anaona ni jambo la kawaida basi anaweza kuitumbukiza nchi katika sintofahamu (siyo nukuu ya moja kwa moja lakini hii ndiyo tafsiri rahisi kabisa ya hofu aliyokuwa nayo Mwalimu)
Sisi sote tumekuwa mashuhuda wa "unabii" huu wa Mwalimu baada ya Magufuli kuwa rais ambapo aliyempokea (Samia) ameendeleza palepale alipoishia mtangulizi wake.
Chini ya awamu ya 5 & 6, tumeshuhudia chama tawala na serekali yake vikijificha nyuma ya jeshi la polisi kwa kujinaisha (criminalize) shughuli halali za kisiasa na uanaharakati kutoka ndani na nje ya chama chao. Na kama tulivyoshuhudia siku za hivi karibuni, mmoja wa makada wa chama tawala amefanya mauaji dhidi ya polisi katika tukio ambalo limetafsiriwa kama ni kisasi dhidi ya jeshi la polisi (ambalo katika nyakati hizi limepewa nguvu kubwa sana sana na serakali na limekuwa likishiriki katika vitendo vya uonevu, unyanyasaji na sehemu nyingine tumekuwa tukipewa taarifa juu ya kuuawa kwa wahalifu na wasio wahalifu bila kufuata mkondo wa kisheria kama inavyotakikana chini ya katiba).
Aidha, wanachama na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na wanaharakati wamekuwa wakikamatwa bila kufuata sheria na kuachiwa kama vile ni jambo la kawaida kabisa. Hii si trend yenye afya kwa mustakabali wa taifa letu. Watu wanaofanyiwa hivi wana watu kwa mamilioni nyuma yao, hivyo chuki dhidi ya jeshi la polisi na serekali ni dhahiri itakuwa inazidi kujengeka ndani ya mioyo mamilioni miongoni mwa ya jamii athirika ya Watanzania. This, needlessly, sets up our beloved country as a potential breeding ground for "The HAMZAs" of this world.
President Samia (my president and above all my dear sister) - please take note and act NOW before this situation gets out of hand. I beg!
Latest episode ya uonevu wa unaofanywa na jeshi la polisi ni hili tukio hapa chini lililotokea leo huko mkoani Mara.