Jeshi la Polisi nchini kutumika na CCM kuwabakiza madarakani ni uvunjifu wa Katiba ya nchi

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,478
30,140
Tukiisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, inasema wajibu namba moja wa Jeshi letu nchini kuwa ni kuwalinda raia na mali zao

Jeshi hilo halipaswi liwalinde watawala, bali linatakiwa litimize majukumu yake kwa weledi bila kupendelea upande wowote

Sasa yanapotokea matamko kutoka kwa viongozi waandamizi wa Jeshi hilo la kuwatisha raia hao ndipo ninaposema hawatimizi wajibu wao bali wanatekeleza "maagizo" toka kwa watawala walio juu, kuyatamka hayo maneno kwa lengo la kuendelea kuwabakisha madarakani

Katika siku za karibuni tumesikia kauli za vitisho zikitolewa na viongozi waandamizi wa Jeshi la hilo kuhusu huo unaoitwa kama uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika hapa nchini, tarehe 24 mwezi huu

Kwanza yalitolewa matamshi kutoka kwa Waziri wa mambo ya ndani, Kangi Lugola, akiwatisha wananchi kuwa yeyote atakayethubutu kuuharibu uchaguzi huo, ataliagiza Jeshi lake la Polisi, kuwa watu wa aina hiyo siyo tu wamwagiwe maji ya washawasha, bali pia wakamatwe na watumbikizwe kwenye matenki ya maji hayo ya washawasha!

Kiongozi mwingine wa juu kabisa aliyetoa vitisho kuhusu uchaguzi huo ni IGP Sirro aliyetishia kuwa watawachanachana hao watakaothubutu kuharibu uchaguzi huo.

Watawala wetu ni lazima watambue kuwa kulitumia Jeshi letu la Polisi kuwatisha raia ni uvunjifu wa Katiba ya nchi yetu, kwa kuwa inafahamika wazi kuwa nchi yetu ni ya kidemokrasia na inayofuata mfumo wa vyama vingi

Hebu tuje kwenye hicho watawala wetu wanachokiita ni uchaguzi wa vyama vingi wa serikali za mitaa

Hebu kwanza tuiangalie Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) inasema hivi nanukuu " Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya mfumo wa kidemokrasia na ni ya vyama vingi" mwisho wa kunukuu

Hivi utawezaje kuiita.nchi kuwa ya kidemokrasia na ni ya vyama vingi wakati watawala wetu wanawaengua wagombea wa vyama vya upinzani, zaidi ya asilimia 95??

Hivi utawezaje kuita huo uhumi uliofanyika, kuwa ni uchaguzi wa vyama vingi, wakati wagombea zaidi ya asilimia 95 wamekatwa majina yao na wasimamizi wa uchaguzi, ambao ni makada wa CCM kindakindaki??

Wakati huo huo wagombea wa CCM, asilimia 100 wakionekana kama "malaika" kwa kuzijaza kwa usahihi kabisa na hivyo kuwafanya wagombea wake kupita bila kupingwa!

Kitendo kilichofanya vyama 8, wakiongozwa na chama kikuu cha upinzani nchini, cha Chadema kutangaza kujiengua, kwenye uchaguzi huo

Vyama hivyo vilivyojitoa vimeendelea kutoa wito kwa watawala wetu, ili waufute uchaguzi huo na kuupanga wakati mwingine, chini ya Tume huru ya uchaguzi, lakini wito huo umewakuta watawala wetu, ambao wamelewa madaraka, wakiwa wameweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kuwasikiliza

Niwaambie tu hawa watawala wetu, watakuwa wanajidanganya mno, wakitumai kuwa Jeshi la Polisi, lina uwezo wa kuwadumisha wao CCM kwenye madaraka milele na milele

Imenenwa kuwa kila chenye mwanzo hapa duniani, ni LAZIMA kifikie mwisho ns mwisho wa CCM umekaribia sana
 
Hata Rais msataafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, aliwahi kuwaasa wanaccm wenzake kuwa ni makosa makubwa sana kulitegemea Jeshi la Polisii nchini kuendelea kuvikandamiza vyama vya upinzani nchini kwa lengo la kuibakiza CCM iendelee kubaki madarakani
 
Back
Top Bottom