Jeshi la Polisi na viongozi wa kisiasa

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
83,334
97,346
Hivi karibuni kumekuwepo kama kutokuaminiana kati ya Jeshi la polisi na viongozi wa vyama vya siasa hasa upande wa upinzani. Ukisikiliza kila upande una hoja za msingi sana. Upande wa jeshi la polisi wanasema wanataarifa zao za kiintelijensia kuhusiana na mikutano ya kisiasa ambayo inaweza kuhatarisha amani, upande wa viongozi wa kisiasa hasa upinzani wanasema mikutano ya kisiasa ndiyo mtaji wao wa kunadi sera zao na kupata wanachama wapya.

Wote hawa jeshi la polisi na viongozi wa vyama vya siasa hasa upinzani wanahoja za msingi kabisa. Tatizo hapa ni moja tu wahajapata muda wa kukaa/kukutana pamoja kuongea na hatimaye wakakubaliana vizuri.

Natoa ombi kwa viongozi wa dini (Kikristo na Uislamu) wawakutanishe viongozi wa jeshi la polisi, mwanasheria mkuu wa serikali na viongozi wa vyama vya siasa wajadili kwa mapana na marefu hatimaye wakubaliane nini kifanyike. Viongozi wote wa vyama vya siasa, jeshi la polisi na watu wote kwa ujumla tunawategemea viongozi wa dini kwa ushawishi wao kwenye jamii. Binafsi naamini mbele ya mashekh na maaskofu hakuna jambo litaharibika. Wakitoka hapo wapinge picha ya pamoja na hatimaye kila upande ushirikiane na upande mwingine.

Nimeomba viongozi wa dini sababu wao ni baba zetu kiimani, pia watasikiliza kila upande na wao kutoa maoni yao ya nini kifanyike baada ya kusikiliza pande zote.

Mwisho ikiwezekana watoe mrejesho wa nini walichokubaliana. Baada ya hapo ambaye ataenda kinyume na makubaliano basi jamii haitamwelewa.

Kabla ya kuwakutanisha niliowataja hapo juu, viongozi wa dini waombee jambo hili lipate Baraka toka kwa Mungu wetu.

Amani tunaipenda na bado tunahitaji kwa afya ya taifa letu la Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania na Mungu bariki viongozi wetu.

Nawasilisha.
 
Polisi hoja yao INA umsingi gani? Wanazuia Mikutano ya Upinzani mpaka ya ndani, CCM wanatuhusiwa, haya hoja yao ni nini

Mikutano IPO kisheria, Kama Serikali inataka kufanya kazi ifanye tu kwani Mikutano ya Siasa inawazuia nini?
 
Namba moja ni jamii yote ya watanzania tuwe wakweli. Polisi hawajawahi kuwa na hoja za msingi kuhusiana na hilo zaidi ya kujidhalilisha kwa uongo na ukinyonga. Jeshi la polisi limeonyesha lina uwezo wa kukabiliana na hatari zote bila kujali ukubwa wake. Badala ya kujigeuza mahakimu wa kutoa mazuio ya kichwara, wawe wanalinda mikutano yote kwa usawa na nguvu ileile.
 
kiintelejinsia kutoka wapi? yule mama wa waste gate na yule mchinjaji wa isis si walipita hapa tanzania? polisi ni chama cha siasa mchina waneshindwa kumkata hadi mwigulu kaenda kuwasaidia kutambua kosa la mchina kujichukulia sheria mkononi hata kama jamaa ana makosa walipaswa kutompiga sasa wasikie gwajima na chadema utaona walivyo vaa kama wanaenda kupambambana na magaidi.
 
TATIZO JESHI LA POLISI LIMEKUWA LIKITUMIWA KAMA MGAMBO VILE .... SIJUI LITAJISAFISHAJE HILI JESHI MAANA LINAPAKWA MATOPE KILA KUKICHA NA WANAOLITUMIA WANALIACHA KAMA KARATASI LA CHOONI
4.jpg
 
Polisi wana nguvu ya kutosha kupambana na uvunjifu wa Amani wa Ania yoyote kama walivyotuonyesha Dodoma baada ya kutishiwa na vijana wa BAVICHA. kwa nini wanaweza kulinda mkutano wa CCM na kushindwa wa CDM?
 
Back
Top Bottom