Jeshi la Polisi na TCRA walipaswa kumuhoji Zitto Kabwe. Anamaanisha nini kwa kusema "The United Republic of Gangsters". Kuna Jamhuri anaikejeli

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Zitto.PNG
Screenshot hapo juu ni statement ya kaka yangu Zitto Kabwe siku kadhaa baada ya kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji almaaruf kama MO

Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu JF.

Ninajua fika baada ya kuandika thread hii kuna watu watanitukana sana, wengine watasema ninajipendekeza kwa wakubwa, wengine watasema ninatafuta uteuzi, wengine watasema mbona ninajishushia hadhi. Ila ninachosema mimi ni kuwa sipo hapa jukwaani kwa minadi ya kufurahisha watu. Bali nipo hapa kuongelea ukweli kama ambavyo unapaswa kusemwa.

Katika ukurasa wa Twitter wa mwanasiasa Zitto Kabwe, nimekutana na post yake moja alioandika kwa lugha ya kiingereza kwamba "The United Republic of Gangsters" kwa tafsiri ya haraka haraka ya kiswahili inaweza kuwa na maana kwamba "Jamuhuri ya Muungano wa Wahuni"



Kwa maoni yangu mimi naona kuiita Jamuhuri fulani kuwa ni ya watu wahuni si lugha yenye staha kwa mwanasiasa kama Zitto (Ingawa hajataja hiyo jamuhuri ni ya nchi gani) vile vile ni kosa kubwa sana la kimtandao (Cyber Crime)

Jeshi la Polisi pamoja na TCRA walipaswa kumuita na kumhoji Zitto kuwa alikuwa anamaanisha nini kwa hiyo statement yake "The United Republic of Gangsters", hiyo jamuhuri ya muungano imeunganisha mataifa mangapi ya wahuni? Je, marais wa nchi hizo zote ni wahuni pia? Watumishi wa vyombo vya usalama wa jamuhuri hiyo ni wahuni pia (army, police, intelligence officers, immigration, anti-corruption, fire brigade, teachers, doctors)

Jamuhuri hiyo ni ipi na ipo wapi? Police walipaswa kuhoji hili. Unakuwaje kiongozi wa chama cha ACT wazalendo alafu unatumia lugha za matusi zisizo na uzalendo dhidi ya Jamuhuri za watu wengine hata kama hiyo Jamuhuri ipo nje ya Africa.

Zitto nilikuwa ninamuona ni moja Kati ya wanasiasa makini kumbe ameanza kukosa staha.

Zitto kama mwanasiasa ndiye anayepaswa kuwa kioo cha jamii kuanzia mienendo, lugha mpaka utii wa sheria za nchi (kutotumia lugha zenye ukakasi na kejeli) leo ndio unaandika maneno ya hovyo kwenye mitandao.

I'm very disappointed in you brother.

IMG_20181017_095153_297.jpg
 
tuambie nii kifungu gani cha sheria ya mtandao au penal code aliyovunja hadi akamatwe
otherwise,futa garbage yako wewe bush lawyer

Manara alikamatwa Kwa kosa la kutangaza Habari Za MO kutekwa bila ya kutumwa Na familia

Kuna penal code iliyotumika?
 
Hivi haya yote yanayotokea; waandishi, wanasiasa wanaharakati na sasa wafanya biashara; kuteswa, kutekwa na au kupotezwa; bila vyombo vya usalama kuwa na clue yoyote na kubihevu kama wapiga ramli ni sawa kweli? Yaani amepotezwa Ben Saanane, ametekwa Azory na Kinguye, ameshamvuliwa TL; wameuwawa wengi Kibiti, wameokotwa wengi fukweni wakiwa kwenye viroba, halaf mtu kwa uchungu na hasira anaamua kuiita nchi hii URG, halafu bila aibu unamlaumu????
 
apples and oranges (yani unalinganisha vitu viwili tofauti)
hakuna sehemu zitto kaitaja nchi yoyote
manara kamtaja mo..

Mie nimezungumzia hoja ya penal code

Kama Mtu kukamatwa Ni lazima itumike penal code wapi kwenye penal code inasema ni kosa kutangaza Habari Za Mtu kutekwa bila ya Ruhusa ya Familia ?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom