Jeshi la Polisi na Serikali ya Tanzania hii siyo sawa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Mgombea Mwenza wa CHADEMA anapita njiani, anakutana na wananchi, wanataka kumsalimia. Polisi walio kwenye msafara wanatoa mabomu na kuanza kuwapiga wananchi.

Lakini wakati hayo yanafanyika mgombea wa CCM yeye akipita sehemu akakuta wananchi njiani, anaongea nao tena masuala ya kuomba kura lakini hatusikii chochote kutoka kwa tume ya uchaguzi juu ya suala hilo

Wakati hayo yanafanyika, Waziri Mkuu naye ambaye hayumo kwenye ratiba rasmi za NEC za mahali wanakotakiwa kufanya kampeni wagombea Urais katika tarehe maalum, yeye hayumo kwenye ratiba iliyotolewa na NEC ya kampeni za urais lakini anazunguuka nchi nzima.

Hii siyo sawa, siyo sawa kabisa ni uonevu mkubwa kwa wananchi. Kwani kosa la wananchi ni nini?.

Mbona Jeshi la Polisi lilianza vizuri, leo imekuwaje mpaka linapiga wananchi wasio na hatia mabomu?

Kwa matendo haya ya Kikatili ya Polisi, ndiyo maana watu wanaichukia serikali, na kama hawajui, mabomu haya yanazidisha chuki dhidi ya Magufuli na Chama cha mapinduzi. Wananchi hawapendi ubabe ubabe na uonevu.

Wakati huo, Mgombea mwenza wa CCM anapita njiani anasalimiana na wananchi na wanachama wa CCM walioko njiani kabla ya kufika kwenye kituo cha kampeni lakini Jeshi la Polisi halitawanyi wananchi hao kwa hoja za kuwa hawako kwenye eneo rasmi la kampeni. Hii double standard na uonevu kwa wapinzani haikubaliki!

IMG-20200930-WA0193.jpg
 
Wananchi tunaipenda Serikali acha kutuchonganisha na Serikali. Hao Polisi unaowasema eti wanatoa mabomu na kuwapiga Wananchi, kwani wao ni vichaa? Iko sababu ya kufanya hivyo na inachagizwa na dharau na kiburi cha viongozi wa Chadema kutokufuata maelekezo, mbona tunawajua vizuri
 
tapatalk_1601418168188.jpeg
 
Si mlikuwa mnamsimanga JK kama legelege, sasa mpepata chuma. Hakuna kusalimiana ni mabomu tuu, mtaisoma namba. Bado miaka mitano ijayo, tena mshukuru Mwalimu alieka term mbili. Vyenginevyo msubiri hadi afariki 😁
 
Hawa ni wapumbavu tu. Hakuna jina zuri zaidi ya hilo.

ni wapumbavu tu kama wale wa tarime tu.

Wanajaribu kuzuia mafuriko kwa vijana vya mkono.
 
Si mlikuwa mnamsimanga JK kama legelege, sasa mpepata chuma. Hakuna kusalimiana ni mabomu tuu, mtaisoma namba. Bado miaka mitano ijayo, tena mshukuru Mwalimu alieka term mbili. Vyenginevyo msubiri hadi afariki 😁
na atafariki kweli ujue. Mungu hadhihakiwi
 
Bomu moja dhidi ya wananchi wasio na hatia linasaidia kuwashawishi wananchi hao kumpa kura Lissu kuliko hotuba ya dakika tano

Waache waendelee na ukatili wao waone kama wananchi hawajawadharau
Mkuu usiwaamshe waliolala, bado siku chache tu 'wanyenchi' tufanye Jambo letu.

Hao waliopigwa mabomu ni sehemu ya watakaoleta mabadiliko chanya hapo tarehe 28 October!
 
Wananchi tunaipenda Serikali acha kutuchonganisha na Serikali. Hao Polisi unaowasema eti wanatoa mabomu na kuwapiga Wananchi, kwani wao ni vichaa? Iko sababu ya kufanya hivyo na inachagizwa na dharau na kiburi cha viongozi wa Chadema kutokufuata maelekezo, mbona tunawajua vizuri
Mbona yanayofanywa na CHADEMA ndo yanayofanywa na CCM lkn CCM hawapigwi mabomu?....endeleeni kujitekenya
 
Si mlikuwa mnamsimanga JK kama legelege, sasa mpepata chuma. Hakuna kusalimiana ni mabomu tuu, mtaisoma namba. Bado miaka mitano ijayo, tena mshukuru Mwalimu alieka term mbili. Vyenginevyo msubiri hadi afariki 😁

Ungesema tumepata "jinga" ungekuwa umemaliza kabisa. Kwa hakika kusingekuwa wala chenji.
 
Back
Top Bottom