Jeshi la Polisi na mabadiliko yanayohitajika

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Wengi wetu tumewahi kwa namna moja au nyingine kugusana na jeshi la Polisi kwa mema au kwa ubaya. Na kama siyo sisi wenyewe tunawajua watu kadhaa ambao wamewahi kuwa na jambo Polisi. Yawezekana wapo ambao hawakufurahia utendaji kazi wa jeshi la Polisi na wangependa iwe tofauti.

Baada ya kwenda sehemu mbalimbali duniani na kuona utendaji kazi wa majeshi mengine bila ya shaka kuna kitu na sisi tunatamani kuona kinatokea katika kulibadilisha Jeshi "letu" la Polisi.

Nimeombwa na mtu mmoja (ndani ya jeshi hilo) kusolicit mawazo ya wana JF kuhusu mabadiliko muhimu ndani ya Jeshi hilo hasa linapojiandaa kukabili matatizo ya karne yetu hii ya "mawasiliano". Tayari binafsi nilishatoa maoni yangu miaka miwili iliyopita ambayo baadhi yalifanyiwa kazi kwa kuunda "Kanda Maalum" ya Dar. Hata hivyo bado kuna mambo mengi sana yanahitajika kuweza kulifanya jeshi hilo kuwa karibu zaidi na wananchi, la kisasa zaidi, na ambalo linafuata sheria zaidi na lenye kuweza kutimiza jukumu lake la "Usalama wa Raia na Mali zao".

Mada itafuatiliwa na baadhi ya wahusika na wataalam wa UDSM ambao tayari walikabidhiwa jukumu la kupendekeza mabadiliko ya Jeshi hilo. Maeneo makubwa matatu yanahitaji kuangaliwa.

- Sheria ya Jeshi la Polisi - Police Ordinance
- Muundo
- Majukumu

Haya wana JF huo ni wakati wetu wa kushine! ni rahisi kukosoa zaidi lakini sasa ni wakati wa kujenga; tutaweza changamoto hii?

M. M.
 
Nitatoa maoni yangu kuhusu muundo wa jeshi la polisi.
Kwanza napendekeza jeshi ligawanywe ktk sehemu kuu tatu.
a, kikosi maalumu,
Hiki kitakuwa na jukumu la kushughulikia mambo ambaya yatahusu masuala ya kitaifa.
b,polisi wa mikoa,
Hawa watakuwa chini ya halimashauri za mahala husika na watawajibika kwa halimashauri au mkoa.
Ajira zao zitatokana na mikoa husika,
Hawa watabeba majukumu ya kulinda usalama wa raia na mali zao,utendaji wao utakuwa ndani ya mikoa yao.
c,polisi jamii,
Hawa ni polisi wa kujitolea ambao watawasaidia hawa polisi wa mikoa,lakini watafanya kazi ktk kata zao,na maeneo yao ya karibu.
 
Mkjj,

polisi kweli wana mpango wa kutumia maoni ya wana JF? yangu macho ila ninawaogopa polisi wa bongo kwa mambo yao kama ukoma
 
Niliwahi kumwandikia IGP barua mwaka jana na kumweleza maoni yanu juu ya polisi wa Usalama Barabarani.Nina omba sasa tena anisikilize kwamba katia kufanya mabadiliko na katika kukabiliana na uhalifu basi Kikosi kile kiondolewe kirudi kama kawaida na Polisi wote wawe ni waangalizi wa Usama wa barabarani muda wowote wawapo kazini .Hil litaondoa uzembe mkubwa wa traffic na kuendekeza rushwa ndogo ndog lakini zina impact kubwa kwa jamii.Tusiwe na muda wa kusema mimi ni polisi wa usalama no tuondoea nguo nyeupe na labda kuacha kikosi cha State Motorcade basi.

Hawa watu wa usalama barabarani wna shida kubwa na kazi zao zinalate rushwa na si effective so naomba warudi kama kawaida iwe kama Nchi za Ulaya ambapo Polisi wan patrol na kuangalia usalama mzima kila kona iwe barabarani na negineyo.

Polisi sasa wapewe nyezo na hasa magari mengi ya kiraia ambayo yamekuwa equiped kama walivyo na pikipiki .Wakia katika mazingira ya namna na hasa miji mikubwa wakiranda kila kona ni rahisi kujua mengi na kutoa taarifa za haraka kunako husika na hatimaye kufanya arrest .

Polisi posti zina nia njema lakini zimebadilika na kuwa na vituko sana .Nalo hili liangaliwe liboreshwe .Nitakuja tena nikisha kuwa na wazo zaidi .
 
Review salary scale! Polisi ku-offer umpe rushwa ya shilingi 2000? It's disgusting!
 
Mwanakijiji na wengine,

Mimi ntaongelea kuhusu uongozi,mfumo na majukumu.

Uongozi wa jeshi la polisi nafikiri hauitaji mabadiliko makubwa ingawa mimi ntatanguliza jopo la watu ambao wataitwa City polisi Authority ambao watateuliwa na IGP kwa kila mkoa.

Watu hawa wataounda CPA watajumuisha majaji, wasomi, wafanza biashara na watu binafsi na wengine itabidi wateuliwe na RPCs ili wawe kwa kila mkoa.

Pamoja na mambo mengine ya ufanisi CPA itashughulika na kuhakikisha kwamba polisi wanakuwa wanawajibika kwa kazi waliyoomba ya kulinda raia na mali zao.

Lakini cha muhimu kitakuwa ni kuhakikisha inashughulikia suala la mishahara ambapo chombo hiki bado kiko hoi na ndio chanzo cha polisi kuwa wapenda rushwa.

Pia katika uongozi huu wa juu, IGP na msaidizi wake watabakia kama walivo.

Hawa watafatuatiwa na Wakurugenzi ama ACPs ambao ni wa idara za utumishi, mabohari na ICT (informationa communication technology) na wengine kama wapo.

Kuhusu mfumo hapa ndipo penye kazi kubwa na ni kama ifuatavo:

Mapolisi wote ambao wana fani mbalimbali na ndio wanaunda utawala wa jeshi la polisi au "management".

Na baada ya hapo ndio pana idara mbalimbali kama zifuatavo:

- RPC na matawi yote ya polisi nchini Tanzania,

- Idara ya CID ambayo itashughulika na uhalifu wa aina zote kama vile wizi wa kuku na madawa ya kulevya.

- Idara ya maalum ya upelelezi wa makosa kama ughaidi, wizi wa kalamu, wizi wa kiaina na usanii wowote ule na hapa ndio patakuwa kiini cha jeshi la polisi kwani patahusisha wataalam mabalimbali wakiwemo watu wasio polisi.

Na mwisho kutakuwa na idara ya ndani au "central operations " ambayo itashughulika na ulinzi wa sehemu kama reli,uwanja wa ndege, ulinzi wa mali ya umma( yoyote ile) na kwa kutumia utaalam kama wa computer.


Hivo ndivo nionavo na kwamba kiini hapa kitakuwa ni hio CPA.
 
............
- Sheria ya Jeshi la Polisi - Police Ordinance
- Muundo
- Majukumu
.........................M. M.

Mzee M'kijiji,

Sina hakika kama Polisi yetu ina website, na hivi hayo mambo matatu hapo juu yatakuwapo ktk website yao?
nasema hvyo kwa sababu ni vizuri tukijua walichonacho...........then tuone mapungufu na namna ya kuboresha zaidi

kuna mtu kazungumzia Polisi Jamii......ni wazo zuri sana.
 
Mzee M'kijiji,

Sina hakika kama Polisi yetu ina website, na hivi hayo mambo matatu hapo juu yatakuwapo ktk website yao?

nasema hvyo kwa sababu ni vizuri tukijua walichonacho...........then tuone mapungufu na namna ya kuboresha zaidi

kuna mtu kazungumzia Polisi Jamii......ni wazo zuri sana.

Ogah

Wanayo mkuu ni hii hapa http://www.policeforce.go.tz/


Mwanakijiji,

Nakuhurumia kwa kuwa utapata wachangiaji wachache sana!!! Watanzania tunapenda kujadili watu sio kujadili hoja, sasa kama mimi muongo subiri.

Nitakuja na mapendekezo yangu punde si punde...
 
nimechoka na hiyo website yao,naona wamekuwa wafanya siasa badala ya kazi.wabongo haya mambo huwa tunacopy tu au yanatoka kwenye akili zetu,huwa tunamawazo mazuri sana lakini utekelezaji wake ni kasheshe.hivi ni nani anayekwamisha hasa utekelezaji wa mawazo yetu ktk serikali au 10% huwa anagoma kwenda.lakini mengine ambayo yanamaslahi kwa walioshika mpini yanakwenda kama roketi.
 
Kasheshe siwezi kushangaa, lakini nadhani ni jambo zuri kuwa na wachangiaji wachache wenye kutoa mawazo yenye maana kuliko kushinda kukosoa kosoa tu. Wenyewe wanasema ni rahisi zaidi kuukata mti kuliko kupanda miche na kuisimamia ikawa miti baadaye!

yataka moyo.
 
Mimi nina mawazo kuhusu vitendea kazi, mwonekano, mawasiliano/lugha, uwajibikaji na mishahara.

1. Vitendea Kazo: Jeshi letu la Polisi linatakiwa kuwa na usafiri/magari maalum ya kufanya doria na kulinda usalama wa wananchi. Kuwepo kwa magari hayo itasaidia sana kwenye “Emergency Response” pale inapohitajika.
2. Mawasiliano/Lugha: Njia za mawasiliano ya simu au radio/emergency call pia zinatakiwa kuboreshwa. Maana hivi leo mwananchi akihitaji msaada wa polisi sijui hata ataanzia wapi? Na hata akifanikiwa kupata hao polisi, watafika vipi kumsaidia kama hakuna usafiri? Pia kwenye swala la mawasiliano, wengi wa mapolisi wetu hawana kauli nzuri kwa wananchi. Yaani ukikumbana na polisi hujui kitakutokea nini hwaswa au kitaanza kipi kati ya hivi – unaweza kutukanwa, kupigwa au kuomba rushwa waziwazi!
3. Uwajibikaji: Jeshi letu linatakiwa kuwajibika kazini na kufanya kazi kwa kufuata utaratibu. Hivi mapolisi wetu (detectives) huwa wanafanya uchunguzi wa kesi kweli ili kupata ushahidi. Samahani kama hapa nitakosea, lakini sina imani hata kidogo. Pia uwajibikaji unatakiwa uwe wa kweli, na sio kutumia takribani masaa mawili asubuhi kufungua kinywa! Au kuongezea masaa mengine mawili kwa chakula cha mchana (na bia juu!). Kwa ufupi, muda wa kazi unatakiwa utumike kufanya kazi.
4. Mishahara: Kwa upande mwingine siwezi kuwalaumu sana wapolisi wetu, maana ukweli ni kwamba mishahara na mafao yao ya huduma muhimu za kijamii ni kidogo sana. Hivyo swala hili linatakiwa kurekebishwa ili mapolisi wetu wasiwe na haja ya kukurupuka kuomba rushwa na/au kuchomoka kazini ili kufanya shughuli zao binafsi kujazilia pengo kati ya mshahara na hali halisi ya maisha.

I hope huyo IGP au walopewa jukumu hili wataviangalia vitu hivi na vinginevyo ili kuboresha Jeshi letu la Polisi.
 
Kaka Mwanakijiji,

Katika post hii natoa ushauri mmoja tu! mingine nitakuja nayo baadaye nashukuru katibu tarafa alitoa wazo kama lakwangu.


Kuna haja ya vitengo ambavyo havihitaji zile skills za kipolice sana zibinafsishwe... Naaminisha nini. Angali kwa mfano Usalama Barabarani na mambo ya Taa za Barabarani! Kuna haja gani ya polisi tuliyemtrain mambo mengi kusimama na kusimamia flowing ya magari barabrani?

Kila halimashauri inapokuwa jiji! kwa sasa Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam, wawe, wanaajiri metropolitan police ambao watakuwa pamoja na mambo mengine wanaangalia flowing ya magari barabarani, ikitokea taa zimezima au... jambo lolote wanahakikisha control ipo.

Kwa nini ni muhimu kufanya hivyo ni kwa sababu ifuatayo:-

  • Barabara za Jiji ni mali ya Halmashauri ya Jiji
  • Huduma za Jiji mbalimbali ziko chini ya jiji
  • Tunapowapa jiji kuhakikisha kwa efficient flow ya magari barabarani ni kazi yao! Watahakikisha wanakuwa no holistic approach ya kuhakikisha barabara za mitaani zinazosaidia barababra kubwa zinafanyiwa matengenezo kwa ajili ya kufanya mji usiwe na kero
  • Itakuwa vizuri kwamba majiji haya yatashindana jinsi yanavyohakikisha flowing ya magari kwenye miji yao eventually italeta ushindani na mwisho ufanisi
  • Itasaidia kwamba Jeshi hili la Polisi lililo chini ya Amri Jeshi mkuu linaajiri watu wachache wenye elimu nzuri kwa ajili ya kutatua mambo ambayo yanahitaji skills za kisheria na kipolisi kweli
  • Halimashauri za Jiji zitakuwa accountable na huduma za jamii za halimashauri zao, na kwa kuwa wao ndio wana hela za Maendeleo watajua wanunue taa za barabara, wawe na Helicopter za kuangalia congestions etc.
  • Halimashauri itakapoajiri kampuni mfano tu (say ultimate security, Secuiricor etc) hii ni mifano tu, wananchi watakuwa wanauwezo mkubwa sana kuangalia utendaji kazi wa hawa waheshimiwa na kwa kweli watakuwa makini sana.
  • Performance Key Indicators zita-be-defined vizuri na itakuwa rahisi kujua wanafanya kazi au ni Richmond nyingine!!! Mikataba itakuwa sio juu ya miaka miwili.
  • Kampuni litakalopewa kazi zinahakikisha pia magari mabovu yanaondolewa barabarani ndani ya nusu saa, saa moja, etc kulingana na umuhimu wa barabara, kama kawaida mwenye gari analipia gharama za breakdown...
  • Kwa vyovyote vile breakdown uchwara zitaondoka outmatically.

Halimashauri ambazo hazijawa na status ya majiji naomba ziwe outside of this scope, reason being kwamba bado hazina uwezo wa kifedha, kiutawala etc... wa Police kukasimu madaraka yao kwa vyombo dhaifu.
 
Kaka Mwanakijiji,

Katika post hii natoa ushauri mmoja tu! mingine nitakuja nayo baadaye nashukuru katibu tarafa alitoa wazo kama lakwangu.

Nawapata vizuri, na nitayajumuisha mawazo yenu yote kwa maana penye wengi pana mengi.. tuendelee kutoa mawazo ya kuliboresha jeshi letu la Polisi.
 
The police force Hq should modernise and reform itself in terms of operations of today’s policing and say bye to the days of beat cops or the warlord look in their land rovers and slinging of AK’s that’s an Assault rifle it has a beating zone( that’s why no scope for aimed shots) imagine a robbery in azikiwe street around 1600hrs the collateral damage that those weapons can cost is beyond imaginable im still surprised to see them in the streets in short that’s a war time weapon not a peace time( unless there is something IGP Mwema is not telling us it seems our forces adapt most from the brits why not go the full circle and form;
Specialist Crime Directorate
It should deal with serious, organised and specialist crime investigations and is divided into commands as follows:
Homicide Command; Made up of a number of major investigation teams (MITs) and is responsible for the investigation of homicide and other serious crimes. ‘man hunts’ for those suspects wanted for murder.
Forensic Services;
Child Abuse Investigation Team ;Made up of the Paedophile Unit, the Hi-Tech Crime Unit, the Child Abuse Prevention and Partnership Unit, the Ports Safeguarding Team and Major Investigation Teams.
Economic and Specialist Crime Command; including the Dedicated Cheque and Plastic Crime Unit, the Money Laundering Investigation Team, Financial Investigation Development Units, the Specialist Crime Operations Team, the Stolen Vehicle Unit, the Arts and Antiques Unit, the Police Central e-crime Unit, the Wildlife Crime Unit, the Extradition and International Assistance Unit, the Criminal Justice Protection Unit, and the Regional Asset Recovery Team.
The Serious and Organised Crime Group; tackles serious and organised crime, life-threatening crimes in action and those who inflict human misery on the people of Tanzania through fast time pro-active response’. The group is made up of the Central Task Force, the Projects Team, covert policing, the Kidnap and Special Investigation Unit, the Hostage and Crisis Negotiations Unit and the Intelligence Support Unit.
Central Operations
Units in this department include: Central Communications Command, Public Order Operational Command Unit, Traffic Operational Command Unit , Traffic & Transport Criminal Justice Unit Transport Operational Command Unit ,Operational Support OCU, comprising Mounted Branch ,Air Support Unit, Dog Support Unit, Marine Support Unit ,Specialist Firearms Command, Territorial Support Group
Specialist Operations
The Counter Terrorism Command, The priority of this command is to keep the public safe and to do everything they can to ensure that Tanzania remains a hostile environment for terrorists. Their responsibilities include: bringing to justice anyone engaged in terrorist or related offences, providing a proactive and reactive response to terrorist and related offences, preventing and disrupting terrorist activity, gathering and exploiting intelligence on terrorism and extremism in Tanzania

questions where in hell do we get the kind of money to do all these gucci stuff one might wonder..

my suggestion would be to form a police force association fund where the area known to all as oysterbay police to turned into a complex(proper shopping mall,appartments offices e.t.c )yet maintain the police station .All the proceed of that venture will go directly to the police force fund of which administered correctly will be used to supliment the force with things the central government cant do even lead them to be more independant
i think,then again what do i know im just a mzalendo
 
Nilipo zungumzia muundo wa jeshi letu la polisi,nilikuwa na maanisha kuwa kama itakubalika kuwa na polisi wa kila mkoa/halimashauri itasaitia kila mkoa kujua kipaumbele chao ni nini kwa wakati huo,hivyo itasaidia kuimarisha vitendea kazi pamoja na miundo mbinu mingine.
Nimeona hapa kijijni kwetu jinsi halimashauri yetu inavyotushirikisha ktk shughuli mbalimbali za ulinzi na usalama kwa watu kutoa maoni na jinsi ya kuboresha utendaji kazi.
Si rahisi kwa IGP kujua kila tatizo la kila mkoa na kutoa kipaumbele ktk utekelezaji,lakini kama jeshi likimilikiwa na mkoa ni rahisi kutatua matatizo yao wao wenyewe kuliko hivi sasa.
Haya matatizo ya kulingiza jeshi ktk siasa au kufuata matakwa ya mtu fulani hayata kuwepo kwani wamiliki na waajiri wao ni wananchi wa hiyo sehemu.
Tatizo ni serikali inajilimbikizia kazi badala ya kusimamia utekelezaji wake,ndio maana kila siku ni matatizo tu yanayoongelewa.kwa zipa madaraka kamili halimashauri serikali yetu itapunguza kashifa zisizo za lazima.
 
Jeshi letu la Polisi ni miongoni mwa idara zilizo organised kuliko idara nyingine zote za Tanzania. Kuna mpangilio na idara zote polisi, lakini kinachohitajika tu ni pesa za mishahara bora na nyumba bora kwa polisi. Hata kikosi cha kuzuia rushwa ambacho hakifanyi vizuri kwa sasa ni kwasababu ni cha kisiasa. Polisi wana kitengo cha CID na kingeweza kufanya kazi nzuri kuliko kitengo cha kisiasa. Ningependa mtu alete hapa organization nzima ya polisi maana watu wengi hawaelewi lakini polisi ni kitengo kilicho pangwa kuliko vyote Tanzania. Huwezi kubomoa kitu bila kuwa na plan na huwezi kuwa na plan nzuri kuliko hii ya polisi ya sasa hivi ni plan ya kisasa sana
 
Miaka nane iliyopita tulianza kuzungumzia hili; kwa hiyo ninapowasoma watu wanaolalamikia polisi nawaelewa wala siwapuuzii kwani hata mimi mwenyewe nimeandika habari za kutosha juu ya polisi na haja ya kuwa na weledi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom