Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,731
- 40,838
Wengi wetu tumewahi kwa namna moja au nyingine kugusana na jeshi la Polisi kwa mema au kwa ubaya. Na kama siyo sisi wenyewe tunawajua watu kadhaa ambao wamewahi kuwa na jambo Polisi. Yawezekana wapo ambao hawakufurahia utendaji kazi wa jeshi la Polisi na wangependa iwe tofauti.
Baada ya kwenda sehemu mbalimbali duniani na kuona utendaji kazi wa majeshi mengine bila ya shaka kuna kitu na sisi tunatamani kuona kinatokea katika kulibadilisha Jeshi "letu" la Polisi.
Nimeombwa na mtu mmoja (ndani ya jeshi hilo) kusolicit mawazo ya wana JF kuhusu mabadiliko muhimu ndani ya Jeshi hilo hasa linapojiandaa kukabili matatizo ya karne yetu hii ya "mawasiliano". Tayari binafsi nilishatoa maoni yangu miaka miwili iliyopita ambayo baadhi yalifanyiwa kazi kwa kuunda "Kanda Maalum" ya Dar. Hata hivyo bado kuna mambo mengi sana yanahitajika kuweza kulifanya jeshi hilo kuwa karibu zaidi na wananchi, la kisasa zaidi, na ambalo linafuata sheria zaidi na lenye kuweza kutimiza jukumu lake la "Usalama wa Raia na Mali zao".
Mada itafuatiliwa na baadhi ya wahusika na wataalam wa UDSM ambao tayari walikabidhiwa jukumu la kupendekeza mabadiliko ya Jeshi hilo. Maeneo makubwa matatu yanahitaji kuangaliwa.
- Sheria ya Jeshi la Polisi - Police Ordinance
- Muundo
- Majukumu
Haya wana JF huo ni wakati wetu wa kushine! ni rahisi kukosoa zaidi lakini sasa ni wakati wa kujenga; tutaweza changamoto hii?
M. M.