Jeshi la Polisi na hasa Trafiki lifumuliwe na kuundwa upya

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,826
35,827
Kwa muda mrefu jeshi la polisi na hasa kitengo cha usalama barabarani limekuwa likilalamikiwa kwa kushamiri kwa vitendo vya rushwa.

Si polisi wa vyeo vidogo au vikubwa wote lao moja.

Inafahamika jitihada wafanyazo polisi vitengo vingine, ili wapate kupangiwa kitengo hiki cha walamba asali.

Wameshindwa kuwa wabunifu au hata kuwa na mkakati wowote endelevu wa kuzuia ajali. Wamejikita katika mikakati zimamoto yenye nia ya kuongeza tu mianya ya rushwa.

IMG_20220729_082949_635.jpg


Ni vizuri kikaja kitengo kipya cha jeshi hili chenye:

1. Kujikita kwenye kushughulika na yaliyo ainishwa waziwazi. Iwe kwenye magari kama magari tu. (Majukumu ya Latra, TRA au taasisi zingine yasiwe na cha kufanya na polisi).

2. Ukaguzi wa magari usiwe kwa utashi wa askari mmoja mmoja kama anavyojisikia yeye. (Nini kinakaguliwa kwa siku kiwe kwenye order ya siku ya jeshi na sawia kwa nchi nzima).

3. Kwenye kituo kimoja cha ukaguzi kusisimamishwe zaidi ya gari moja.

4. Malipo ya faini yasiwe na kamisheni yoyote kwa polisi husika. Malipo ya faini yasiwe ni mapato ya kitengo cha traffic kiasi cha wao kujiona kuwa wanayo haki ya kutumia sehemu ya mapato hayo kama yao.

5. Polisi waachane na habari ya ukaguzi wa ubovu wa magari wasiokuwa na ujuzi nao. Hawa si mafundi magari. Ufundi magari ni kazi rasmi ya wenyewe.

Kinatakikana kikosi kipya kitakacho yaangazia haya kwa uwazi kwa magari yote yakiwamo ya polisi, umma, serikali na watu binafsi.

Katika kikosi kipya askari wake wa vyeo vyote ni muhimu wasidumu bila ukomo.

Wachafu waliomo mle sasa wasiachwe hivi hivi, bila ya kufuatiliwa vyanzo vya ukwasi walio nao.

IMG_20220801_162824_138.jpg


Pichani kama nawaona wabaya wetu wakiwa na mwingi msongo wa mawazo.

Asante Mh. Kinana kwa hakika kwao hatimaye kimenuka!
 
Back
Top Bottom