Jeshi la polisi mtaacha lini kutoa report zenye mkanganyiko? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la polisi mtaacha lini kutoa report zenye mkanganyiko?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by satellite, Mar 13, 2012.

 1. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa mara nyingine tena jeshi la polisi limeingia kwenye kutoa report tata zinazoibua maswali juu yake,kwenye sakata la kuibia naibu waziri Malima polisi wamesema aliyeiba sio mwanamke lakini vitu vilivyoibiwa vimekutwa kwa mwanamke swali linakuja kwani huyu naye sio mtuhumiwa wa kupokea vitu vya wizi tena vyenye thamani kubwa?
  Pili wamekanusha Malima hakuwa na silaha aina ya SMG ambayo ni vita,siku ya tukio TBC walionesha Malima mwenyewe akikiri alikua na silaha 2 na alizitaja moja ikiwa bastora na nyingine SMG tena alisema hii nyingine ni ya hatari ila mwizi hakuijua ndo maana aliiacha,Je polisi mnasema uongo kumkinga nani?
  Polisi achane kutoa conclusion ya taarifa msizokua na uhakika nazo maana mmekana kuwa aliyeiba siyo mwanamke ila hamjamtaja alyeiba wala kutoa ushahidi.jamii inakosa imani na nyie na mnakua mnatoa taarifa kama vile ziko cooked tena na watu ambao hawajui jinsi ya kucook data.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  HAdi hapo watakapo ajiri wenye busara!!!!!
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hakuna weledi kwenye hilo jeshi, limejaa wala rushwa na kubambikiza kesi kwa raia. Mwema alipewa kuongoza jeshi kwa uswahiba ndio maana ameachia tu mambo yanajiendea tu hovyo. Mfano mzuri wachunguze askari jinsi uniform zao zilivyochakaa, na viatu wanavaa vya kichina. Hii ni ishara tosha uongozi mbovu
   
 4. M

  Mat.E Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jeshi la polisi ni noma! Kiambiwa na mkubwa ua huyo,naua! Kiambiwa sema likuwa naleta furugu, nasema! Kiambiwa acha hiyo,potesea, naacha,napotesea! Kiambiwa bambikisa, nabambika! Kiambiwa sema mekula sumu, nasema! Sasa meambiwa sema simji haiko,MESEMA!
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,783
  Trophy Points: 280
  Mafunzo wanayopewa hawa askari wetu ni mafunzo ya kuwa na roho mbaya dhidi ya raia.
   
 6. B

  Burebure Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kazi ya polisi ni Ulinzi wa raia na mali zao lakini sasa naona kuwa Kazi ya Polisi ni Ulinzi wa Wahalifu na Mali zao!
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaaaa!!! Umenifurahisha sana!

  Sena hakuna manamke loiba, nasema hifohifo,

  Ulishawahi kusikia kibaka anajua aina za silaha na asiibee?

  Kwamba hii ni simjii, hii ni shotgani, hii ni gobole!!! Halafu anaziona na anaziacha!
   
 8. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  ndio yale yale magari yao yanavuja madawa ya kulevya kila mara wakikamata mzigo, juzi tena wamekamata kilo tatu ikafika kituoni ikiwa kilo moja unusu - sababu ya utofauti inaelezewa walikadiria tu wakati wanatangaza, lakini baada ya kupima kwenye mzani wamehakikisha uzito,
  siku tutawataja kwa majina wahusika,
   
Loading...