dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya SMG ikiwa na magazini moja yenye risasi 22,baada ya watu watatu waliokuwa wamepanda pikipiki moja kuitelekeza, kutokana na kuwaona polisi waliokuwa katika doria,huko wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishina Msaidizi Hamisi Issa Suleimani amesema kuwa,tukio hilo limetokea katika kijiji cha Utyatya,kata ya kipanga wilayani Sikonge,baada ya wasamalia wema kuwashukia watu hao na kutoa taarifa kwa jeshi hilo wilayani Sikonge,ambapo silaha hiyo ilidhaniwa ingefanya uhalifu wa utekaji magari.
Katika hatua nyingine Kamanda Hamisi Suleimani amesema kuwa upelelezi wa awali unaonyesha silaha hiyo imekuwa ikitumika katika wilaya ya Uyui na Sikonge,kwani hata pikipiki hiyo aina ya Sanlg No,MC 230 AKW,iliporwa kwa mwananchi mmoja mkazi wa kijiji cha Mwampapa ajulikanaye kwa jina la Sylivester Jandika,ambapo pia yalifanyika mauaji.