Jeshi la polisi mkoani Morogoro lakamata silaha ya kivita aina ya AK47

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu wakiwemo watu sita wanaodaiwa kukutwa na silaha moja ya kivita aina ya AK47 ikiwa na Magazini mbili zilizokuwa na risasi 31 huku jeshi hilo pia likiwakamata wahamiaji haramu saba raia wa Ethiopia wakiwa wametelekezwa kichaka kando ya barabara ya Morogoro Dar es Salaam katika kijiji cha Maseyu wilaya ya Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro kamishna msaidizi wa polisi SACP Wilbroad Mutafungwa amesema watu hao wamekamatwa wakati wa doria za kawaida za jeshi hilo za kuwasaka na kuwakamata wahalifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Aidha kamanda Mutafungwa amesema kuwa jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata Bangi magunia sita pamoja na pakiti 546 za pombe haramu aina ya origino iliyokuwa kwenye vifungashio vilivyopigwa marufuku na serikali.
 
Back
Top Bottom