Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lamshikilia kijana wa miaka 32 kwa tuhuma za mauaji

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Bariki Kajuni mwenye miaka 32 ambaye ni mkazi wa Makambako, Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za kosa la mauaji ya Ansalemo Stawi Kisheria.

Ansalemo Stawi Kisheria alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Zahanati ya Isangawana kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na mtuhumiwa.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendelea na msako na mnamo tarehe 10.09.2020 majira ya saa 17:30 jioni huko Kitongoji na Kijiji cha Mgololo Mufindi, Wilaya ya Mafinga, Mkoa wa Iringa askari Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na askari wa Mafinga walimkamata mtuhumiwa".

Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
 
Kinachokuchekesha
Inachanganya.

Jeshi la polisi Mkoa Mbeya

Limemkamata mtuhumiwa wa Njombe

Limemkamatia mkoa wa Iringa.


Sasa hawa polisi wa Mbeya walipewa jukumu hilo?

Watalaam wa mambo ya intelijensia watasaidia kutuelewesha
 
Inachanganya.

Jeshi la polisi Mkoa Mbeya

Limemkamata mtuhumiwa wa Njombe

Limemkamatia mkoa wa Iringa.


Sasa hawa polisi wa Mbeya walipewa jukumu hilo?

Watalaam wa mambo ya intelijensia watasaidia kutuelewesha
Mtoa post kachanganya files
 
Inachanganya.

Jeshi la polisi Mkoa Mbeya

Limemkamata mtuhumiwa wa Njombe

Limemkamatia mkoa wa Iringa.


Sasa hawa polisi wa Mbeya walipewa jukumu hilo?

Watalaam wa mambo ya intelijensia watasaidia kutuelewesha
... ni sawa. Mtuhumiwa ni mkazi wa Makambako/Njombe kaenda kufanya mauwaji Mbeya then kakimbilia Mafinga/Iringa (kujificha?). Maelezo yako consistent; no contradiction.
 
Mtoa post kachanganya files
... sio Kurzweil ninayemfahamu hapa JF! Yuko sahihi! ... Mtuhumiwa ni mkazi wa Makambako/Njombe kaenda kufanya mauwaji Mbeya then kakimbilia Mafinga/Iringa (kujificha?). Maelezo yako consistent; no contradiction.
 
Inachanganya.

Jeshi la polisi Mkoa Mbeya

Limemkamata mtuhumiwa wa Njombe

Limemkamatia mkoa wa Iringa.


Sasa hawa polisi wa Mbeya walipewa jukumu hilo?

Watalaam wa mambo ya intelijensia watasaidia kutuelewesha
Mbona suala liko clear,
-Mtuhumia: mkazi wa Makambako , Njombe
-Mauaji: yamefanyika Mbeya
-Muuaji kamkibilia: Kijiji cha Mgololo, Mufindi Iringa.
-Polisi wachunguzi: mauaji yalipotokea Mbeya
-Polisi wakamataji: jurisdication ya Polisi wa Iringa

Huo ndio utaratibu Polisi Mbeya hawawezi kukamata mtuhumiwa mkoa mwingine bila kuarifu mkoa husika kwa utaratibu wa kipolisi.
 
Back
Top Bottom