Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, linawashikilia watoto sita Raia wa Ethiopia akiwemo mwenye umri wa miaka mitano kwa siku 20

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha,linawashikilia watoto sita RAIA wa Ethiopia akiwemo mwenye umri wa miaka mitano baada ya kukuta wamehifadhiwa kwenye nyumba ya MTU binafsi eneo la Ngureso katika halmashauri ya jiji la Arusha.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa,Jonathan Shanna amesema kuwa watoto hao wenye umri wa miaka mitano hadi kumi na mbili waligundulika February 20 mwaka huu kuhifadhiwa nyumbani kwa Amina Ally na Mohammed Mahamudu mkazi wa Ngusero jijini Arusha.

Kamanda Shanna amefafanua kwamba polisi walipata taarifa kuwa nyumbani kwa Amina kuna watoto wamefichwa na kwamba watoto hao walikuwa hawajui lugha yoyote za hapa nchini ndipo polisi walipovamia katika nyumba hiyo na kufanikisha kuwakuta watoto hao sita akiwemo mwenye umri wa miaka 5.

Amewataja watoto hao kuwa ni ,Rukia Tajibu Ismail(12),Zainabu Tayibu(11)Kuruthunu Tayibu(10)Yimaji Tayibu(9)Arafat Tayibu (5) pamoja na Umayi Tayibu wote wakiwa RAIA wa Ethiophia.

Aidha Kamanda Shana ameongeza kuwa Mara baada ya kuwahoji watoto hao wamedai kuwa walitoroshwa kutoka nyumbani kwa mama yao nchini Ethiopia ili wapelekwe Afrika kusini kwa baba yao kupitia Nairobi Nchini Kenya na wameingia nchini kupitia mpaka wa Namanga.

Aidha kamanda Shana amesema kuwa wakati wanaendelea kuwahoji watoto hao alijitokeza MTU mmoja aitwaye Ateyibo Isumail Yusuf(45) kutoka nchini Afrika kusini akidai kwamba yeye ni baba wa watoto hao..

Hata hivyo polisi walimtilia shaka na kuamua kumshikilia katika kituo cha polisi baada ya kubaini kwamba hana kibali halisi cha kuingia nchini .

Kamanda Shana amedai kuwa polisi wamechukua vipimo vya vina saba kwa watoto hao na MTU huyo anayedai ni baba wa watoto hao ili kujiridhisha kama kweli ni baba wa watoto hao.

Polisi bado inawasiwasi kuwa huenda watoto hao walikuwa wanasafirishwa kwa ajili ya kufanyiwa biashara ya haramu ya binadamu kupitia Nchi ya Tanzania.

Kamanda Shana amesema kwa sasa jeshi hilo linawasiliana na askari wa kimataifa (Enter pool) kwa ajili ya kuwarejesha watoto hao nchini kwao Ethiopia na kwamba Eteyibo Isumail anayedai ni baba wa watoto hao atafikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini bila kufuata sheria.

Watoto hao ambao walikamatwa tangu February 20 mwaka huu wanafikisha siku 19 wakiwa bado wanasota mahabusu ya jeshi la polisi jijini Arusha wakisubiri uchunguzi wa jeshi la polisi .

Hata hivyo mdau wa haki za binadamu,bi Hasna Ally mkazi wa jijini Arusha amelitaka jeshi hilo kuangalia njia sahihi ya kuwasaidia watoto hao kuwa Huru kuliko kuendelea kuwashikilia kutokana na umri wao kuwa mdogo.

Ameiomba Ofisi ya RCO Arusha kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo ili watoto hao waweze kukabidhiwa kwa Wazazi wao.
IMG-20200311-WA0077.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ethiopia ni nchi tajiri lakini inaongoza kwa raia wake kukimbia nnchi hapa kuna tatizo pia na sisi tujifunze.
 
Maswali ya msingi ambayo hayajatoleea maelezo
1.) Amina mohammed ambaye ndiye kakutwa na hao watoto yuko wapi?
2.) Amina aliyekutwa na watoto katoa maelezo gani juu ya hao watoto?
 
Mmh Human trafficking,
Halafu hao watoto kama ni wa mama mmoja inakuaje wamepishana mwaka mwaka tu yaan mama yao alikua anazaa kila baada ya miezi!!?

Kuna kitu hakipo sawa hao watoto wamesaidika kutoka kwenye biashara ya utumwa.
 
Back
Top Bottom