Jeshi la Polisi Matukio ya watu kupigwa Risasi yameongezeka sanaaa!

cement

JF-Expert Member
May 5, 2012
581
195
Jeshi la Polisi sijui mnatwambia nn watanzania kama kila kukicha watu wanapoteza maisha kwa kupigwa Risasi wakati nyie mpo kuna siri ani kati yenu ya hawa wauaji inauma sana juzi ndugu yangu anafanya biashara ya Mpesa kapigwa risasi jirani kabisa kama hatua ishirini tu kutoka kituo cha polisi tumechoka na matamko yenu ss hivi mnasema wanaomiliki silaha wazirudishe wenyewe mko wapi mpk watu wanazimiliki pasipo vibali!

Mkuu wa Jeshi la polisi tuambie nn kinaendelea?? Katika hili mnatumaliza hii week ya pili kila siku watu wanauawa tumekosa imani na Jeshi la Polisi kama flani inayotizamana na kituo cha polisi mtu anauawa na nyie mnaangalia khaaaaa haya ni maajabu ya Tanzania.
 
CRN

Member
Oct 24, 2012
60
0
kuna askari gani mjinga wa kukukamatia silaha kipindi hiki? JK aliwaahidi kuwapatia mishahara mikubwa wakati anatafuta kura mwaka 2005 na alipoingia madarakani akapata ushauri kutoka kwa MARRY NAGU kuwa hakuna haja ya kuwapa pesa nyingi askari kwa kuwa watalewa na kusahau majukumu yao,haya yanayotokea ni matokeo ya AHADI [PROMISE],na ukitaka kujua AHADI inaposhindwa kutekelezwa kipi hutokea,rejea MAANDIKO MATAKATIFU,kwa maisha magumu waliyonayo polisi kwa sasa,si rahisi kupambana na uharifu wakati familia haina chakula,hakuna Ada ya shule kwa watoto,stress za ndugu zao n.k,nikisikia Polisi wanaogoza kwa kula Rushwa huwa sioni ajabu sana kwani waliowaandalia maisha hayo ni watawala wetu wenyewe ambao ni Serikali sikivu ya CCM.
 
katalina

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
262
0
Maoni yangu: Kwanza pole ndugu yangu uliyepata mkasa huo, lakini ningependa kusema kwamba wanaopiga watu kwa risasi ni watoto wetu, jirani zetu, wajomba zetu etc. Hivyo ni vizuri tukaimarisha familia zetu. Unategemea nini kuwa na watoto watano, sita, saba, nane etc na hawana kazi wakati huohuo wanataka kula. Mimi naamini kila mtu akiwa na familia anayoweza kuitunza vizuri twaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa kadhia hii. Huu ni mtizamo wangu badala ya kulalama na polisi....
 
  • Thanks
Reactions: CRN

Dogo1

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,358
2,000

Umenena! Hata wezi ni watoto wetu, ndugu zetu, majirani zetu n.k. Ukiwa na mtoto mwizi unafurahia anapoleta vitu ambavyo unaamini hana uwezo navyo na haturipoti polisi. Tunahitaji maadili yaliyotukuka kuanzia ngazi ya familia hadi huko makazini
 
moshingi

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
278
0
Jeshi la Polisi sijui mnatwambia nn watanzania kama kila kukicha watu wanapoteza maisha kwa kupigwa Risasi wakati nyie mpo kuna siri ani kati yenu ya hawa wauaji inauma sana juzi ndugu yangu anafanya biashara ya Mpesa kapigwa risasi jirani kabisa kama hatua ishirini tu kutoka kituo cha polisi tumechoka na matamko yenu ss hivi mnasema wanaomiliki silaha wazirudishe wenyewe mko wapi mpk watu wanazimiliki pasipo vibali!

Mkuu wa Jeshi la polisi tuambie nn kinaendelea?? Katika hili mnatumaliza hii week ya pili kila siku watu wanauawa tumekosa imani na Jeshi la Polisi kama flani inayotizamana na kituo cha polisi mtu anauawa na nyie mnaangalia khaaaaa haya ni maajabu ya Tanzania.

Hakuna nchi duniani ambayo haina uhalifu kabisa ndiyo maana karibia kila nchi inayo idara/jeshi la polisi ama watu wanaofanya kazi ya kulinda usalama wa watu na mali zao... hata hivyo hakuna nchi yeyote ambayo imefanikiwa kuzuia uhalifu kama vile mauaji/armed robbery kwa asilimia 100. Jambo kubwa linalofanyika ni kupunguza na ikitokea upelelezi ufanyike kwa haraka na wahusika wafikishwe mahakamani kwa haraka. Hata hivyo kabla ya kuwalaumu Polisi ni lazima tujue sababu ya kuongezeka kwa uhalifu. Wengi tunakubaliana kuwa pengo kati ya wale walionacho na wasiokuwa nacho limeongezeka sana...wapo watu ambao wamepoteza kabisa matumaini ya kuwa nacho kwa kutumia njia halali, ndio maana utakuta wale wasomi wanaghushi hundi au kuiba kupitia mtandao, bali wale wasio na kisomo na ambao wamekata tamaa ya kupata mali/fedha kupitia njia halali kutokana na mfumo uliopo kutokuwa fair basi huamua kutumia silaha ili kujinyakulia kwa nguvu mali/fedha kutoka kwa yeyote. HATA HIVYO IELEWEKE KWAMBA HAKUNA SABABU YEYOTE INAYOTOSHA KUHALALISHA UHALIFU. Kila mtu anayodhima ya kupambana na uhalifu wa aina yeyote pale alipo na sio kuwategemea Polisi 100%, wao ni binadamu, wanayo mapungufu mengi kama ambavyo sekta nyingine walivyo kwa mfano wagonjwa hufa hospitalini lakini ni nadra kusikia madaktari wakilaumiwa, majengo huporomoka, barabara huharibika bila ya wahandisi kusakamwa, mikataba mibovu yenye kuua mamilioni ya watanzania kwa kipindi kirefu lakini wanasheria hawalaumiwi sana..basi na upolisi ni taaluma, tuiheshimu na kuisaidia ili sote tuwe salama. Hata hivyo tusiache kukosoa tabia zisizofaa za askari wetu hawa, lengo letu liwe ni kujenga wala si kutweza...mtu yeyote ukimtweza kamwe hatakusikiliza. Tuwasaidie ili chombo hiki kiwe huru chini ya katiba mpya ijayo, kituhudumie vizuri na kwa haki.
 
  • Thanks
Reactions: CRN

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,274
2,000
Miji yetu inakuwa kwa kasi kimaendeleo na halikadharika uhalifu unaongezeka kwa kasi, hiyo ni sifa ya miji mikubwa karibu yote duniani uhalifu uko juu, na ni jukumu la serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama, kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu. binafsi sifurahishwi na maandalizi ya vyombo vya ulinzi na usalama ktk kukabiliana na hali hiyo. tazama mkoloni alivyopanga kambi za polisi na vituo vya polisi, wakati mji ukiwa mdogo, na tizama sisi tulivyojiachia huku mji ukipanuka bila mpangilio wa kambi na vituo vya polisi, hatuna Dog section iliyokubwa na ya kisasa kwa ajiri ya kuzalisha na kutunza mbwa bora kwa ajili ya ulinzi imara wa raia na mali zao, mbali ya kambi za polisi kilwa road, ukonga field force, buguruni polisi, magomeni polisi, msimbazi polisi, oyerstebay polisi, chang'ombe polisi, kunduchi polisi , utaona baaasi hakuna teena ukamataji wa maeneo makubwa na kujenga kambi za askari,vituo vya polisi na uzalishaji na utunzaji wa mbwa na farasi , nasisitiza ulinzi madhubuti katika miji yeyote mikubwa doria ya mbwa na farasi haiepukiki. doria za magari na matengenezo ya magari jamii ikiona inahudumiwa ipasavyo aishindwi kuchanggia ,magari mabovu yaliyoegeshwa kwenye vituo vya polisi jamii inaweza kuyatengeneza yakawatumikia wakiona /wakionyeshwa ni kwa ajili ya usalama wao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom