Jeshi la Polisi: Madai ya Makonda kuuawa, kama yupo ‘siriasi’ aende Polisi

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amemshauri Paul Makonda kwenda kituo cha polisi kuripoti tuhuma alizozitoa mtandaoni, ikiwamo ya kudai kutishiwa maisha.

“Sijaongea naye (Makonda), lakini kupitia ninyi (vyombo vya habari), namshauri aende kituo chochote cha polisi endapo madai aliyoyatoa yana ukweli. Inategemea yeye (Makonda) anakaa wapi, lakini aende kituo cha polisi cha karibu kwa ajili ya kutoa maelezo ya madai yake,” alisema Muliro.

Juzi katika mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa zilizoibua mjadala zikimhusu Makonda, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwamo iliyokuwa na kichwa cha habari, “nafahamu kuna mkakati unaoratibiwa na makundi matano kuangamizi maisha yangu.”

Hata hivyo, Kamanda Muliro alisisitiza umuhimu wa Makonda kwenda kutoa taarifa polisi, akisema hivi sasa mifumo inafanya kazi vizuri, hivyo akipeleka jambo lake hata kwa maandishi litashughulikiwa.

“Kazi yetu polisi kuchunguza malalamiko yoyote ya kijinai, lakini jambo linalochunguzwa lazima kuwepo kwa ushahidi wa kuridhisha. Narudia kama kweli amelalamika na madai yana ukweli basi aende kituo cha polisi cha karibu,” alisema Kamanda Muliro.

Source: Mwananchi

Ngoja tuone ..
 
jamaa wanafanya kazi kwa maelekezo ya kutoka juu
angekuwa mpinzani angeambiwa ajisalimishe
 
Hao watu unaowazungumzia wana maarifa ya kutosha kujua wafanye nini, kama hana imani basi ofisi za Serikali zingefungwa, kama watu wanakwenda afu wewe unasema huna imani, mtu mmoja akisema hana imani lakini robo tatu wakienda na kupata huduma nani tumfuate hapo,” Muliro.
Labda anataka afuatwe nyumbani kwake
 
Muda mfupi baada ya RC wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuandika mtandaoni kuwa kuna makundi matano yanamuwinda ili kumuua, Jeshi la Polisi limesema kama kweli ana hofu anatakiwa aende kutoa taarifa Kituo cha Polisi.

Akizungumza na Kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema: “Raia yeyote wa nchi hii ana haki ya kutoa taarifa Polisi kama ni kweli na ni jambo ‘serious’.

“Mimi sijaliona hilo tamko lake, najua watu ambao wapo serious wanaenda Polisi. Siwezi kushauri kuhusu hilo, watu unaowaongelewa wana weledi, wanajua taratibu, na ninajua wanajua, kwanza siamini, wana maarifa ya kutosha.

“Hao watu unaowazungumzia wana maarifa ya kutosha kujua wafanye nini, kama hana imani basi ofisi za Serikali zingefungwa, kama watu wanakwenda afu wewe unasema huna imani, mtu mmoja akisema hana imani lakini robo tatu wakienda na kupata huduma nani tumfuate hapo,” Muliro.

Source: CLOUDS FM

Pia soma:

Paul Makonda: Kuna makundi matano yanataka kuniua, likiwemo wanaotafuta kulipa kisasi kwa Wasaidizi wa Magufuli

Huyu wamnyonye mavi kabisa aliumiza wengi kipindi cha mwendazake! Washikilie hapo hapo wasiachie
 
Back
Top Bottom