johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,615
- 141,443
Polisi mkoani Morogoro inawashikilia wanachama watatu wa Chadema walioghushi barua za utambulisho wakijifanya ni wanachama wa chama cha SAU na kutaka kuchukua fomu za kugombea ubunge kwa njia ya udanganyifu.
------
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa, alisema jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Sheila Lukuba, akitilia shaka barua ya utambulisho kutoka kwa Edga Msigwa akidai kuwa ni mwanachama wa SAU.
“Tulipopata taarifa ya kutilia shaka kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi, tulifika ofisini kwake na tulipokagua hiyo barua tulikuta ina mapungufu na hata tulipochunguza tumebaini chama cha SAU hakina hata ofisi ya wilaya au mkoa ndani ya Morogoro,” alisema Mutafungwa.
Alisema baada ya kumhoji alikiri kuwa si mwanachama wa chama hicho bali alipewa barua hiyo na Christian Daniel ambaye ni mratibu wa uchaguzi wa madiwani wa manispaa ya Morogoro pamoja na dereva wa mgombea ubunge Jimbo la Morogoro Mjini kupitia CHADEMA aliyetambulika kwa jina moja la David.
Kamanda Mtagungwa alisema watuhumiwa wote watatu wanaendelea kuhojiwa ili kujua sababu zilizopelekea kufanya udanganyifu huo.
“Tunamshikiria huyu ni dereva wa Devotha Minja, mgombea kupitia CHADEMA, ndiye alitumia gari ya mbunge huyo kumbeba Edga Msigwa, ambaye alikuwa na barua ya kughushi kwa hiyo tumemkamata yeye pamoja na gari alilolitumia,” alisema Mutafungwa.
IPPMedia