Jeshi la Polisi linavyoendelea kuwapasua vichwa Marais wa JMT

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,476
37,749
Tarehe 12.12.2021 katika chuo cha Polisi Dar es salaam yalifanyika mahafari ya kuhitimu mafunzo ya Uofisa maafisa wa Polisi zaidi ya 700. Mgeni rasmi katika mahafari hayo alikuwa Rais wa JMT mama yetu Samia Suluhu Hassan wengi wakifupisha SSH.

Katika hotuba aliyotoa mgeni rasmi alionesha kukerwa sana na mwenendo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi hususani kitengo cha Usalama barabarani. Alitolea mifano matukio yaliyowahi kumkumba yeye binafsi yakihusisha polisi na yote yalihusu utendaji mbovu wa kikosi cha Usalama barabarani.

Nikirudi nyuma awamu iliyopita, kila alipopata nafasi ya kushiriki matukio ya kipolisi, Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli (JPM) hakuacha kulaumu na kukemea utendaji mbovu wa jeshi la Polisi lakini yeye alijikita kwenye vikosi vingine vya polisi hasa manunuzi na upelelezi. Yeye alifikia hatua ya kutamka wazi kati ya taasisi zinazompasua kichwa ni jeshi la Polisi.

Kwa hiyo ni dhahiri marais wanaumizwa vichwa na utendaji wa chombo hiki ambacho kina kazi kubwa ya kulinda maisha ya Watanzania na Mali zao.

Leo naomba niongee na MAMA kuhusu utendaji wa chombo hiki. Mama yetu anasikitishwa na utendaji wa polisi hasa traffic na kumtaka IGP achukue hatua. Ni jambo jema kwa kiongozi wa nchi kutaka vyombo vinavyomsaidia kazi kutenda kazi kwa weledi na hivyo kumpa sifa yeye, kinyume chake lawama zote za ubovu wa taasisi hii unarudi kwenye utendaji wake yeye mwenyewe.

Lakini Leo naomba kumwambia Mheshimiwa Rais kama anawashangaa traffic basi ni kwa vile hajawahi kukumbana na Wapelelezi wenyewe wanawaita CID. Hawa ni balaa zaidi ya traffic wanaohusika na matajiri wenye magari. CID wanahusika na Watanzania wa aina zote wakiwemo matajiri wachache na maskini ambao ni wengi nchini kwa sababu ya kudhulumiwa kijinai.

Kwanza niongelee chanzo cha matatizo ya traffic na CID kulalamikiwa kwa utendaji usioridhisha. Chanzo cha tatizo ni viongozi wao wanaowaongoza traffic na CID ngazi ya wilaya. Nikianza na wakuu wa traffic wilaya hawa wamewageuza askari wa chini yao kuwa ATM zao kila jioni kwa vile wao hawaendi barabarani.

Kwanini hatushangai kuona Wakuu wa traffic wilaya hawasimamishi magari barabarani lakini wana maisha ya juu kuliko askari wao wanaosimama kila siku barabarani na kupokea elfu mbilimbili? Ni kwamba kila askari ana kiwango anachokipeleka kwa bosi jioni.

Yaani yeye anakaa ofisi lakini jioni anapata kilichokusanywa barabarani. Ukiongea na askari wengi wadogo wa barabarani wanalalamika kuhusu hili lakini kwa vile na wao ni sehemu ya wafaidikaji hawawezi kukata mkono unaowalisha.

Nikija upande wa CID hali ni hiyo hiyo, Wakuu wa upelelezi wilaya ni chanzo cha utendaji mbovu wa CID. Kwa uchunguzi mdogo niliofanya kwa kuwauliza askari ambao ni marafiki zangu, kikanuni Mkuu wa Upelelezi wilaya ndiye mpelelezi Mkuu na wao ni wasaidizi tu.

Sasa tatizo linakuja kwa pale ambapo Mkuu wa upelelezi ametekwa na wenye uwezo kwenye Mji husika. Kuna wilaya katika nchi hii ambako Mkuu wa upelelezi amekaa hapo hadi miaka 8 sasa, na wengine walianzia kazi hapo akiwa askari wa chini hadi amekuwa Mkuu wa upelelezi au Mkuu wa traffic hapo hapo. Huyu ameshajulikana na kujenga ukaribu na wenye uwezo kifedha ndani ya Mji husika.

Tajiri au ndugu yake anapopata kesi dhidi ya mtu maskini hata kama askari mpelelezi ataandika haki kwenye jalada, mwamuzi wa mwisho ambaye ni Mkuu wa upelelezi eneo husika atapindisha maamuzi kwa faida ya tajiri akitarajia maslahi binafsi toka kwake.

Tutawalaumu askari wadogo bila kujua ugumu wanaokutana nao kwa mabosi wao ambao wameshajenga himaya za ukwapuaji. Kama wakuu wa Usalama barabarani na wakuu wa upelelezi wangekuwa watenda haki askari wa chini yao wasingeonea wananchi.

Inawezekana Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania akawa hajui hili maana si yote yanamfikia. Lakini namuomba aitishe uhakiki wa wakuu wa Usalama barabani na wakuu wa upelelezi waliokaa sehemu moja zaidi ya miaka 5 na wale wanaofanya kazi hapo hapo walipoanzia kazi jinsi walivyojenga himaya na kuwa chanzo cha lawama kwa jeshi la polisi. Uwezo wa kujisahihisha na kupunguza makemeo toka kwa Rais anao kama atadhibiti ujengaji wa himaya za wakubwa wa polisi nchini.

Jambo jingine analotakiwa kulifanya Mkuu wa Polisi ni kuweka watu waaminifu wanaopost hawa wakubwa. Kwa maelezo ya baadhi ya Maafisa wa polisi, nafasi nilizozitaja zinanunuliwa au zinalindwa kwa rushwa.

IGP akumbuke Mchelea mwana kulia atalia yeye. Mama akichoka ataona yeye hana msaada kwake na atajua atamfanya nini.
 
Ni wakati SSH ateue IGP mwingine, Tena awe mwanamke,

Kuna dada mmoja nilisikiliza clip zake akiwakemea polisi wala rushwa na waonevu, yule dada alifaa Sana kupewa u-IGP
 
ni wakati SSH ateue IGP mwingine, Tena awe mwanamke,

Kuna dada mmoja nilisikiliza clip zake akiwakemea polisi wala rushwa na waonevu, yule dada alifaa Sana kupewa u-IGP
Inaweza kuwa suluhisho kama atakayeteuliwa hatakubaliana na mfumo mbovu uliopo. Viongozi makini wanapoona mambo hayaendi sawa, wanaingia kazini wenyewe badala ya kuendelea kuamini wasaidizi wanaokuangusha. Bila kuwabana wakuu wa hivi vikosi na kusubiri askari wadogo wadogo wakosee ndo waadhibiwe huku wakubwa wakibaki bila kuguswa haitamsaidia. Atakuja IGP na atakuja tena na tena lakini polisi watabaki hivi hivi maana wanaoharibu wanabaki wanaondolewa wasionacho.
 
ni wakati SSH ateue IGP mwingine, Tena awe mwanamke,

Kuna dada mmoja nilisikiliza clip zake akiwakemea polisi wala rushwa na waonevu, yule dada alifaa Sana kupewa u-IGP
Tena hamchague muislam aweze kutenda haki
 
AUYZ3t.jpg
 
Sasa hivi wanawaponda lkn ukifika wkt wa uchaguzi ndio hua wanawategemea kuwaletea ule ushindi wa kishindo.
 
ni wakati SSH ateue IGP mwingine, Tena awe mwanamke,

Kuna dada mmoja nilisikiliza clip zake akiwakemea polisi wala rushwa na waonevu, yule dada alifaa Sana kupewa u-IGP
Hakuna kitu hapo,huyo dada sidhani hata Kama anafikia robo ya uadilifu aliokua nao Sirro kabla hajawa IGP.Sirro enzi hizo akiwa RPC Mwz aliwaambia serikali mtangazeni huyo mbunge wa upinzani aliyeshinda sisi hapa hatuna uwezo wa kuzuia watu wanaofanya vurugu huko nje ya ofisi za jiji na mbunge wa upinzani akatangazwa.Na baada ya hapo akapelekwa makao makuu kupigwa benchi(OP Maalum).

Alivyokuja kupewa uboss wa Police nadhani mnajua kilichofuata.Kule juu Ni kupokea maagizo na kutekeleza tu.
 
Ndo maana sijagusia nafasi yake na ubovu wake maana mengi yanajulikana. Nimeongelea tatizo la utendaji mbovu unaosababishwa na viongozi wa mchongo ndani ya traffic na CID.
 
Watanzania walio wengi wako hivi.: kila mteule anayeteuliwa wanapenda atoke, yaani hata kesho yake tu baada ya kuwa ameteuliwa. Hapa walipo wakisikia hata wateule wote wa Rais wamebadilishwa na kuwekwa wengine wapya kabisa, hapo sasa ndiyo furaha yao. Lakini kesho tena wateule hao hao wapya wanatakiwa watoke waingie wengine tena, unashindwa kuelewa hii ni vicious cicle ya namna gani inatakiwa ku-operate kwenye maisha ya viongozi wa Tanzania
Tumpeni nafasi mama afanye kazi, siyo kila mara mnashinikiza abadilishe viongozi. IGP Sirro atastaafu kwa cheo hicho na wala hataondolewa, na Mama ataendelea kufanya kazi siku zote huku akiwa na pamoja na Mungu. Mungu azidi kwenda na Mama kwa kishindo kikuu kama kile cha watu wanne waliokaribia kufa kwa njaa lakini kutokana na kishindo chao walipokuwa wanatembea, walisababisha kikosi kizima cha majeshi ya washami kuikimbia kambi yao na kuacha chakula tele kwenye kambi wakati wa njaa. Mungu azidi kwenda na Mama kwa kishindo cha aina hiyo
 
Kiujumla umepuyanga. Hivi huwezi kusoma na kuelewa kinachoandikwa ukapata cha kuchangia? Hoja yako kweli ina uhusiano na andiko langu? Hakuna mahali nilipomsema Sirro anatakiwa kujiuzulu, Hakuna nilipomlaumu Rais Kwa utendaji wake. Soma tena uone ulivyopuyanga.
 
Hi take it easy!. Kuna mtu niilisahau kum-quote, amepost hapo juu kabla yangu, ndiye nilikuwa namjibu na siyo wewe. Ubarikiwe na Bwana kwa ushauri
Post hii hapa #3
 
Back
Top Bottom