Jeshi la polisi linaposalimisha weledi wake kwa wanasiasa wa CCM

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
225
Hili jeshi letu la polisi limepoteza maadili kabisa kwa sababu limesalimisha weledi na mamlaka yake kwa wanasiasa wa CCM. na mara nyingi linapofanya hivyo linajikuta linaaibika. Mfano ni issue ya Mbowe ya madai ya 'kukwepa dhamana ya mahakama' na suala lile la Tarime kuhusu kutupa maiti barabarani.

Hata Igunga katika tukio la DC polisi wataaibika kwa sababu hatua wanazochukuwa dhidi ya CDM siyo za kiweledi, bali la maagizo ya wanasiasa wa CCM. Nasema kwa mfano ingekuwa ni kiongozi wa CDM ndiye angekuwa amefumaniwa, nadhani saa hizi angekuwa kisha kamatwa na kufikishwa mahakamani. Iko kazi kwkweli!
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,879
9,832
Hili jeshi letu la polisi limepoteza maadili kabisa kwa sababu limesalimisha weledi na mamlaka yake kwa wanasiasa wa CCM. na mara nyingi linapofanya hivyo linajikuta linaaibika. Mfano ni issue ya Mbowe ya madai ya 'kukwepa dhamana ya mahakama' na suala lile la Tarime kuhusu kutupa maiti barabarani.

hata la tarime polisi wataaibika kwa sababu hatua wanazochukuwa dhidi ya CDM siyo za kiweledi, bali la maagizo ya wanasiasa wa CCM. Nasema kwa mfano ingekuwa ni kiongozi wa CDM ndiye angekuwa amefumaniwa, nadhani saa hizi angekuwa kisha kamatwa na kufikishwa mahakamani. Iko kazi kwkweli!

Duh iko hii kisheria?
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Acha kulialia mwanaume! Hizo ndiyo gharama za demokrasia, muulize Raila Odinga wakati wa harakati zake na Moi.
 
Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,414
Hili jeshi letu la polisi limepoteza maadili kabisa kwa sababu limesalimisha weledi na mamlaka yake kwa wanasiasa wa CCM. na mara nyingi linapofanya hivyo linajikuta linaaibika. Mfano ni issue ya Mbowe ya madai ya 'kukwepa dhamana ya mahakama' na suala lile la Tarime kuhusu kutupa maiti barabarani.

hata la tarime polisi wataaibika kwa sababu hatua wanazochukuwa dhidi ya CDM siyo za kiweledi, bali la maagizo ya wanasiasa wa CCM. Nasema kwa mfano ingekuwa ni kiongozi wa CDM ndiye angekuwa amefumaniwa, nadhani saa hizi angekuwa kisha kamatwa na kufikishwa mahakamani. Iko kazi kwkweli!

Samahani, kuna mtu kafumaniwa huko!?
 
franksarry

JF-Expert Member
Nov 9, 2009
1,284
480
Umefika muda mwafaka wa kutenganisha kofia mbili!
ipo cku messenger wa CCM Lumumba au Dodoma HQ atapigiwa salute na kutoa maagizo kwa IGP na wengineo ktk Police Force!
 
kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
18,561
11,336
Police wapo kwa ajili ya kuwalinda CCM tu na si wengine,alafu cha ajabu wanalipwa mishahara kiduchu na makato ya kodi juu ka hela kote kanaishia tumboni, ndio maana police akiacha kazi au kuachishwa anaishia kuwa mlevi wa gongo.
 
kiroba

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
324
114
Hapa polisi wenyewe ndio wanatatizo. Iweje wewe polisi uliosoma na ukafuzu ukubali kutumiwa kwa manufaa ya mtu binafsi. Kwa kweli jeshi la polisi limeshuka sana hadhi kwani wamejiuza utu wao kwa bei ndogo sana.

Eti unapewa maagizo ya kipuuzi na wewe bila kuhoji unatii tu, huu jamani si ni ujinga usio na kifani. Amkeni acheni kutumika na wanasiasa. Tumieni taaluma zenu kukataa maelekezo na maagizo ya kipuuzi ya wana siasa uchwara waliokosa sera za kuwaambia wananchi.

Hapa polisi hukumu mnao ninyi wenyewe, kama mnataka muendelee kuonekana kama mboya basi ni juu yenu na kama mumekwishaona enough is enough basi chukueni hatua. Haswa ninyi polisi wenye vyeo vya chini. Elimishaneni mkatae kabisa kutmika kwani kwa kufanya hivyo mtakuwa mmekataa kabisa kudhalilishwa kwa utu wenu.

Mimi nadhani ninyi ni mabosi zaidi ya hao wanasiasa mnaowaogopa. Achaneni nao njooni kwa wananchi na sisi tutawalinda kwa gharama yeyote hata kama itabidi tuandamane kudai uhuru weni tupo tayari. Amkeni kwenye usingizi huo mliolala jamani.
 
mtolewa

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
729
518
jeshi la polisi badala ya kulinda raia na mali zao na hivyo kulinda haki limegeuka kuwa kikundi cha kulinda maslahi ya ccm na viongozi wake huku vikiikandamiza haki na demokrasia kwa malipo ya posho za oparesheni haramu na kuruhusiwa kula rushwa wazi wazi kutoka kwa wananchi wanyonge kama asante yao.JWTZ nayo imegeuka kuwa jeshi la watawala wa tanzania.bunge na mahakama navyo vimeuza uhuru wao kwa ccm na viongozi wake.TBC imegeuka kuwa tbccm huku PCCB nayo ikiwa kibaraka wa ccm na taasisi ya kubariki rushwa.
ni kwa sababu hiyo mimi binafsi nimeziasi taasisi hizi pamoja na Kanisa la DR. RWAKATARE kwani imeandikwa".................ukishindwa kabisa,uchukie moyoni na huo ni udhaifu wa imani"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom