Jeshi la Polisi linajua majukumu yake au bado tunafikiri kianalogia wakati tupo kidijitali

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,535
2,000
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba haifungamani na dini yeyote Kama inavyo ainishwa kwenye ibara ya 3 -,(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokirasia na ya kijamaa,isiyokuwa na dini,yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.

JESHI la POLISI Tanzania,linapokuja na tamko la kuzuia sherehe za itikadi za kidini mbali na kutengeneza kwa makusudi viashiria vya uvunjifu wa amani vinaingiza serikali katika mgogoro mkubwa wa kiimani ambao ibara ya 3(1) imetahadharisha.

Maanake nini!!!

Ni kutafuta chokochoko na minyukano isiyo na ulazima kwa kuwa serikali haina dini ila wananchi wake wana dini zao,na serikali in heshimu dini za wananchi wake.

Unapo wanyima watu huru wa kuabudu una vunja na kuikanyaga katiba ya Jamhuri ya Muungano. Ukizingatia ibara ya 19(2) cha katiba ya Jamhuri ya Muungano imetanabaisha kuwa kazi ya kutangaza dini,kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi,na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

Anapo simama msemaji wa JESHI la POLISI Tanzania,msomi Misime na kutoa tamko Hilo hakuzingatia mamlaka ya katiba Kama ilivyojieleza hapo juu!!!!!

Kwanini JESHI letu linashindwa kujitambua kwa kuendeleza double standard kwa kiwango hiki!!!

Nimsihi mwanasheria mkuu wa serikali kuwa makini Sana pale matamko ya Vyombo vya dola yanapo kiuka kwa makusudi matakwa ya kikatiba. Mambo haya yakiachwa hovyo hovyo mnacho kitafuta mtakipata.

Watanzania ni wapole,tusiwachokoze kwa kugusa imani zao,ukimya wao kwa kunyamazia mambo isiwe sababu ya kugusa au kuzuia imani za dini zao.

Nimsihi Misime arudi tena kwenye mics kuondoa tangazo lake kwa mustakabali wa huru wa kuabudu.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,286
2,000
Hao ndiyo maana wanaitwa policcm! Wapo kwa ajili ya ccm na viongozi wake. Na siyo kwa ajili ya kuwalinda raia na mali zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom