Jeshi la polisi limechafuka - liundwe upya kama JWT 1964 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la polisi limechafuka - liundwe upya kama JWT 1964

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 2, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Saidi Mwema akionyesha namna ya kulenga shabaha

  Yaliyotokea mwaka 1964 kukwama kwa jaribio la mapinduzi ya kumpindua Nyerere na kisha kuishia Nyerere kufanya mabadiliko makubwa (mapinduzi) katika JWT, Jeshi la polisi kwa sasa hakuna njia nyingine ila kufuata mkondo huo huo. Badala ya kulinda usalama wa raia na mali zao, jeshi hilo wengi wa waajiriwa wake wajihusisha na majambazi, kusafirisha biashara haramu, rushwa na uvunjaji wa sheria.

  Wengi wanaweza kufanya makosa kumhusisha Rais katika matukio mengi, lakini tujue kwamba mengi ya matukio hayo hata Rais pengine anashtukia tu, kwani majeshi yako huru katika system yake na hivyo walio juu ndio wenye kujitahidi kulinda maslahi binafsi kitu kinachochochea wa chini yake kufuata mkondo ule ule, nani wa kumnyooshea kidole wakati wote wanakula? Baba akiwa mwizi atamfunza mtoto kuwa mwizi na kujenga utetezi kwamba mtoto wake si mwizi hata kama akijulikana kwamba ni mwizi.

  Matarajio yetu ni jeshi la polisi kusaidia vita vya rushwa kinyume chake kadiri ya utafiti Jeshi hilo ndio linaloongoza kwa rushwa nchini Tanzania wakati ndio wenye kulinda sheria za nchi na
  raia.

  [​IMG]
  Jerry Muro alipoachiwa huru na mahakama ya Kisutu

  Jeshi hili limelalamikiwa kuwabambikizia watu kesi kama za yule mtangazaji wa TV ya taifa Jerry Muro alipowalipua kwanye vyombo vya habari kwa kupokea rushwa hadharani.
  Jeshi la polisi limevunja rekodi ya umwagaji damu badala ya kuokoa damu isimwagike kama mauaji ya Arusha, Mbeya, Mara, Pemba na machimboni.

  Mwakiembe alipoundiwa kundi la kumwangamiza na yeye kuja kutambua wanaomfuatilia na kupeleka taarifa polisi, jeshi hilo lilimtuma mmojawapo ambaye anahusuka katika tuhuma za kuwa katika jopo la wanaolinda majasusi wa kumwangamiza Mwakiembe kwenye kufanya mazungumzo ya kiutafiti kwa Mwakiembe. Mwakiembe alishalipua bomu hili na polisi hawajakanusha zaidi ya kupeleka jalada la kutaka kumshtaka Samwel Sitta athibitishe kwamba Mwakiembe alipewa sumu.

  [​IMG] [​IMG]
  Dr. Stephen Ulimboka hospitalini Mhimbili. Dr. Ulimboka akimkaribisha Pinda mkutanoni

  Tukio la Daktari kiongozi wa mgomo wa madaktari wenzake kutekwa na kupelekwa katika moja ya siri huku amefungwa usoni kwa t-shirt nyeusi asione anakoenda na baada ya umahututi kumpata wakamtelekeza msitu wa Mabwepande, kesho yake wamewapeleka walewale watesaji wake kwenda kumhoji mteswa ambaye mmoja wapo alitambuliwa na mteswa, wakati mwingine akagundulika akiongea kwa simu chooni kitendo kilichompa zawadi ya kichapo toka kwa wavaa vipima joto shingoni.

  Kitendo hicho kimekanushwa vikali na jeshi la polisi kwa kisingizio kwamba huyo alipelekwa kufanya upelelezi. Jambo la kujiuliza wakati waliomteka na kumtesa Dr. Stephen kama hawajulikani na upelelezi unaendelea, jeshi la polisi linawezaji kujenga utetezi dhidi ya aliyetambuliwa na mjeruhiwa kwamba amrudishie wallet yake na vitu vingine walivyomwibia?. Ni sawa na kuingilia kesi iliyo mahakamani kitu ambacho ni kinyume cha taratibu za kisheria, ndio usanii wa jeshi letu. Utaratibu wa mwathirika kumtambua mhisiwa au kumtuhumu mhusika ni jambo la kisheria ambalo jeshi halipaswi kujenga utetesi kwa vile jeshi la polisi hutumia njia hiyo hiyo kumtambua mtuhumiwa.

  Jeshi linawezaje kutoa utetezi huo kabla ya uchunguzi kuanza au ungali unaendelea kufanyika? Baadhi ya watuhumiwa wanatoka katika jeshi hilo tume ya uchunguzi inaweza kufanyika na jeshi nasita kuamini kwa vile dalili za awali zimeshaanza kujionyesha kwa viongozi wa jeshi hilo kuwatetea baadhi ya wanaotuhumiwa au kuhisiwa kuhusika katika tukio la kujeruhiwa Dr. Stephen.

  [​IMG]
  Abdallah zombe akipelekwa mahabusu kutoka mahakamani

  Tumeshuhudia mengi katika jeshi la polisi kwa kujenga utetezi dhaifu na pengine kuwa na hoja dhaifu kutetea watuhumiwa kutoka jeshi la polisi kama Zombe ili kushinda kesi kwa malengo ya kulindana. Kesi za Arusha dhidi ya vyama vya upinzani, kesi za CUF kule visiwani, kutupwa maiti barabarani na jeshi la polisi huko Mara kwa kutoa visingizio visivyo na kichwa wala miguu. Pinda kulidanganya bunge mara kadhaa kwamba uchunguzi unafanyika wakati sasa karibu zaidi ya mwaka hakuna kinachoendelea.

  Hii ndiyo serikali sikivu, huu ndio utawala bora tunaojisifia? Kuna kazi ambayo hata Rais inamwumiza kichwa, kwani mara moja nilikuwa masomoni USA, tukio moja la kuuawa kwa utatanishi mtumishi mmoja wa serikali kipindi cha utawala wa Mkapa, mama mmoja (jina kapuni) aliyekwenda kumtembelea mwanae aishiye Marekani, mama huyu ambaye yuko katika mfumo wa inteligensia alisema hata Mzee Mkapa mambo mengi hayajui, anashtukia tu ila inabidi atulize kichwa, kwani yanachanganya sana.

  Kuna haja ya kufanya mapinduzi makubwa katika mfumo wa jeshi la polisi, lakini mapunduzi ya mfumo huo si katika utawala wa CCM, kwani hata kama katiba ikiwa mpya wanaoendesha mfumo huo mbovu wakabaki walewale itakuwa ni kutupakaa mafuta kwa mgongo wa chupa.Fagio babu kubwa na kuweka kizazi kipya ndio itasaidia kuondoa uvundo ndani ya nyumba.
   
 2. N

  Njele JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uzalendo unapotangulizwa na ubinafsi matokeo ndio ya kila mwenye nafasi kufikiria manufaa yake dhidi ya anaowatumikia. Kuna haja ya kufanya mageuzi makubwa katika jeshi hili. Pamoja na Katiba mpya, lakini wananchi wawe na haki katika jeshi la polisi kama ilivyo kwa mataifa makubwa ya Ulayaa na Marekani. Wenye kuunda uchunguzi na kuwahoji polisi na wananchi, kwani kama kesi inawahusu polisi itakuwaje wajiundie uchunguzi wenyewe? Sawa na kumpelekea Fisi kesi ya kondoo.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Njele@ ni dhahiri wasimamizi wa sheria za nchi ndio wavunjaji wa kwanza wa sheria na kutetea uvunjaji wa sheria hizo kama ni sahihi kwa uwajibikaji wao. Hapa kuna tatizo.
   
Loading...