Jeshi la Polisi lijitazame na kujitathmini

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Kuna mambo ya msingi lazima tuyahoji kwa usalama wa taifa na watu wake,tukinyamazia kila jambo bila kulisemea tukisubiri rais atumie jicho la tatu kuona tutakuwa tumepoteza dira na mwelekeo.

Jukumu la usalama wa nchi ni la kila Mtanzania kwa kushirikiana na chombo cha dola chenye mamlaka ya kusimamia usalama wa raia wa nchi na watu wake. Jukumu hili likitekelezwa kwa weredi hakika hali ya amani itakuwa shwari na kila raia na hata wageni watakuwa salama pia.

Jukumu la usalama wa raia na mali zao lipo chini ya jeshi la Polisi,pamoja na mapungufu yanatokana na kurithi mfumo wa jeshi la kikoloni ambalo jukumu lake lilikuwa likitekeleza matakwa ya malkia ,limeshindwa kujinasua katika misingi ya kikoloni na kujikita katika ukinzani wa utekelezaji wa haki za binadamu hali inayotoa taswira kwa chombo hiki cha ulinzi na usalama kuwa kituo cha ukandamizaji wa haki kwa raia wake.

Marehemu Derefa aliyewahi kuwa mbunge wa Shinyanga mjini aliwahi kuishauri serikali ya awamu ya tatu kulivunja jeshi hili kulitoa katika mfumo wa kikoloni na kukifanya chombo cha umma kinachotekeleza majukumu yake kwa misingi bila upendeleo. Watu hawakumuelewa,waliona kama amekurupuka,lakini kumbe maoni yale yangefanyiwa kazi katika kulibadili jeshi hili matukio yanayotokea wakati huu yasingejitokeza kamwe.

Mathalani,mtu anatoa bastola hadharani mbele ya polisi tena mbaya zaidi na kamanda wa mkoa wa kipolisi akishuhudia bila hata kuchukua tahadhari kwa polisi wake kumkamata aliyetoa silaha ile,baada ya muda mfupi inatoka taarifa kuwa aliyetoa silaha ile si askari. Hoja hata kama angekuwa ni polisi,mazingira yale yaliruhusu kutolewa silaha ile hadharani kwa mujibu wa sheria na kanuni za matumizi na umiliki wa silaha.

Pamoja na mapungufu yaliyojitokeza kwenye tukio la mh. Nape kuzuiliwa kuongea na waandishi wa habari kwa kutishiwa silaha,bado jeshi hilo hilo lilishindwa kuchukua hatua katika kuzuia uhalifu mpya wa kutishia silaha wananchi wasio na hatia mpaka waziri mwenye dhamana alipomuagiza IGP kuhakikisha mhalifu huyo anakamatwa ndipo jeshi letu linastuka na kuchukua hatua,kwa tukio hili wananchi wanapata wapi imani kwa chombo hicho ikiwa kinatekeleza majukumu yake kwa upendeleo!

Ukilinganisha tukio la Nape,Ney Wamitego na RC wa Dar es sàlaam utaona jinsi gani jeshi letu lilivyopoteza mwelekeo na kuwa chombo kinachotekeleza majukumu yàke kinyume cha sheria kwa minajili ya kukitumikia kikundi fulani kuwakandamiza walio wengi wenye mtazamo unaokinzana na wachache hao.

Kutokana na mwendelezo wa matukio hayo yanayoigharimu serikali yetu sikivu kwa matumizi mabaya ya fedha za umma, kutumia madaraka ya umma vibaya na kupelekea chombo hiki kuwa kisababishi cha uvunjaji wa amani,IGP jitathimini na uwajibike.
 
Makonda ni Mtoto wa Baba kipnezi kabisa,hata afanyeje haoni,maovu ayafanyayo yanasababishwa na wauza unga.Hata alipovamia Clouds ni sababu ya wauza unga walimweleza akavamie.

Kununua vyeti ni wauza unga wamemwambia anunue.Kazi ipo.

Niko kwa ajili ya wanyonge lakini wanyonge hawa lazima wawe kutoka Home town aka USUKUMANI na lazima uwe mpendwa wangu
 
Nadhani katiba mpya ilikuwa ifunike mashimo kama haya, kama ingefanywa kwa malengo chanya.

Leo hii watu wanafanya kazi kama taasisi ya waimba kwaya.weledi haupo tena mpaka wanaonekana vituko mbele ya jamii.

Na hii niseme tu wazi, si polisi pekee,sababu yenyewe ni nyepesi kudhihirika kiutendaji.

Leo hii polisi hawezi kujibu maswali ya wakili, sababu tu haelewi nini anachosimamia/anachofanya.ilikuwa kazi rahisi kwao ila inakuwa ngumu sababu wameamua iwe hivyo.
 
Back
Top Bottom