Jeshi la Polisi lawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji Mtwara

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Jeshi la Polisi lawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji Mtwara

JESHI la Polisi mkoani Mtwara, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya waendesha pikipiki wawili waliotekwa na kuuawa wilayani Masasi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara, ambaye pia ni mkuu wa upelelezi wa mkoa, Leonard Makona, alisema baada ya kufanya uchunguzi juu ya matukio hayo wamewatia mbaroni watu watatu, wakazi wa Masasi.

Alisema jitihada za kuwakamata zilitokana na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na waendesha bodaboda baada ya vijana hao kuamua kuzunguka katika kila kijiji kuwasaka watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, hatimaye kuwakamata watatu.

Makona alieleza licha ya bodaboda hao kuwakamata watuhumiwa watatu na kuwafikisha katika kituo cha polisi cha wilayani Masasi, mwingine aliyetakiwa kukamatwa, alifanikiwa kukimbia, hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na bodaboda hao wanaendelea kumsaka.

“Tunawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji haya ya vijana wa waendesha bodaboda, tunatoa wito kwa bodaboda wenyewe kuwa na ushirikiano katika kuwabaini hawa wahusika kwani tukiwa kitu kimoja sisi na hawa bodaboda, matukio mengi ya wizi na kutekwa kwa waendesha bodaboda yatakwisha,” alisema Makona.

Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya waliokamatwa kwa maelezo kuwa watuhumiwa wengine wanaweza kutoroka.

Makona alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote, huku Jeshi la Polisi likiendelea na msako wa watuhumiwa wengine.

Mwishoni mwa wiki, zaidi ya waendesha bodaboda 100 Masasi waliamua kuwasaka wanaojiita ‘watu wasiojulikana’ ambao wanadaiwa kufanya matukio ya utekaji na mauaji kwa waendesha bodaboda watatu wilayani humo.

Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kuona ndani ya wiki mbili yakitokea matukio matatu mfululizo ya wenzao kuchinjwa kikatili hadi kufa na miili yao kukutwa imetupwa vichakani.

Watu hao wanaojiita wasiojulikana wamekuwa wakiwakodi bodaboda, kuwaua kikatili kisha kuondoka na pikipiki zao.

Mmoja wa waendesha bodaboda, Musa Rashidi, mkazi wa Kata ya Mkuti, alilieleza gazeti dada la Nipashe Jumapili kuwa wanasikitika kuibuka kwa matukio hayo ya kutisha na kutishia usalama wao baada ya wenzao watatu kuuawa ndani ya wiki moja.

Alisema pamoja na matukio hayo kutokea, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na vyombo husika.

“Sisi kama bodaboda kwa kweli tumeshtushwa na haya matukio ya wenzetu kuendelea kuuawa kikatili, hadi sasa wenzetu watatu wamekufa na pikipiki zao kuibiwa ndani ya wiki mbili mfululizo, sasa tunakwenda kila kijiji kuwasaka wauaji hawa,” alisema Rashidi.

Dereva mwingine John George, kutoka Kata ya Jida aliliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa matukio hayo, ili kuwabaini wahusika.

Naye Bakari Salumu wa Kata ya Napupa, alisema wanapofanya biashara ya kubeba abiria ni vigumu kwao kufahamu kama ni watu wema au wabaya.

Mbunge wa Masasi, Rashidi Chuachua, alisema amesikitishwa na matukio hayo na ameshamweleza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kuhusu hali hiyo.

Aidha, mbunge huyo alikutana na Kamanda wa Polisi wa Wilaya, Moshi Sokolo, na kumuomba afanye mkutano na waendesha bodaboda wote wilayani humo, ili kuwapa elimu kuhusu ubebaji wa abiria kwenye vyombo hivyo kwa kuchukua tahadhari.

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda wilayani Masasi, Idrisa Swalehe, alisema wanalaani matukio hayo ambayo yanawavunja moyo vijana walioamua kujitafutia ajira huku baadhi yao wakichukua mikopo ya kununulia vyombo hivyo.
 
Mimi ushauri wangu,hizi bodaboda zingeruhusiwa kuwa na dereva na mwenzake,ambaye atakuwa amepanda nyuma ya pikipiki,halafu pikipiki,iwe na 'side' car,ambayo imeshikizwa kwenye pikipiki, ndio atapanda abiria.Kwa hiyo abiria akiwa kwenye 'side car',hataweza kumtia kabari dereva wa pikipiki,halafu dereva wa pikipiki atakuwa na mwenzake,wa kusaidiana naye,pakitokea tatizo lolote.Au waendesha pikipiki,wangeunganishwa kwenye mfumo wa mtandao kama vile uber,taxify au mondo,ili anayetaka kukodisha awe amesajiliwa kwenye mtandao,na waendesha pikipiki,wasikubali kuchukuwa abiria,ambaye hajajisajili kwenye mtandao,kwa abiria wasiyemfahamu.
 
Back
Top Bottom