Jeshi la polisi latoa ufafanuzi wa kifo cha PC Suzana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la polisi latoa ufafanuzi wa kifo cha PC Suzana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Jul 29, 2010.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hivi hii timu ya uchunguzi hiko makini kweli? Repoti hii ya uchunguzi siamini kama imeandaliwa na jeshi letu la polisi na kama ni kweli basi tuna safari ndefu katika idara hii.

  JESHI LA POLISI LATOA UFAFANUZI WA KIFO CHA PC SUZANA

  Na Aron Msigwa – MAELEZO.

  Jeshi la Polisi nchini limesema kifo cha askari Polisi WP.7338 PC Suzana kilichotokea katika kituo cha Polisi Tarime tarehe 4/7/2010 kilitokana na tukio la askari huyo kujipiga risasi kifuani.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi Nchini ASP Advera Senso amesema askari huyo WP .7338 PC Suzana siku ya tukio hilo aliingia kazini asubuhi na baadaye kutakiwa kuelekea kwenye lindo kwa muda kuzuia magari yasiingilie msafara wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikuwa na ziara wilayani Tarime siku hiyo.
  Amesema siku hiyo msafara wa rais ulipofika alipokuwa PC Suzana uligawanyika gari la RPC Mara liliacha njia ya msafara na kuingia barabara ya Bomani kwenda ofisi ya DC likifuatiwa na magari mengine matatu likiwemo la Rais.
  ASP Senso amefafanua kuwa eneo ulipogawanyikia msafara kuna kilima na kona kali iliyosababisha RPC Mara kupotezana na magari yaliyokuwa mbele yake na hivyo kushindwa uelekeo wa msafara.

  “Mara baada ya kuona amepotea RPC wa Mara alisimama alipokuwa PC Suzana na kutaka kujua kwa DC ni wapi, akawaonyesha njia ya mkato ambayo haikuwa rasmi iliyopangiwa msafara” amesema.

  Amefafanua kuwa ilionekana PC Suzana alielewa kuwa RPC Mara alitaka kwenda Ofisi ya DC wakati yeye alitaka kuelewa njia ulipopita msafara. Baadaye RPC Tarime Rorya alimwagiza mkuu wa kituo Tarime apeleke askari mwingine eneo hilo na PC Suzana arudi kituoni umbali wa takribani mita 100 toka alipokuwa amepangiwa kazi.

  Amesema PC Suzana alipofika chumba cha mashitaka aliendelea na kazi, baadaye kwa kushirikiana na askari mwenzake PC Dora waliaadaa makabidhiano ya zamu na wakati wakiendelea kuandaa ghafla PC Suzana alichukua silaha moja kati ya mbili zilizokuwa kwenye sanduku na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa kituo na kufunga mlango.

  Amefafanua kuwa askari wengine waliokuwa kwenye chumba cha mashtaka walipoona hivyo walikwenda kwenye mlango alipoingilia PC Suzana na kujaribu kuuvunja ndipo akapiga risasi mlangoni na risasi hiyo kutoboa mlango kitendo kilichowafanya kurudi nyuma na baada ya muda walivunja mlango na kumkuta PC Suzana akiwa amejipiga risasi kifuani.

  ASP Advera amesema Jeshi la Polisi limechukua hatua za kiutawala na kuboresha mwongozo wa namna ya kusimamia misafara kwenye mikoa ya kipolisi yenye makamanda zaidi ya mmoja chini ya mkuu wa mkoa mmoja, mafunzo kazini na vyuoni kuhusu namna ya kukabilianma na msongo (stress Management).
  Hata hivyo amebainisha kuwa kifo cha WP Suzana ni suala linalohitaji uamuzi wa kisheria na jalada la tukio hilo limekamilishwa na kupelekwa ofisi ya wakili wa serikali kanda ya Ziwa kwa maamuzi ya kisheria.​
   
 2. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  mh...haya,ila ukweli ni taa,haujifichi milele
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ripoti imejaa uwongo na contradictions kibao ukilinganisha na maelezo waliyotupa mwanzoni.
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Stress what was the stress in this case? Tuambiwe hiyo stress ilikuwa kubwa kiasi gani mpaka binti wa watu ajiue.

  Silaha zilizokuwa kwenye kisanduku? Sitaku kuamini kama polisi wako careless namna hii kwenye utunzaji wa silaha za moto.

  Ofisi ya mkuu wa kituo, hiyo though ni public office lazima itakuwa ni private kutokana na unyeti wa Mkuu wa kituo. Sitaki vilevile kuamini kuwa Mkuu wa kituo anaweza kuacha wazi ofisi na funguo ikiwa ndani na kuondoka kwenda kupuyanga, kama ni hivyo huu ni uzembe wa hali ya juu.

  Inaonekana PC suzana alielewa: assumption kwenye kitu serious kama hiki, nani aliwaambia wakati PC SUzana is no more?

  Hadithi haijatungwa vizuri, utamu haujakolea leteni stori nyingine.
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi huu ni uchunguzi kweli? Hata wasiangalie family background? Uhusiano wowote wa mapenzi? Hivi siku zote hawakuwa na somo la stress management/ rehabilitation course kutokana na hiyo kazi yao kwani kuua ni nje nje!!!! Nafikiri huyo RPC ndiye anayehitaji leadership skills/ top management course!! Je, lugha iliyotumika kumwondoa pale kwenye lindo ni ipi? Hapa kwenye lugha jibu gumu kwani Suzana ni marehemu!!! Lugha ipi ilitumika kwa yule aliyekwenda kum-leave marehemu Suzana? Na kwa nini yule mwingine asingekuja kumuunga mkono Suzana? Hivi RPC mzima hujui barabara za wilayani? JK analiongeleaji hili suala?
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hii ndivyo UwT wanavyoandaa ripoti zao ili kuokoa JAHAZI. Hapo kwenye red ni sehemu ambazo zinahitaji ufafanuzi zaidi kwani zinatia shaka mno.

  wanatusikia na wanauma meno sasa..

  HATUDANGANYIKIIII. PC Suzana ameuliwa wala hajajiua. read between the lines.
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Kwani mlitegemea nini zaidi ya maelezo hayo?

  IGP alishatoa ufafanuzi toka day one!

  So this was basically "faking" the public:

  YANA MWISHO: RIP Susan
   
 8. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hii inanikumbusha report ya silaha za maangamizi pale UN wakati C. Powell alipokuwa anajitahidi kutetea uhozo wakati ndani ya nafsi yake anafurukutwa. Ukitizama news za jana, huyo kaimu msemaji wa jeshi la polisi alikuwa anakitetemeshi cha haja. Naomba kujua wajumbe walioshiriki katika tume hii ya 'uchunguzi'
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Watanzania wenzetu wenye uchu na madaraka na vibaraka wao, watawaua watanzania wenzao wengi tu ambao ni wazalendo wa kweli.

  Ila bahati njema ni kwamba hata hao wauaji hawataishi milele, sanasana wataishi kwa maluweluwe ya damu walizozimwaga.
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kwa nini DPP asishinikizwe chini ya sheria ya inquest Act

  18. Power of D.P.P. to order inquest
  The Director of Public Prosecutions may, if he considers it necessary or desirable in the public interest order that an inquest
  be held into the death of any person, and if a Coroner is so required by the Director of Public Prosecutions he shall hold an
  inquest into the cause of and the circumstances connected with the death of any person.


  Hii itaondoa ubishi kwani itakuwa more official kuliko kesi ya nyani kumpelekea ngedere, unategemea kitu gani??????
   
 11. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hii inanikumbusha enzi zile za Redio Tanzania na Mazungumzo baada ya habari, hahaaaa. Waache ujinga hawa nani wanamletea story.... Hizo risasi zilizopigwa mlangoni, hazikumjeruhi yeyote kati ya wavunjaji wa huo mlango? Awali tuliambiwa alijipiga risasi 4 kifuani, je mbona hicho kioja hawajakirudia tena? Na hiyo sero alomowekwa ndo hiyo ofisi ya RPC?

  Anyway hayo masimulizi mliyotuletea siyo nani kawapa, aliacha ujumbe?
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuweka hii habari chini ya thread za siasa kunaweza kufanya watu waijadili kisiasa. Better uipeleke kwenye habari za intelligence au habari nyinginezo.

  Kama ni kweli alijua inaweza kuwa ni suala la kauthirika kisakolojia au kuathiriwa kisaikolojia(Stress/streseds) kutokana na matukio yaliyofuata baada ya issue ya msafara wa mkuu.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Napenda kweli wanaposema "serikali imesema", "jeshi limesema", "Wizara imesema".. imekaa kiofficial kweli hata kama haina akili.
   
 14. A

  Adili JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,014
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Maelezo yote hayana kichwa wala mkia. Kama kuna aliyeelewa naomba anifafanulie.
   
Loading...