Jeshi la Polisi lataja wahusika wa mauaji Kibiti mkoa wa Pwani

Kajirutaluka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
1,224
995
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

JESHI la polisi mkoani Pwani ,limewabaini baadhi ya mtandao wa watuhumiwa wa mauaji yanayoendelea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji wapatao kumi na mbili akiwemo mwanzilishi wa mauaji Abdurshakur Ngande Makeo .

Aidha jeshi hilo linaendelea na msako kuwatafuta watu hao ambao wanne picha zao zimepatikana .

Akizungumzia hali ya kiusalama ya Mkoa kutokana na vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika wilaya hizo ,Kamanda wa polisi mkoani hapo,Onesmo Lyanga ,alisema wanaendelea na mapambano na upelelezi kuwapata wahusika wote .

Alieleza ,jeshi la polisi limewabaini kwa majina na picha kwa baadhi yao .

Kamanda Lyanga ,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni

  1. Faraj Ismail Nangalava
  2. Anaf Rashid Kapera
  3. Said Ngunde
  4. Omary Abdallah Matimbwa
  5. Shaban Kinyangulia
  6. Haji Ulatule
  7. Ally Ulatule
  8. Hassan Uponda
  9. Rashid Salim Mtulula
  10. Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri
  11. Hassan Njame

Kamanda Lyanga ,alieleza kwamba ,Saidi Ngunde inadaiwa anaishi Ikwiriri na Omar Abdallah Matimbwa anaishi Dar es salaam ambapo picha zao wanazo pamoja na ya Faraj na Anaf .

Alieleleza wengine nane bado picha zao hazijapatikana hadi sasa .

“Jeshi letu limebaini hayo kwa kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi ” alibainisha .

Kamanda Lyanga alisema ,watuhumiwa hao ,wamegundulika kuwa hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga ,kisiwa cha Saninga kijiji cha Nchinga .

Kamanda huyo ,alifafanua kijiji kingine ni cha Mfesini kata ya Nyamisati na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti ,Rufiji na Mkuranga.

Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa siri kufichua watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama kimkoa .

Limetangaza bingo ya kumpatia sh. mil .tano yeyote atakaefanikisha zoezi hilo

Hivi karibuni jeshi hilo lilitangaza kuwa kuna mtandao wa majina ya wauaji 102 ambao wanawasaka hadi sasa ili kudhibiti vitendo vya mauaji vinavyotia hofu wananchi.





d23a3356bd20fd54f8a0a75bb0b7b760.jpg

f756162d50a56ef109e6eee210179ddd.jpg
 
Duh, yangu macho na masikio ili kuona na kusikia kwamba amani inapatikana na wahalifu wanadhibitiwa!
 
Back
Top Bottom