Jeshi la Polisi lasema askari aliyejinyonga alikuwa peke yake mahabusu

Inasikitisha sana!

Mzee Mwinyi akiwa Waziri wa mambo ya ndani alijiuzulu katika mazingira kama haya ya Mtwara!
Ikibidi kila askari akifanya kosa anajiuzulu waziri wa mambo ya ndani, mbona SSH atachoka kuteua mawaziri wa ndani.
 
Sasa huyo aliyeweka vitu ambavyo mahabusu anaweza kujinyonga ni nani?
Alifanya kwa bahati mbaya au makusudi?
Au walikula mchongo kwamba kifaa hicho kiwekwe ili mtuhumiwa ajinasue kupitia kifo?
Aliyekufa ameondoka lakini waliomuweka mahabusu nao wawekwe mahabusu hapo kuna ajenda ya siri.
Waliowahi kufika mahabusu wanajua maana hata mkanda wa suruàli huvai iweje matambara?

Maswali ni mengi sana kwenye hili waliohusika nao nibora wakawekwe selo yenye mapanga na majembe wajikadirie huko,wasiachwe
Nyie wote mnahangaika bure. Hii pesa ilipopigwa kulikuwa na mgao toka wahusika kwenda juu. Ndiyo maana yaliizima na kutaja kiasi kidogo kuliko kiasi halisi. Baada ya mambo kupamba moto, wakaona hili kaa la moto kulizima ni lazima mmoja anyongwe, alafu asingiziwe kuwa ndiye aliyehusika na unyang'anyi wa pesa na na mauaji. Mtuhumiwa alitundikwa na kunyongwa mpaka kufa. Wakuu sasa wanachekelea na mgao, maana kila kitu kasukumiwa marehemu polisi.
 
Acheni utoto, yeye awekwe peke yake halafu yeye huyo huyo ndio ajinyonge? Hiyo ni Conincidence ya namna gani? Tunataka familia ya marehemu wapewe hizo picha na taarifa za kiuchunguzi ili wajiridhishe.
"Tunataka" ww na akina nani?
Sishabikii polis ila utangoja sana ..hilo unalotaka lifanyike
 
Hawa polisi ni watu waajabu kweli..

Waeleze vitendeaa kazi alivitoa wapi?

Hapa waziri atumie akili hawa panya washughulikiwe chapu
 
Back
Top Bottom