Jeshi la Polisi lapiga marufuku mikusanyiko kwenye sikukuu ya Eid

Hulda-Tamarri

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
415
250
Hii tahadhali inahusu tz yote, ila watu wa Dar mnaweza kubaki na disko lenu kama rais wenu alivyowaambia. Sisi wa mikoani wacha tufuate maelekezo kutoka jeshi la polisi, tusherehekee kwa amani na utulivu.

AFYA YAKO NI JUKUMU LAKO MWENYEWE, 👈 ndilo la msingi.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,630
2,000
Kuna mambo tunafanya kama ''fashion'' si kwa kusudio lake

Kuzuia mikusanyiko kuna maana ya kuzuia maambukizi miongoni mwa waliokusanyika.

Sasa unazuiaje watu wasikusanyike wakati wa Idd ikiwa walikusanyika katika misikiti '' chumba kikuubwa cha kusalia'? hii haina mantiki kabisa. Ni sawa na kujisetiri na ''kitambaa upande wa mbele ukiacha mwingine wazi''

Kosa lile lile la kufunga shule na vyuo na kuacha wazi misikiti na makanisa. Hakuna mantiki kabisa

Tunafanya mambo kiasi cha wenzetu kujiuliza, hivi hili Taifa lina wasomi ?

JokaKuu Pascal Mayalla jmushi1
 

NJOLO

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
504
500
Ifike mahali maagizo ya Mh. Rais yafuatwe ili Wanainchi wasipotoshwe.
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania aliagiza kuwa wasemaji wa maswala ya Corona ni Waziri wa, Afya, Msemaji mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu. Msemaji mkuu ni Yeye Rais.
Rais ameagiza watu waendelee na shughuli zao kama kawaida. Wanafunzi wa chuo KIkuu kama UDOM ambao wanafikia jumla ya 40,000 wameambiwa warudi chuoni na wakakusanyike. Huu ni mkusanyiko mkubwa sana. Hakuna sababu kuzuia watu 20 au hata 50 ambao ni marafiki na ndugu kukaa pamoja lakini ukaruhusu watu 40,000 wasiofahamiana kukusanyika.
Kuna kila dali dali baadhi ya Taasisi zilitaka kuwe na lock down ili wapate mwanya wa kuwatesa watu ambao hawatatii amri hiyo kama ilivyofanyika Unganda na Rwanda.
Huu ugonjwa tumeuzoea na tiba tunaifahamu.
Watu wanakutana, wanapeana mbinu mbali mbali za kupambana na ugonjwa.
Katika hili tumefanikiwa sana na maambukizi yamepungua kwa sababu watu wanaruhusiwa kukusanyika na kupeana ushauri.
Haiwezekani kukawa na vita lakini askari wakafungiwa ndani kwa sababu ya kuogopa kufa.
 

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
1,929
2,000
Sasa yule alotuaminisha kufanya fujo na kupiga kelele si akamatwe? Mnatuchanganya tu sisi.
 

Junior Nicky

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
432
500
Vidonge vya rangi mbili...hii nchi bana kila mmoja ana kauli juu ya mwenzake.

Ila Sirro atajishusha maana akikumbuka lile sakata la shisha makonda alivyomuandama hahahaha....mm na bet J2 watu wanalimwaga sebene kama kawa wakishehereka(Dar corona festival)

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,538
2,000


Jeshi la polisi limesema kuwa sikukuu ya Eid el Fitri itasherehekewa huku dunia ikiwa imekumbwa na ugonjwa wa Corona, hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Msemji wa jeshi la polisi, David Misime imeeleza kuwa jeshi polisi linatoa wito na msisitizo mkubwa kwa Watanzania kusheherekea huku wakizingatia kimamilifu maelekezo yaliyotolewa na yanayoendelea kutolewa na viongozi wakuu na wataalamu wa afya ya namna ya kujikinga na Corona.

“Tuna uhakika kila mmoja kuzingatia maelekezo hayo kuanzia ngazi ya familia mafanikio makubwa ambayo tumeanza kuyapata katika kukabiliana na ugonjwa huu nchini kwetu ,” amesema.

taarifa hiyo imeeleza kuwa jeshi la polisi halitegemei na halitarajii kupambana na watu kutokana na kukiuka maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya Corona.

“Tunategemea kila mmoja kwa nafsi yake kuthamini maisha yake na kufuata maelekezo, hivyo hatutegemei watu kuwa katika mikusanyika isiyo ya lazima kama viongozi na wataalamu walivyoelekeza na hata viongozi wa dini watakavyowaelekeza,”

Aidha, wakati wa sherehe hizo jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inakuwa ni ya uhakika na kwamba waumini wa dini ya Kiislamu na Watanzania wote wanasherehekea katika mazingira ya amani na utulivu
Iko wapi hiyo taarifa?
Haya ni maneno yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom