Jeshi la Polisi lapiga marufuku mikusanyiko kwenye sikukuu ya Eid

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
46,565
2,000
Kamanda Sirro anataka kutuharibia sherehe ya maazimisho ya kilele cha korona iliyopangwa kufanyika jumapili hapo Dar
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
2,506
2,000
jeshi la polisi limekumbusha raia kuzingatia kanuni za kujikinga na corona kipindi hiki cha skuku ya idi.
jeshi limekumbusha tu.
ila buzuki la jpili lipo palepale mpaka kuchere

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
6,377
2,000


Jeshi la polisi limesema kuwa sikukuu ya Eid el Fitri itasherehekewa huku dunia ikiwa imekumbwa na ugonjwa wa Corona, hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Msemji wa jeshi la polisi, David Misime imeeleza kuwa jeshi polisi linatoa wito na msisitizo mkubwa kwa Watanzania kusheherekea huku wakizingatia kimamilifu maelekezo yaliyotolewa na yanayoendelea kutolewa na viongozi wakuu na wataalamu wa afya ya namna ya kujikinga na Corona.

“Tuna uhakika kila mmoja kuzingatia maelekezo hayo kuanzia ngazi ya familia mafanikio makubwa ambayo tumeanza kuyapata katika kukabiliana na ugonjwa huu nchini kwetu ,” amesema.

taarifa hiyo imeeleza kuwa jeshi la polisi halitegemei na halitarajii kupambana na watu kutokana na kukiuka maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya Corona.

“Tunategemea kila mmoja kwa nafsi yake kuthamini maisha yake na kufuata maelekezo, hivyo hatutegemei watu kuwa katika mikusanyika isiyo ya lazima kama viongozi na wataalamu walivyoelekeza na hata viongozi wa dini watakavyowaelekeza,”

Aidha, wakati wa sherehe hizo jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inakuwa ni ya uhakika na kwamba waumini wa dini ya Kiislamu na Watanzania wote wanasherehekea katika mazingira ya amani na utulivu
Kwa hiyo sebene na fiesta la Makonda ndo itakuwaje?
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,450
2,000
Sasa hapo ndio ngoma inaanza, nani kidume. RC Makonda hivi sasa katangaza tenda ya kutafuta DJ bora wakushusha magoma Beach katika Corona Festival halafu anakuja kiongozi wa idara ya CCM iitwayo Policcm eti hakuna?
Ndio atajua yeye Makonda ana uhusiano gani na #1 katika kipande hichi cha dunia. Hata hivyo Sirro ajiandae kuaibika na yote hiyo ni kwa sababu hakuna utamaduni wa kuachia usiposikilizwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom