Jeshi la Polisi lapewa siku 7 liwe limepeleka mikataba kamati ya Bunge, PAC

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imelipa siku saba kuanzia jana Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi, iliyopewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima.

Hadi sasa kampuni hiyo imeshalipwa asilimia 99 ya fedha, ilihali vituo vilivyofunga mashine hizo ni 14 kati ya 108.

Maagizo ya kamati hiyo yaliyotolewa jana Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilal wakati kamati hiyo ilipokutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Aeshi alisema jeshi hilo mwaka 2011 liliingia mkataba na Kampuni ya Lugumi Enterprises kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima ambavyo viko 108.

Alisema mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote ili hali vituo vilivyofungwa mashine hizo ni 14 tu, kati ya vituo vyote 108.

“Ukiangalia kazi iliyofanywa tangu mwaka 2011 hadi leo ni kidogo na pesa hawa kampuni wameshachukua asilimia 99, sasa tumewaagiza watuletee huo mkataba ndani ya wiki moja walioingia na kampuni hiyo ili tuupitie,” alisema Aeshi.

Kuhusu mali zinazokamatwa na polisi kwenye matukio mbalimbali nchini yakiwemo ya wizi, Kamati imewaagiza CAG, Polisi na Mhakiki Mali wa Serikali kufanya ukaguzi wa mali zote zinazokamatwa na polisi ili kuzifahamu kuzipa thamani halisi kulingana na idadi yake.

Alisema hivi sasa mali zinazokamatwa na polisi hazifanyiwi uhakiki kujua idadi na thamani yake hivyo nyingi zinapotea bila kujua zilipokwenda na nyingine ambazo kesi zake zimeisha, zinauzwa kwa bei ndogo kuliko thamani halisi.

Kuhusu maduka ya bidhaa ya majeshi nchini, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeiomba serikali idhini ya ukaguzi na utoaji mizigo ya maduka ya jeshi bandarini ufanywe na jeshi hilo badala ya utaratibu wa sasa ambao mzabuni ndiye anayesimamia jambo hilo.

Akizungumzia hilo, Aeshi alisema maombi hayo ya jeshi yalitolewa wakati kamati hiyo ilipokutana na JWTZ juzi na kuomba ukaguzi wa bidhaa zinazoagizwa kwa ajili ya maduka yao zifanyiwe ukaguzi na wao kwani inawezekana bidhaa zinazoingizwa zikawa nyingi au zikachanganywa na vitu vingine kwa kuwa wao hawana dhamana ya kukagua.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Ernest Mangu alisema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile uhaba wa nyumba na kwamba mikakati yao hivi sasa ni kufanya mabadiliko na kulifanya jeshi hilo liwe la kisasa zaidi.
 
Inaonekana nchi hii iikuwa ya wachache dhidi ya wengi.
 
duu tufanye zinazotakiwa ziwe 30 ndio hayo mabilioni yaani moja bilioni moja...kweli bongo watu wanatafuna kodi zetu kuna muda nikimsikiliza kayombo wa TRA naona nae ndio wale wale tuu..elimu kwa walipa kodi sawa mbona Elimu kwa wanaotumia hamna..
 
Kwenye majeshi yetu ndiyo kuna madudu mengi sana, waishie jeshi la polisi na magereza, JWTZ wasijaribu wasije kutuingiza kwenye matatizo
Mkuu MKWEPA KODI sisi tunaombea waishie hukohuko Polisi...JWTZ yetu watuachie kabisaaa,hatutaki kuchinganishwa na Jeshi letu la Wananchi
 


Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma(PAC) chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni mbunge wa S'wanga Mjini Mheshimiwa Haeshi,imenusa harufu ya ufisadi mkubwa ndani ya jeshi la polisi baada ya kampuni iliyopewa zabuni ya kusambaza mashine za kusomea alama za vidole(Finger Print) kushindwa kufanya hivyo licha ya kiasi kikubwa cha pesa kilichotolewa na serikali.

Kampuni hiyo ya lugumi inasemwa kupewa zaidi ya bilioni 30 ili iweze kutoa mafunzo kwa askari ya jinsi ya kutumia mashine za kusoma alama za vidole na pia kufunga mashine hizo ktk vituo vyote vya polisi Tanzania.Uchunguzi mdogo uliofanywa na PAC umegundua kuwa licha ya serikali kutoa zaidi ya bilioni 30 kutekeleza mradi huo na pesa kuonekana kutumika,kampuni hiyo imefunga mashine hizo katika vituo vya Polisi 14 tu Tanzania nzima,huku baadhi ya vituo mashine hizo kuwepo bila kuwa na polisi wenye ujuzi wa kuzi-operate na hata katika vituo vingine mashine hizo kuwepo tu kama mapambo baada ya kuwa zimeharibika.

Kampuni hiyo ya lugumi ilipewa kazi ya kununua mashine hizo na kusambaza katika vituo vikubwa vya Polisi nchi nzima na pia kutoa mafunzo kwa maafisa wa Polisi watakaotumika kuendesha mashine hizo.Mwaka 2013 mradi huo ulitakiwa kuchukua maafisa wa polisi wawili kila Wilaya ili kutoa mafunzo hayo kwa vitendo kwa muda wa week mbili,licha ya maafisa hao kupewa mafunzo na baadhi "kupunjwa" hata pesa za posho za mafunzo hayo,mpaka sasa hakuna mashine zilizopelekwa katika vituo hivyo kuanzia walayani mpaka mkoani,zaidi ya hizo mashine 14 ambazo nazo hazina ufanisi wowote.

Lengo la mradi huu ilikuwa na kuviwezesha vituo vya Polisi vya Wilaya na Mikoa kuwa na uwezo wa kusoma alama za vidole kwa mambo ya kiusalama,serikali iliamua kufanya hivi ili kupunguza msongamano wa huduma hiyo katika makao makuu ya Polisi tu.

PAC imemtaka Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kuufuatilia mradi huu na kuugagua na kutoa ripoti itakayoibua mianya ya rushwa na ufisadi wa namna tender ilivyotangazwa na kushinda,ili wale wote waliohusika na kashfa hii wajulikane na kutambulika.

Hii kampuni ya Lugumi Interprises imekuwa ikisemwa kwa kuhusika na ununuzi wa vifaa vya kijeshi vya polisi kwa muda mrefu,kampuni hii ipo Jengo la ATCL Posta mkabala na PPF Towel,na habari zisizo rasmi ni kuwa Mr Lugumi mmiliki wa kampuni hii ni mkwe wa kigogo mmoja mstaafu wa Jeshi la Polisi aliyekuwa na cheo cha juu katika Jeshi la Polisi la Tanzania

Kampuni hii pia inamiliki KZ Security ambayo ni kampuni Tanzu ya Lugumi inayojihusisha na mambo ya ulinzi katika ofisi za Serikali na zile za binafsi.

Kuifahamu zaidi kampuni hii na wamiliki wake(Associates) gonga hapa lugumi

Kwani ni polisi kweli au ni genge tu la CCM ni tawi la CCM. nchi CCM wameivuruka vibaya sana
 
Mkwe wa kigogo mmoja mstaafu ? Inaweza kuwa pia Mkwe na Mtoto wa kiume wa huyo kigogo wana ubia kwenye kampuni hiyo ya ulinzi ,nilipata kusikia sehemu mtoto wa kigogo huyo anahusika na kampuni ya ulinzi

Kigogo mwenyewe sio yule aliyeibiwa sijui nini ya Gold ofisini kwake ?? Kwanza ilishapatikana ?
 
image.jpeg
image.jpeg


Mkuu UncleBen fuata hiyo link hapo aliyotoa mtoa mada.Nimekutana na mambo mazito.Eee Mungu iokoe nchi hii inaangamia
 
Kwenye majeshi yetu ndiyo kuna madudu mengi sana, waishie jeshi la polisi na magereza, JWTZ wasijaribu wasije kutuingiza kwenye matatizo
Hakuna mwamba wala jiwe juu ya jiwe kitakalosalia.wewe kama unaogopa matatizo hama nchi tu, maana hamna namna tena.

Huu sio mda wa kuchekea wapuuzi.
 
Mkuu MKWEPA KODI sisi tunaombea waishie hukohuko Polisi...JWTZ yetu watuachie kabisaaa,hatutaki kuchinganishwa na Jeshi letu la Wananchi
Jeshi letu la wanachi kama lina chawa kazima litamwagiwa tu maji ya moto na kuanikwa juani.kwa kuhifadhi wajinga wachache ni kurutubisha uraniam ambayo mwisho wake...........

Askari hawagomi, umeishawahi jiuliza wakichoka kuvumilia wapuuzi wachache nini kitafuata???
 
Ila lile la Lugumi liko wazi! Baada ya wale CP kuondoka pale nikajua mchezo uko wazi sasa! Ubay nasikia Boss wa Zamani wa Mlowola nae a kashfa yake kwenye uniform baa kujiona mjinga wenza wote wako kwenye payroll na partnetship na Lugumi! Takukuru malizeni kazi na Lugumi! Ana siri nzito hadi yal magari ya police yanaitwa Leyland! Maajabu! Vile vigali vitamfukuza landcruiser kwenye rough road kweli? Mwaka huu tunaomba uhai tu!
 
Atumbue Mpaka Mwili Mzima Ujae Makovu Tujue Moja Kuwa Wote Wameoza Na Kupungukiwa Utukufu Wa Mungu.
 
Back
Top Bottom